Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, September 2, 2011

CWT Mbeya waanza mkwara kwa serikali



CHAMA cha walimu (CWT) mkoani Mbeya kimetishia kuitisha mgomo iwapo serikali itaendelea kupuuza madai ya walimu ya jumla ya shilingi 2,755,035 ,283 wanayodai yakiwa ni malimbikizo ya kipindi cha kuanzia mwaka 2007 hadi 2011.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa CWT mkoani hapa Kajuni Nelusigwa madai hayo ni ya malipo ya Uhamisho,likizo,Matibabu,Walimu kwenda masomoni,Mapunjo baada ya kupandishwa madaraja pamoja na fedha ya kujikimu kwa ajira mpya.

Nelusigwa ametoa tamko hilo alipozungumza na waandishi wa habari ambapo alibainisha kuwa madai ya mapunjo ni ya walimu 1509 wanaodai 2,373,626,179, uhamisho  walimu 160 wanaodai shilingi 302 ,417,384  na walimu 143 wakiwa wanadai 39,056,200 za likizo.

Aliongeza kuwa walimu 85 wanadai shilingi 21,511,010 za masomoni,36 wanadai shilingi 16,688,510 za malipo ya kijikimu na watano wanadai shilingi 1,736,000 fedha kwaajili ya matibabu.

Mwenyekiti huyo pia alisema yapo pia madai ya walimu kupandishwa daraja ambapo jumla ya walimu 1964 hawajapandishwa madaraja wanayostahili kwa muda mrefu.

Aliitaka serikali kulipa malipo hayo kwakuwa ni halali ili kuleta tija katika utendaji wa walimu vinginevyo watatangaza mgogoro baina yao na serikali utakaopelekea mgomo aliouita kuwa wa kihistoria.

Hata hivyo alitoa mwito kwa walimu wanaodai fedha hizo kuendelea kufanya kaazi kwa kujituma katika kipindi hiki ambacho uongozi unashughulikia madai yao.

1 comment: