URASIMU na rushwa vimetajwa kuwa changamoto kubwa
inayokwamisha mfumo wa stakabadhi ya mazao gharani licha ya serikali kulipa
uzito suala hilo.
Katibu Tawala Msaidizi uchumi mkoa wa Mtwara Shangwe
Twamala aliyasema hayo jana jijini Mbeya alipokuwa akitoa mada ya Mfumo wa Stakabadhi
ya Mazao Ghalani kwa washiriki kutoka halmashauri zote za wilaya mkoa wa Mbeya.
Twamala alisema mkoa wa Mtwara uliokuwa wakwanza
kutumia mfano huo katika zao la Korosho umekumbana na vikwazo vingi katika
utekelezaji wa mfumo na kutaja moja ya vikwazo hivyo kuwa ni rushwa inayotolewa
na wanunuzi waliokuwa wakiwanyonya wakulima wa zao hil
Alitolea mfano kuwa kuna wakati wafanyabiashara hao
walichanga pesa na kuwahonga madereva wa malori yaliyopewa kazi ya kusafirisha
gunia tupu kutoka Dar es salaam hadi mkoani hapo kwaajili ya kuhifadhia zao
hilo na kuwataka wazicheleweshe kwa kulala njiani.
“Waliwahonga madereva wa malori wakiwataka wawe na
vituo vingi vya kulala ili wakulima waone mfumo huu haufai na kuamua kuuza
korosho kwa wafanmyabiashara vwa siku zote.Ilitubidi tukaongea na makamanda wa
polisi wa mikoa yote ya njiani kuwaomba wasiruhusu gari hizo zilale njiani
ndiyo tukafanikiwa” alisema.
Nao uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kyela
ulisema urasimu katika utoaji wa leseni za usajiri wa Maghala umesababisha
kushindwa kwa mfumo huo msimu huu ambapo ilitarajiwa mfumo huo utumike kwa
mazao ya mpunga na korosho lakini mpaka sasa maghala waliyonayo hayajasajiriwa.
No comments:
Post a Comment