Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, September 2, 2011

RC awawakia madiwani kutaka posho bila kukusanya kodi


MKUU wa mkoa wa Mbeya John Mwakipesile amewataka madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya kushirikiana na watendaji wa halmashauri hiyo kuweka mikakati ili kuongeza tija katika ukusanyaji mapato hali itakayoipunguzia utegemezi kwa serikali kuu.

Mwakipesile amelazimika kuyasema hayo katika kikao maalumu cha baraza la madiwani  ambapo imebainika kuwa bajeti ya halmashauri hiyo ni tegemezi kwa serikari kuu kwa asilimia 97 hivyo inachangia kwa asilimia tatu pekee.

Mkuu huyo wa mkoa amesema hali hiyo inatokana na madiwani pamoja na watendaji  halmashauri kubweteka huku wakiendelea kumtaka mkurugenzi awalipe posho kwa kila kikao wanachokaa pasipokujua fedha zinatoka wapi.

“Huo nao ni ufisadi kwakuwa mnalipana posho kwa fedha mnazopewa bure.Mlipaswa kuhakikisha mnaongeza kasi katika ukusanyaji wa kodi ndipo mdai posho zenu.Mepewa ardhi,watu na sheria kwa nini mnashindwa kuzalisha.Mnabweteka kwa kujua mtapata tu fedha.Ipo siku serikali itaamua kufuta ahlmashauri zote zisizo na uwezo wa kujiendesha sijui mtakuwa wapi”

Aliishangaa halmashauri hiyo kuwa na mapato kidogo licha ya kuwa na vitega uchumi vingi lakini inashindwa kuchangia katika pato la taifa na kuwataka wahusika hao kwenda katika halmashauri nyingine kwenda kujifunza ni jinsi gai wanakusanya ushuru.

Alisema zipo halmashauri nyingi zikiwemo za Jiji la Mbeya,Rungwe na Mbozi ambazo awali zilikuwa zikikusanya kodi kidogo lakini kwa kujituma kwa madiwani ambao walifikia hatua ya kuanza kusimamia wenyewe mapato katika kata zao hivi sasa zinafanya vizuri.

Ameutaka uongozi wa halmashauri wa halmashauri hiyo kuona uchungu kwa kuanzia kupiga hesabu ya gharama inayotumia fedha za serikali kuwalipa watumishi katika kata na kujiuliza kata husika inachangia kiasi gani mapato.


No comments:

Post a Comment