Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, September 23, 2011

TUCTA Mbeya wapongeza uchaguzi wao taifa,Waonya


SHIRIKISHO la vyama huru vya wafanyakazi TUCTA mkoani Mbeya limetoa saalamu za pongezi kwa viongozi wapya washirikisho waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika septemba 15 mwaka huu mjini Arusha.

Kaibu katibu wa TUCTA mkoani Mbeya Thomas Kasombwe akizungumza na gazeti hili amesema kuchaguliwa kwa mara nyingine kwa mwenyekiti shirikisho hilo Omary Ayoub na katibu Nicholaus Mgaya kunadhihirisha jinsi wanashirikisho walivyo bado na matumaini na uonmgozi wao.

Kasombwe alisema tawi la Mbeya linatambua mchango wa viongozi hao katika kupigania maslahi ya wafanyakazi kwa waajiri wao hivyo wanaamini kuwa mikakati waliyoianzisha kwenye kipindi kilichopita wataiendeleza katika uongozi huu.

Hata hivyo alisema nguvu zaidi ya ushirikiano katika utendaji inahitajika ili kufikia malengo ya utatuzi wa changamoto zinazowakabili wanachama wa vyama vya wafanyakazi hivyo ni vema wakafanya kazi kwa bidii.

Kaimu katibu huyo aliyataja mabo ambayo uongozi huo mpya ni vema wakaanza naayo kwakuwa yapo mezani kwao kuwa ni pamoja na kuendelea kuihimiza serikali kuongeza kima cha chini cha mishahara kutoka 150,000 cha sasa na kufikia 315,000.

Changamoto nyingine ni serikali kupunguza kiasi cha kodi kwa wafanyakazi kwa asilimia 9 au 10 kabisa badaala ya punguzo la asilimia moja lililotangazwa na serikali hivi karibuni.

Alisema ni vema pia uongozi wa shirikisho ukakaa pamoja na serikali na kujadili ni jinsi gani itaweza kutatua tatizo la mgawo wa umeme kwa haraaka pamoja na kushusha bei ya nishati hiyo muhimu katika maendeleo ya jamii.

“Tunatambua sote kuwa kukosekana kwa umeme wa uhakika kwa kiasi kikubwa kunayumbisha uchumi wan chi yetu.Waananchi wanashindwa kuzalisha,viwanda havifanyi kazi ipasavyo na hiyo inasababisha hata serikali kukosa kodi.Lakini hata utakapopatikana umeme wa uhakika tungependa bei yake ishuke ili isiwaumize watanzania” alisema

Alisema suala jingine ni kutokuwepo na utaratibu maalumu unaoongoza kupanda na kushuka kwa mafuta hali inayozusha mgongano wa mara kwa mara baina ya wadau husika hali inayopaswa kuisimamiwa na uongozi wa shirikisho kusaiduiana na serikali kupata ufumbuzi wake.

No comments:

Post a Comment