Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, May 26, 2015

HAPA NDIPO TUNAPOANZIA KUPOROMOSHA MAADILI YA JAMII YETU



KATIKA kipindi cha miaka ya zamani Ualimu ulikuwa wito.Ni kutokana na hali hiyo watu walioajiriwa kwenye tasnia hiyo walikuwa wenye staha kulingana na walivyofundishwa chuoni.

Uwepo wao katika kundi lolote ndani ya jamii uliwatofautisha na makundi mengine.Walionekana watu wenye kutegemewa na jamii kwenye masuala ya ushauri na hakika jamii iliyowazunguka ilinufaika na uwepo wao.

Walimu katika miaka hiyo hawakuishia kufundisha wanafunzi darasani,walifundisha jamii yote.Palipotokea na jambo jamii ilikusanyika na kuhimiza lazima mwalimu flani awepo kwenye kikao hicho.

Leo hii mambo ni tofauti!Walimu wamekuwa chanzo cha jamii kupoteza mwelekeo.Mavazi yasiyoendana na wadhifa walio nao imekuwa jambo la kawaida kwa walimu wetu.

Ni vema jamii ikatambua kuwa shuleni ni sehemu muhimu kwenye makuzi ya mtoto.Ili kuepuka matokeo mabaya ya mtoto katika siku za baadaye ni muhimu jamii ikaona umuhimu wa kuweka mazingira yenye kuwezesha walimu wenye staha na wenye kutambua wajibu wao katika jamii inayowazunguka.

MAJIMBO YA MBEYA KUGAWANYWA.



MAJIMBO ya Mbeya mjini na Mbeya vijijini huenda yakagawanywa na kuwa majimbo mawilimawili iwapo Tumea ya taifa ya uchaguzi itaridhia maombi yaliyopendekezwa na wadau kwenye vikao vya Ushauri vya wilaya vilivyofanyika jana.

Vikao vya kuyagawa majimbo hayo vimefanyika kwa nyakati na tofauti kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya ambapo kwa jimbo la Mbeya mjini wadau wamependekeza kuundwa kwa majimbo mapya ya Iyunga na Sisimba huku Jimbo la Mbeya vijijini likipendekezwa kuundwa kwa majimbo ya Mbeya na Isangati.

Akizungumza kwenye kikao cha Ushauri cha wilaya,Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Bwana Musa Zungiza amesema mapendekezo ya mgawanyo wa jimbo la Mbeya mjini yanazingatia maeneo ambayo awali yalikuwa ni tarafa.

Bw.Zungiza amesema katika Tarafa ya Iyunga ambayo sasa inapendekezwa kuwa jimbo kuna kata 21 na mitaa 116,iinakadiriwa kuwa na wakazi 327,122 hadi kufikia Julai 2015 idadi aliyosema inakidhi vigezo vya tarafa hiyo kuwa jimbo.

Kwa upande wa tarafa ya Sisimba inayopendekezwa kuwa jimbo la Sisimba amesema ina kata 15 inayokadiriwa kuwa na wakazi 106,264 kufikia Julai mwaka huu.

Naye mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Bibi Upendo sanga amesema jimbo la Mbeya litakuwa na kata 11 zinazokadiriwa kuwa na jumla ya wakazi 107,349.

Bi.Sanga amesema jimbo la Isangati lenye kata 15 zinazokadiriwa kuwa na jumla ya wakazi 221.

 Mwisho.


Saturday, May 23, 2015

WANANDOA WACHINJWA NA KUUAWA KWA KUTENGANISHWA VICHWA


WANANDOA wawili wakazi katika kitongoji cha Makambo  Kata ya Itenka wilayani Mlele Mkoani Katavi wameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo zao na  kutenganishwa kichwa na kiwiliwili  baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana wakati wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao.

Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  amewataja wanandoa hao wawili waliouawa kuwa ni  Seth Mwakalimbwa (65) na Yakoba  Kalulu(48)  wakazi wa kitongoji hicho.

Kidavashari amesema jana kuwa tukio hilo la mauaji ya kikatili lilitokea hapo juzi nyakati za usiku  wa manane nyumbani kwa wanandoa hao waliokuwa wakiishi pamoja kama mke na mume

 Amesema kwamba  marehemu  hao wakutwa na mauti hayo wakati wakiwa ndani ya nyumba wamelala ambapo kundi la watu wasiofahamika walivamia nyumba yao na kuwaua kwa kuwakata kata na mapanga mwilini kiasi cha kupoteza fahamu kisha kuwachinja kwa kuwatenganisha kichwa na kiwiliwili.

Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa, Balozi wa eneo hilo, Wilbroad Mahenge   alisema kuwa yeye ndio alibaini kutokea kwa mauaji hayo baada ya kutowaona wanandoa hao kwa siku mbili pasipo kuwa na taarifa yoyote.

Mahenge alisema kuwa kutokana na kutokuwa na taarifa yoyote ukizingatia kwamba pia yeye ni jirani yao, alikwenda katika makazi yao  na alipofika hapo,  alikuta  milango ya nyumba yao iko wazi hali ambayo ilimfanya apate mashaka zaidi

 Ameongeza kwamba  alijaribu kuwaita kwa majina yao lakini hakuna  aliyeweza kuitika   hivyo aliamua  kuingia ndani  ya nyumba  yao  na  ndipo  aliwakuta wakiwa  wamelazwa kitandani  huku   wakiwa wamefariki dunia kwa kuchinjwa shingo zao na kutenganishwa na kiwiliwili

 Baada ya kuona hali hiyo,  Mahenge alitoka nje na kasha alikwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa Serikali ya Kitongoji ambao na wao walitoa taatifa kwa jeshi la polisi ambao walifika kwenye eneo hilo muda mfupi baadaye.

Kamanda Kidavashari amesema  chanzo cha  tukio la mauaji hayo ya kikatili  linahusishwa  na imani  za  kishirikina  na mpaka sasa  hakuna mtu  wala watu  waliokamatwa  kuhusika na tukio hilo lakini polisi inaendelea kuwasaka watu hao.

CHANZO-PEMBEZONI KABISA BLOG

Friday, May 22, 2015

MAAFISA UANDIKISHAJI BVR MKOA WA MBEYA WALIPOAPISHWA KWAAJILI YA KAZI HIYO








TMA YAPELEKA HUDUMA ZIWA NYASA

Mkuu wa wilaya ya Kyela Thea Ntara(wa tatu kutoka kulia) akiwa na maafisa wa TMA na wadau wengine wa shughuli za kimaendeleo katika ziwa Nyasa.Wadau hawa walikutana mjini Kyela kupashana habari za ujio wa TMA katika ziwa Nyasa sambamba na kupeana uzoefu juu ya majanga ya ziwa hilo.
 Kaimu mkurugenzi wa huduma za ufundi za TMA Dk.Pascal Waniha akielezea namna TMA ilivyoona umuhimu wa kufikisha huduma zake kwa watumiaji wa ziwa Nyasa.
 Wadau mbalimbali wa ziwa Nyasa wakiwemo wavuvi wakishiriki semina ya kupeana uzoefu juu ya majanga ya ziwa hilo. 


 Wanahabari kama anavyoonekana mwandishi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo Solomon Mwansele ni miongoni mwa wadau ambao wametajwa kuwa na umuhimu mkubwa kwenye usambazaji wa taarifa zitakazotolewa na TMA juu ya utabiri wa hali ya hewa ndani ya ziwa Nyasa.
 Mkuu wa wilaya ya Kyela Thea Ntara akibainisha namna ujio wa TMA katika ziwa Nyasa ulivyoleta neema kwa watumiaji wa ziwa hilo


Mkurugenzi wa huduma za Utabiri za TMA Dk.Hamza Kabelwa akibainisha mikakati ya TMA katika utoaji taarifa za hali ya hewa.

                            HABARI KAMILI.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imepeleka huduma zake katika wilayani Kyela lengo ni kusogeza huduma ya upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa kwa watumiaji wa ziwa Nyasa.

Kwa mujibu wa watumiaji wa ziwa Nyasa wakiwemo wavuvi na wasafirishaji,kwa muda mrefu wamekuwa wakilazimika kutumia njia za asili kubaini majanga yanayoweza kutokea ndani ya ziwa hilo na wakati mwingine walilazimika kutumia taarifa zilizotolewa na mamlaka ya hali ya hewa ya nchi jirani ya Malawi.

Wakazi wilayani Kyela wanasema kutokana na changamoto hiyo madhara makubwa yamekuwa yakitokea ikiwemo vifo vya wavuvi kutokana na vimbunga vilivyowakumba wakati wakiendelea na shughuli zao ndani ya ziwa Nyasa.

Kaimu mkurugenzi wa huduma za ufundi za TMA Dk.Pascal Waniha anasema mamlaka hiyo imeamua kuwafikia watumiaji wa ziwa Nyasa kutokana na mahitaji yaliyopo.

Mkuu wa wilaya ya Kyela Thea Ntara anasema sasa watumiaji wa ziwa hilo wako katika mazingira salama kwakuwa kabla ya kufanya shughuli zao watapataa taarifa za uhakika juu ya utabiri wa hali ya hewa.