KATIKA kipindi cha miaka ya zamani Ualimu ulikuwa
wito.Ni kutokana na hali hiyo watu walioajiriwa kwenye tasnia hiyo walikuwa
wenye staha kulingana na walivyofundishwa chuoni.
Uwepo wao katika kundi lolote ndani ya jamii
uliwatofautisha na makundi mengine.Walionekana watu wenye kutegemewa na jamii
kwenye masuala ya ushauri na hakika jamii iliyowazunguka ilinufaika na uwepo
wao.
Walimu katika miaka hiyo hawakuishia kufundisha wanafunzi
darasani,walifundisha jamii yote.Palipotokea na jambo jamii ilikusanyika na
kuhimiza lazima mwalimu flani awepo kwenye kikao hicho.
Leo hii mambo ni tofauti!Walimu wamekuwa chanzo cha
jamii kupoteza mwelekeo.Mavazi yasiyoendana na wadhifa walio nao imekuwa jambo
la kawaida kwa walimu wetu.
Ni vema jamii ikatambua kuwa shuleni ni sehemu
muhimu kwenye makuzi ya mtoto.Ili kuepuka matokeo mabaya ya mtoto katika siku
za baadaye ni muhimu jamii ikaona umuhimu wa kuweka mazingira yenye kuwezesha
walimu wenye staha na wenye kutambua wajibu wao katika jamii inayowazunguka.
No comments:
Post a Comment