Friday, August 22, 2014
Thursday, August 21, 2014
Wednesday, August 20, 2014
WATOTO 9700 WAKABILIWA NA UTAPIAMLO KALAMBO
WATOTO 9700 waliopo katika vijiji vya Kisumba, Kasote na Chisenga
kwenye kata ya Kisumba vilivyoko wilayani Kalambo mkoani Rukwa
wanakabiliwa na tatizo kubwa la utapiamlo mkali kufuatia kuwepo kwa
malezi duni kutoka kwa wazazi na walezi wao.
Hali hiyo imesababisha mkoa wa Rukwa kuwa miongoni mwa mikoa mitano ambayo inakabiliwa na tatizo la udumavu licha kuzalisha kwa wingi mazao ya chakula hususani ni mahindi.
Baadhi ya wanawake wa kijiji hicho walisema hayo wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana wakati wa sherehe za siku ya afya kijiji iliyoandaliwa katika kijiji cha Kisumba iliyoandaliwa na shirika la Africare linalotekeleza mradi wa wazazi na mwana wenye lengo la kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano mkoani humo.
Mmoja wa wanawake hao, Yusta Sangu alisema kuwa hali hiyo imejitokeza kutokana na kukosekana kwa elimu sahihi ya afya uzazi kwa muda mrefu kiasi cha kufanya wanawake wengi wajifungulie majumbani bila kufuata uzazi wa mpango hivyo kuwa na idadi kubwa mno ya watoto
KWA HISANI YA BLOG YA PEMBEZONI KABISA
Hali hiyo imesababisha mkoa wa Rukwa kuwa miongoni mwa mikoa mitano ambayo inakabiliwa na tatizo la udumavu licha kuzalisha kwa wingi mazao ya chakula hususani ni mahindi.
Baadhi ya wanawake wa kijiji hicho walisema hayo wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana wakati wa sherehe za siku ya afya kijiji iliyoandaliwa katika kijiji cha Kisumba iliyoandaliwa na shirika la Africare linalotekeleza mradi wa wazazi na mwana wenye lengo la kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano mkoani humo.
Mmoja wa wanawake hao, Yusta Sangu alisema kuwa hali hiyo imejitokeza kutokana na kukosekana kwa elimu sahihi ya afya uzazi kwa muda mrefu kiasi cha kufanya wanawake wengi wajifungulie majumbani bila kufuata uzazi wa mpango hivyo kuwa na idadi kubwa mno ya watoto
KWA HISANI YA BLOG YA PEMBEZONI KABISA
CHADEMA MBEYA YAPATA VIONGOZI WAPYA
CHAMA Cha Demokrasia na
Maendeleo(CHADEMA), Mkoani, kimepata viongozi wapya kupitia uchaguzi
uliofanyika jana jijini Mbeya.
Katika uchaguzi wa jana,
Msimamizi wa uchaguzi huo Mratibu wa chama hicho kanda ya Nyanda za Juu Kusini,
Franky Mwaisumbe, amemtaja Joseph China kuwa mwenyekiti mpya.
China ameibuka mshindi
baada ya kupata kura 36 dhidi ya kura 19 alizopata Zabron Nzunda na nne
alizoambulia Meshack Kapange aliyejiunga na chama hicho hivi karibuni akitokea
CCM.
Kwa nafasi ya Katibu
msimamizi amesema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho wagombea wa nafasi hiyo
huomba na majina yaliyopendekezwa katika ngazi husika hupelekwa katika kamati
ya utendaji taifa ambayo huthibitisha jina moja kati ya walioomba.
Mwaisumbe amesema kwa
mkoa wa Mbeya walioomba nafasi hiyo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa mpito wa chama
hicho mkoa, Boyd Mwabulanga,Mwenyekiti wa Wilaya ya Mbarali, Kazamoyo
Jidawaya na Fanul Mkisi.
Akifafanua zaid imatokeo
ya uchaguzi,msimamizi huyo amesema nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la vijana
(Bavicha)Mkoa wa Mbeya, imechukuliwa na Tito George, wakati nafasi ya
Baraza la wanawake (Bawacha) ikishikwa na Happynes Kulabya, huku nafasi
ya Mwenyekiti Baraza la wazee ikienda kwa Martin Mpwani.
Monday, August 18, 2014
NI SHIDA!!!!!!!TUKO KIKAZI ZAIDI.
Mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Joachim Nyambo(kulia) akifuatiwa na mwandishi wa magazeti ya Mwananchi,The Citizen na Mwanaspoti mkoani Mbeya Brand Nelson na mwandishi wa Chanel Ten Rose Chapewa.Katikati wapo Solomoni Mwansele wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo,Rashidi Mkwinda wa Majira na Charles Mwaipopo wa Baraka FM.Mwenye suti kushoto ni mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro
Saturday, August 16, 2014
Lyamba Lya Mfipa yatembelea ofisi za Tushiriki
Mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Bw.Joachim Nyambo(wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la TUSHIRIKI alipotembelea ofisi za shirika hilo zilizopo Soweto jijini Mbeya.
Shirika la Tushiriki linaendesha mradi wa kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira ya misitu iliyopo pembezoni mwa mlima Rungwe.
Shirika la Tushiriki linaendesha mradi wa kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira ya misitu iliyopo pembezoni mwa mlima Rungwe.
Friday, August 15, 2014
MBEYA CITY,TANZANIA PRISONS WAZUIWA KUTUMIA UWANJA WA SOKOINE
KIKOSI CHA MBEYA CITY
KIKOSI CHA TANZANIA PRISONS
KIKOSI CHA TANZANIA PRISONS
WAMILIKI wa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
wameendelea na jitihada za kuukarabati uwanja huo ikiwa ni sehemu ya maandalizi
ya michuano ya ligi kuu ya Tanzania bara itakayoanza kutimua vumbi Septemba 20
mwaka huu.
Ukarabati unaoendelea hivi sasa katika uwanja huo
utakaotumiwa na Timu za Mbeya City na Tanzania Prison kama uwanja wa nyumbani
ni pamoja na kuondoa magugu yasiyohitajika katika eneo la kuchezea maarufu kama
Pichi.
Akizungumza na Lyamba Lya Mfipa,Meneja wa
Uwanja huo Modestus Mwaluka amebainisha namna shughuli nzima ya kuondoa magugu
hayo inavyoendeshwa,shughuli ambayo pia imesababisha Timu za Mbeya City na
Tanzania Prison kuzuiwa kuendelea kuutumia uwanja huo kwa mazoezi.
Mwaluka amesema wanalazimika kuyaondoa magugu hayo
kutokana na asili yake mbaya ambapo huweka nundu nundu uwanjani na kusababisha
mpira kukosa mwelekeo unaopaswa wakati ukichezwa katika uwanja husika.
Amezitaka timu za Mbeya City na Tanzania Prisons
kutojawa na hasira baada ya kuzuiwa kutumia uwanja huo kwa mazoezi badala yake
watambue kuwa uongozi wa uwanja una nia
ya dhati ya kuboresha miundombinu itakayosaidia timu hizo kucheza mpira mzuri
na wenye kuvutia.
Mbunge wa zamani asimikwa kuwa kamanda wa UVCCM kata ya Kapele
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoa wa Mbeya Aman Kajuna akimvisha Joho Aliyewahi kuwa mbunge wa Mbozi Magharibi(Sasa Momba) Eliakim Simpasa baada ya kumsimika rasmi kuwa Kamanda wa UVCCM kata ya Kapele wilayani Momba.
Simpasa ambaye hivi sasa ni Mjumbe wa halmashauri kuu CCM mkoa akitafakari jambo
Thursday, August 14, 2014
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax - +255252503734
MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 14.08.2014.
·
MTOTO MDOGO MWENYE UMRI WA KATI YA MIAKA 03-04
AFARIKI DUNIA PAPO HAPO KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI MBOZI.
·
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MIWILI AFARIKI DUNIA
BAADA YA KUZAMA KATIKA BWAWA LA KUFUGIA SAMAKI.
·
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA
CHUNYA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUNIKWA NA KIFUSI CHA UDONGO.
·
WATU WAWILI WAKAZI WA KIWIRA ROAD WILAYA YA
RUNGWE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA BHANGI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTOTO MDOGO
MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 03 – 04
ALIYETAMBULIKA KWA JINA MOJA LA JACK
AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 140 BCU AINA YA SUZUKI LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA ELIUD KALINGA (54) MCHUNGAJI WA KANISA LA KKKT –
TUNDUMA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.08.2014
MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO
MAENEO YA VWAWA SEKONDARI, KATA YA NDALAMBO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI,
MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI YA VWAWA. DEREVA
AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTOTO MWENYE
UMRI WA MIAKA MIWILI (02)
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FROLA MLINGO
ALIKUTWA AMEKUFA MAJI KWENYE BWAWA LA KUFUGIA SAMAKI
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.08.2014
MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA MAHANGO,
WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA KIFO CHAKE NI
KUZIDIWA NA MAJI YA BWAWA HILO WAKATI AKICHEZA NA WATOTO WENZAKE.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA ILI
KUEPUKA MADHARA/MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU MMOJA MKAZI
WA KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA CHNUYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ASANGILWISYE MWAISANILA (21) ALIFARIKI
DUNIA BAADA YA KUFUNIKWA NA KIFUSI CHA UDONGO WA KUFYATULIA TOFALI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 12.08.2014
MAJIRA YA SAA 15:45 ALASIRI HUKO
KATIKA KIJIJI NA KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA. INADAIWA KUWA, MAREHEMU ALIANGUKIWA NA KUFUNIKWA NA KIFUSI HICHO WAKATI
AKICHIMBA UDONGO KATIKA ENEO HILO.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII
KUWA MAKINI KATIKA SHUGHULI ZAO HASA KWA KUCHUKUA TAHADHARI ILI KUEPUKA
MATATIZO.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. JAMSE
MBILINYI (27) NA 2. AMBWENE SANGA
(25) WOTE WAKAZI WA KIWIRA ROAD WAKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO MOJA KWENYE
MFUKO WA RAMBO.
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 12.08.2014
MAJIRA YA SAA 19:40 JIONI HUKO
KATIKA ENEO LA KIWIRA ROAD, KATA YA KAWETERE, TARAFA YA TUKUYU MJINI, WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA WATUMIAJI WA BHANGI HIYO,
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA NI
KINYUME CHA SHERIA.
Imesainiwa na kutolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Wednesday, August 13, 2014
MILA NA TAMADUNI ZA MTANZANIA
Tanuri linalosadikiwa kuwa lilikuwa likitumiwa na wahunzi zaidi ya miaka 100 iliyopita kuyeyushia udongo wenye madini ya chuma na kisha kutuyatumia kwaajili ya kutengenezea zana mbalimbali ikiwemo silaha za jadi kwaaji ya vita vya miaka ya zamani.Mabaki ya tanuri hili la asili yapo katika moja ya mapori yaliyopo kwenye kata ya Kapele wilayani Momba mkoani Mbeya.
Mabaki ya matanuri haya yameendelea kupotea siku hadi siku.Huenda miaka kadhaa ijayo yasionedkane kabisa na watanzania wasiweze kujifunza kwa vitendo juu ya mambo ya kihistoria yaliyoachwa na mababu wa kabila la kinyamwanga hapa wilayani Momba.
Saturday, August 2, 2014
MBEYA CEMENT YACHANGIA MIFUKO 1000 YA SARUJI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA UNAOJENGWA CHUNYA
.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akipokea msaada wa Mifuko ya Saruji kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa kiwanda cha Mbeya Ciment Catherine Langreney.
Mwandishi wa habari za michezo mkongwe George Chanda akielezea namna wilaya ya Chunya ilivyowahi kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa ilipotoa wanamichezo waliokwenda kushiriki mashindano ya kimataifa miaka ya nyuma
MIFUKO 1000 ya saruji sawa na Tani 50 zimetolewa na kampuni ya Lafarge kupitia kiwanda chake cha Saruji cha Mbeya kwaajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo wilayani Chunya.
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Saruji Mbeya Catherine Langreney amekabidhi msaada huo kwa mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro mbele ya wadau mbalimbali waliofika kushuhudia tukio hilo katika eneo la Mbugani unapojengwa uwanja.
Akikabidhi msaada huo.Langreney ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika ujenzi wa uwanja huo huku akisisitiza kua kutoa mifuko 1000 ya saruji ni mwanzo tu wa mahusiano mazuri baina ya kiwanda na halmashauri ya wilaya ya Chunya.
Amesema lengo la kiwanda ni kuendelea kuisaidia jamii inayoishi jirani kujenga miji ya kisasa yenye muonekano mzuri na kwa bei nafuu na kutaja ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo sawa kuwa miongoni mwa vitu vinavyohitajika katika miji bora.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro ameishukuru kampuni hiyo kwa kuungana na wadau wengine walioamua kujitoa kuchangia michango ya hali na mali ili kuwezesha kujengwa kwa uwanja huo.
Amesema hadi kukamilika kwa ujenzi huo utakaokuwa na viwanja vya michezo mbalimbali ndani yake zinahitajika zaidi ya shilingi bilioni nane na hadi hivi sasa wadau wameweza kuchangi kiasi cha shilingi milioni 107 zikiwa ni fedha taslimu na nguvu kazi.
Subscribe to:
Posts (Atom)