WATOTO 9700 waliopo katika vijiji vya Kisumba, Kasote na Chisenga
kwenye kata ya Kisumba vilivyoko wilayani Kalambo mkoani Rukwa
wanakabiliwa na tatizo kubwa la utapiamlo mkali kufuatia kuwepo kwa
malezi duni kutoka kwa wazazi na walezi wao.
Hali hiyo imesababisha mkoa wa Rukwa kuwa miongoni mwa mikoa mitano
ambayo inakabiliwa na tatizo la udumavu licha kuzalisha kwa wingi mazao
ya chakula hususani ni mahindi.
Baadhi ya wanawake wa kijiji
hicho walisema hayo wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana
wakati wa sherehe za siku ya afya kijiji iliyoandaliwa katika kijiji
cha Kisumba iliyoandaliwa na shirika la Africare linalotekeleza mradi wa
wazazi na mwana wenye lengo la kupunguza vifo vya wajawazito na watoto
chini ya miaka mitano mkoani humo.
Mmoja wa wanawake hao, Yusta Sangu alisema kuwa hali hiyo
imejitokeza kutokana na kukosekana kwa elimu sahihi ya afya uzazi kwa
muda mrefu kiasi cha kufanya wanawake wengi wajifungulie majumbani bila
kufuata uzazi wa mpango hivyo kuwa na idadi kubwa mno ya watoto
KWA HISANI YA BLOG YA PEMBEZONI KABISA
No comments:
Post a Comment