Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, August 2, 2014

MBEYA CEMENT YACHANGIA MIFUKO 1000 YA SARUJI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA UNAOJENGWA CHUNYA

. Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akipokea msaada wa Mifuko ya Saruji kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa kiwanda cha Mbeya Ciment Catherine Langreney. Mwandishi wa habari za michezo mkongwe George Chanda akielezea namna wilaya ya Chunya ilivyowahi kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa ilipotoa wanamichezo waliokwenda kushiriki mashindano ya kimataifa miaka ya nyuma MIFUKO 1000 ya saruji sawa na Tani 50 zimetolewa na kampuni ya Lafarge kupitia kiwanda chake cha Saruji cha Mbeya kwaajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo wilayani Chunya. 

 Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Saruji Mbeya Catherine Langreney amekabidhi msaada huo kwa mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro mbele ya wadau mbalimbali waliofika kushuhudia tukio hilo katika eneo la Mbugani unapojengwa uwanja. 

 Akikabidhi msaada huo.Langreney ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika ujenzi wa uwanja huo huku akisisitiza kua kutoa mifuko 1000 ya saruji ni mwanzo tu wa mahusiano mazuri baina ya kiwanda na halmashauri ya wilaya ya Chunya.

 Amesema lengo la kiwanda ni kuendelea kuisaidia jamii inayoishi jirani kujenga miji ya kisasa yenye muonekano mzuri na kwa bei nafuu na kutaja ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo sawa kuwa miongoni mwa vitu vinavyohitajika katika miji bora. 

 Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro ameishukuru kampuni hiyo kwa kuungana na wadau wengine walioamua kujitoa kuchangia michango ya hali na mali ili kuwezesha kujengwa kwa uwanja huo. 

Amesema hadi kukamilika kwa ujenzi huo utakaokuwa na viwanja vya michezo mbalimbali ndani yake zinahitajika zaidi ya shilingi bilioni nane na hadi hivi sasa wadau wameweza kuchangi kiasi cha shilingi milioni 107 zikiwa ni fedha taslimu na nguvu kazi.

No comments:

Post a Comment