Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, August 20, 2014

CHADEMA MBEYA YAPATA VIONGOZI WAPYA


CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Mkoani, kimepata viongozi wapya kupitia uchaguzi uliofanyika jana jijini Mbeya.

Katika uchaguzi wa jana, Msimamizi wa uchaguzi huo Mratibu wa chama hicho kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Franky Mwaisumbe,  amemtaja Joseph China kuwa mwenyekiti mpya.


China ameibuka mshindi baada ya kupata kura 36 dhidi ya kura 19 alizopata Zabron Nzunda na nne alizoambulia Meshack Kapange aliyejiunga na chama hicho hivi karibuni akitokea CCM.

Kwa nafasi ya Katibu msimamizi amesema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho wagombea wa nafasi hiyo huomba na majina yaliyopendekezwa katika ngazi husika hupelekwa katika kamati ya utendaji taifa ambayo huthibitisha jina moja kati ya walioomba.

Mwaisumbe amesema kwa mkoa wa Mbeya walioomba nafasi hiyo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa mpito wa chama hicho mkoa, Boyd Mwabulanga,Mwenyekiti wa Wilaya ya Mbarali, Kazamoyo Jidawaya  na   Fanul Mkisi.

Akifafanua zaid imatokeo ya uchaguzi,msimamizi huyo amesema nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la vijana (Bavicha)Mkoa wa Mbeya, imechukuliwa na Tito George, wakati  nafasi ya Baraza la wanawake (Bawacha) ikishikwa na Happynes Kulabya, huku  nafasi ya Mwenyekiti Baraza la wazee ikienda kwa Martin Mpwani.

No comments:

Post a Comment