Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, November 26, 2014

GARI YA POLISI NAYO YACHOCHORA,ALIKUWEMO RTO MKOA WA MBEYA

                                  NI KATIKA MTEREMKO WA IWAMBI KWENDA MBALIZI

Sunday, November 23, 2014

WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 120,YUMO ASKARI POLISI PC JAMES

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mbeya imewahukumu kifungo cha miaka 120 watu wanne akiwemo aliyekuwa askari wa jeshi la Polisi baada ya kukutwa na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
 
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, James Mhanusi,ambapo  mbali na kuwatia hatiani washitakiwa hao Mahakama hiyo pia imemuachia huru mshtakiwa mmoja kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuna ushahidi unaomhusisha na tukio moja kwa moja.
 
Mwendesha mashtaka wa Serikali,Catherine Paul, aliwataja washtakiwa kuwa ni aliyekuwa Askari wa Jeshi la Polisi,8303 Pc James, Elinazi Mshana,Lusajo Jeremia na Abdalah Mohamed ambao kwa pamoja walitenda kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha Oktoba 7, 2013.
 
Mwendesha mashtaka huyo alisema watuhumiwa hao wenye kesi namba 23/2014 walitenda kosa hilo kinyume cha kifungu cha 287 (a) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ambapo walifanikiwa kupora Kahawa yenye thamani ya shilingi Milioni 119.2 yenye uzito wa kilogramu 30091.
 
Akisoma Hukumu kwa watuhumiwa hao, Hakimu Mhanusi amesema kutokana na ushahidi wa upande wa mashtaka na upande wa utetezi mahakama imeona mshtakiwa namba tatu katika kesi hiyo ambaye ni Gwantwa Malakasuka hakukuwa na ushahidi unaomtia hatiani pasipo shaka hivyo akaamuru kuachiwa huru.
 
Kwa upande wa Washtakiwa wengine, amesema ushahidi wa mazingira pamoja na kutambuliwa na shahidi wa kwanza ambaye pia ndiye aliyekuwepo eneo la tukio unathibitisha pasipo shaka kutenda tukio hilo kutokana na kufanya tukio hilo majira ya jioni wakati kuna mwanga hivyo ilikuwa rahisi kutambuliwa.
 

Thursday, November 20, 2014

ASKARI ALIYEMUUA MWANAFUNZI HUYU AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA


 Huu ni mwili wa Marehemu kijana Daniel Mwakyusa mara baada ya kufanyiwa uchunguzi baada ya kuuawa.Daniel alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha TEKU
 Haya ni baadhi ya majeraha aliyojeruhiwa askari alipokutwa Univesal Pub siku ya Valentine akiwa na mwanamke aliyesadikiwa kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na askari Maduhu

 Mwili wa mwanafunzi huyo kabla ya kuzikwa mara baada ya kuagwa na ndugu,jamaa na marafiki.Jeshi la polisi liligharamia shughuli za maziko ya mwanafunzi huyo na hapo ndipo shitaka likaanza kuunguruma mahakamani.
                             
                        HABARI KAMILI
MAHAKAMA Kuu kanda ya Mbeya imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa askari wa jeshi la polisi F 5842 DC Maduhu aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) Daniel Mwakyusa.

Aidha mahakama hiyo pia imewaaachia huru washitakiwa wengine wawili wa kesi hiyo F 7769 DC Shaban na WP 6545 DC Neema baada ya kuwakuta hawana hatia.

Hukumu hiyo ya kesi namba 16 ya mwaka 2013 imetolewa leo(Nov 19) na jaji Rose Temba baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili.

Awali ilielezwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali Archiles Mulisa akisaidiwa na Catherine Paul kuwa washitakiwa walifanya mauaji ya kukusudia mnamo Februari 14 mwaka 2012 kinyume cha kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Kwa mujibu wa Wakili Mulisa washitakiwa hao kwa pamoja walihusika na mauaji ya Daniel Mwakyusa baada ya kumpiga marehemu huyo kwa kutumia silaha inayodhaniwa kuwa ni bunduki nje ya ukumbi wa starehe ujulikanao Univesal uliopo Uyole jijini Mbeya.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo,jaji Temba amesema mshitakiwa namba moja DC Maduhu anahusika moja kwa moja na mauaji hayo kutokana na ushahidi wa kimazingira ikiwamo yeye kuwa mtu wa mwisho kuondoka na marehemu eneo la tukio na kumpeleka kwenye gari,risasi tatu kupungua kwenye bunduki yake na pia kuwa mtu wa mwisho kurejesha silaha kituoni.

Wednesday, November 19, 2014

BADO HAKUJACHANGANYA,TUNASUBIRI WATEJA WAMWAGIKE

 Baadhi ya vibanda vilivyojengwa na wafanyabiashara wadogo(Wamachinga) baada ya halmashauri ya jiji la Mbeya pembezoni mwa Bustani ya jiji vikionekana havijaanza kutumika.
 Licha ya mamlaka husika kupeleka magari madogo ya abiria maarufu kama daladala katika barabara za eneo hilo bado baadhi ya wamachinga wanasema biashara haijawa nzuri kama maeneo waliyokuwa wakifanyia shughuli zao awali



Saturday, November 15, 2014

MAHAFALI YA KOZI YA NNE YA ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI YALIVYOFANA

Wahitimu wa mafunzo ya awali wakipita mbele ya mgeni rasmi kwa ukakamavu kwenye mahafali yaliyofanyika katika chuo cha Magereza Kiwira kilichopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya.






 Mgeni Rasmi Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Ame Silima akikagua gwaride la wahitimu

 Naibu waziri akikabidhi vyeti kwa wahitimu waliofanya vizuri kwenye mafunzo yao









 Kikosi cha kujihami kikiwa uwanjani tayari kuonesha namna askari wa Zimamoto na Uokoaji anavyoweza kupambana na adui pasipo kutumia silaha za moto
























 Askari wa kike akionesha umahiri wa kuvuka kutoka eneo moja kwenda jingine kwa kupita juu ya kamba