Mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela (Kushoto)akipokea msaada wa saruji kutoka kwa mkurugenzi wa mradi wa kampuni
ya State Grid mhandisi Andrew Mwaipaja
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela (Kushoto)akipokea msaada wa saruji kutoka kwa Mkurugenzi wa fedha wa TOL Gases Evarist
Telafu
MSAADA wa Saruji na Sealingboard wenye jumla ya
thamani ya shilingi milioni 4.7 umetolewa kwa wilaya ya Rungwe mkoani hapa ili
kuiwezesha wilaya hiyo kukamilisha ujenzi wa maabara kwa wakati.
Kampuni ya State Grid inayosambaza umeme vijijini
kupitia wakala wa umeme vijijini(REA) imetoa mifuko 100 ya saruji na sealing
board 80 vyote vikiwa na jumla ya thamani ya shilingi milioni tatu na Kampuni inayojishughulisha
na uzalishaji na uchakataji hewa mkaa ya TOL Gases imekabidhi mifuko 100 ya
Saruji yenye thamani ya shilingi milioni 1.7.
Wakikabidhi msaada huo mkurugenzi wa miradi wa kampuni
ya State Grid mhandisi Andrew Mwaipaja na Mkurugenzi wa fedha wa TOL Gases Evarist
Telafu wamesema kampuni hizo zimechukua uamuzi wa kusaidia ujenzi wa maabara za
shule za sekondari baada ya kuguswa na mikakati ya ujenzi huo.
Akipokea msaada huo,Mkuu wa wilaya ya Rungwe
Chrispini Meela amesema kampuni hizo mbili ambazo shughuli zake ni za kisayansi
zimeonesha mfano mzuri wa wadau wa masuala ya sayansi kutowaachia wazazi pekee
kutekeleza agizo la rais.
Mkuu huyo wa wilaya amesema licha ya kuwepo kwa
changamoto za baadhi ya wananchi kutoona umuhimu wa kuchangia upo uhakika wa
kutosha kuwa maabara katika shule za sekondari wilayani hapa zitakamilika kabla
ya Novemba 15 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment