Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, September 30, 2014

SHUGHULI YA UJENZI WA MAKABURI YA FAMILIA YA NDG.BENJAMIN MWENDA MKOANI NJOMBE

Nuru Benjamini Mwenda akiwa amepiga magoti kwenye kaburi la Baba yake mzee Benjamini mada baada ya kukamilika kwa shughuli za ujenzi wa makaburi manne likiwemo la mzee huyo.
Awali wakati shughuli ya ujenzi ikiwa inaendelea.Kushoto ni MC maarufu mkoani Mbeya Ben Benjamini ambaye ni mtoto wa Mzee Benjamini akishiriki katika shughuli za ujenzi.
Mke wa Marehemu Benjamini akiwa katika kaburi la mumewe pamoja na shemeji yake Victor na mtoto wa Marehem Benno

















 Bosco Benjamini Mwenda akiwa katika kaburi la baba yake mzazi marehemu mzee Benjamini Mwenda


 MC Ben Benjamini maarufu kama Duble B baaada ya kukamilisha ujenzi wa makaburi mne likiwemo la baba yake mzazi.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 30.09.2014.


  KATIKA TUKIO LA KWANZA:

KIKONGWE MWENYE UMRI WA MIAKA 90 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BAPONDO NGAO MKAZI WA KIJIJI CHA UKWILE WILAYANI MBOZI ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA MNAMO TAREHE 29.09.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI UKWILE, KATA YA ISANDULA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WATU HAO WALIMVIZIA MAREHEMU AKIWA AMELALA NDANI YA NYUMBA YAKE NA KISHA KUMVAMIA NA KUANZA KUMKATAKATA NA KUPELEKEA KIFO CHAKE.

CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO KUFAHAMIKA. MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA NA MAJERAHA MAKUBWA MAWILI YA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI. MAREHEMU ALIKUWA ANAISHI PEKE YAKE MAENEO YA MASHAMBANI UMBALI WA ZAIDI YA KILOMITA TANO [05] KUTOKA MAKAZI YA WATU.

HAKUNA MTU/WATU WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI, MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO ILI AZITOE MARA MOJA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.


KATIKA TUKIO LA PILI:

MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA KATIKA SHULE YA MSINGI SANZYA WILAYA YA MOMBA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VALIUD SIAME@KIMUNDE (13) MKAZI WA KIJIJI CHA KAONGA ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MCHANGA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 29.09.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAONGA, KATA YA CHILULUMO, TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WAKATI TUKIO HILO LIKITOKEA MAREHEMU ALIKUWA NA WANAFUNZI WENZAKE WAKICHIMBA NA KUBEBA MCHANGA KWA AJILI YA UJENZI WA NYUMBA ZA KULALA WAALIMU SHULENI HAPO.

MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUTOA UANGALIZI WAKUTOSHA IKIWA NI PAMOJA NA KUWASIMAMIA WATOTO KATIKA SHUGHULI WANAZOWATUMA KUFANYA ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Monday, September 29, 2014

ASKOFU MWELA ASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 60 YA KUZALIWA




 Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Nyanda za juu kusini,John Mwela akiwa katika ibada ya shukrani kwa kutimiza umri wa miaka 60 huku mkewe Mama Elizabeth Mwela akiwa akisherehekea kutimiza miaka 50.Ibada hii ilifanyika jumapili hii katika kanisa kuu la Anglikana lililopo Uhindini jijini Mbeya.
Wanakwaya wa kanisa kuu wakimpa mkono Askofu Mwela kama ishara ya kumpongeza na kumtakia maisha marefu zaidi
 Ushukuriwe Ee Mwenyezi Mungu kwa kumjalia Askofu huyu kutimiza umri wa miaka 60 huku akionekana kuwa na nguvu zaa kuendelea kukutumikia
Kwaya ya Chisomo kutoka nchini Malawi wakimuimbia bwana Mungu katika ibada hiyo ya shukrani.Kwaya hii iliyoimba nyimbo zake kwa lugha ya nchini Malawi ilikuwa kivutio kikubwa kwenye ibada hii.


Mhubiri na muandaaji wa vipindi vya dini katika redio mbalimbali mkoni Mbeya Victoria Kalengo akihubiri kwenye ibada hiyo ambapo aliwasihi vijana kumkumbuka Mungu siku za ujana wao.


Askofu Mwela akikabidhiwa fimbo kwaajili ya kumsaidia kutembelea iwapo kuna siku afya yake itatetereka kutokana na kuwa na umri mkubwa

Baada ya Ibada sasa sherehe ikahamia nyumbani kwa Askofu huko maeneo ya RRM jijini Mbeya.
Kisha keki maalumu iliyoandikwa kumpa Bwana Shukri ikawekwa mezani.
Hapa Askofu Mwela na Mkewe Mama Elizabeth Mwela wakikata keki tayari kwa kulishana na kuwalisha watu wengine
Askofu Mwela akionesha upendo kwa mkewe kwa kumlisha kipande cha keki.
Mke wa Askofu akionesha upendo wa dhati kwa kumlisha keki Mumewe,Jambo la kumshukuru Mungu pia ni kuwa ndoa ya wawili hawa imetimiza umri wa miaka 25,hivyo.Shukrani hii ilibeba jubilei ya mambo mengi.





















Kwa niaba ya jopo zima la Lyamba Lya Mfipa,mhariri mkuu wa Blogu hii Bw.Joachim Nyambo anaitakia maisha yenye baraka tele familia ya Askofu Mwela.Mungu na Awabariki nyote!