Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, September 22, 2014




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.



 
RPC.                                                                                               Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                               Mkoa wa Mbeya,                                                                                    
Namba ya simu 2502572                                                                                         S. L. P. 260,
Fax - +255252503734                                                                                                 MBEYA.
E-mail:-  rpc.mbeya@tpf.go.tz                                                                      




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 22.09.2014.
 

·         MTOTO WA MIAKA 08 AFARIKI DUNIA AKIWA ANAOGELEA KATIKA MTO ILUMA WILAYANI MOMBA.


·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WATATU WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.



KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 08 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ANITHA SHARIFU MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI KATIKA SHULE YA MSINGI NKANGAMO ALIFARIKI DUNIA AKIWA ANAOGELEA KATIKA MTO ILUMA ULIOPO WILAYANI MOMBA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.09.2014 MAJIRA YA SAA 18:30 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA NDALAMBO, KATA NA TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA MBEYA. INADAIWA KUWA MTOTO HUYO ALIZIDIWA NA MAJI YA MTO HUO HALI IYOPELEKEA KUZAMA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO, KUTOWARUHUSU KWENDA KUOGELEA HAMA KUKARIBIA MAENEO YENYE MAJI KAMA MITO NA MABWAWA YENYE MAJI KWANI NI HATARI KWA WATOTO.


KATIKA MSAKO:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AMBAO NI 1. SHUGUTI SHIMACHO (30) 2. AWADHI SULEIMAN (27) na 3. TAKATARI AYELE (20) KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 21.09.2014 MAJIRA YA SAA 20:54 USIKU HUKO MAENEO YA STENDI KUU YA MABASI TUKUYU MJINI, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU MJINI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA TARATIBU ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI UCHUNGUZI DHIDI YAO UFANYIKE. AIDHA, ANATOA WITO KWA WAGENI KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA ZA KUINGIA NCHINI KWANI KUTOFANYA HIVYO NI KINYUME CHA SHERIA.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment