POLISI mkoani Mbeya inawashikilia wahamiaji haramu
sita raia wa nchi za Ethiopia,Kongo DRC na Burundi kwa tuhuma za kuingia nchini
bila kibali.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed
Msangi wanaoshikiliwa ni Zainabu Asseta(29) na Kadeh Wahalu(27) wote raia wa
Ethiopia.
Wengine ni mtoto Jackline Uhasu(7) na wengine
waliofahamika kwa jina moja moja ambao ni Devine(25) na Beatha(30) raia wa
Burundi na raia wa kongo aliyefahamika kwa jina moja pia la Oliver(25).
Kamanda Msangi amesema wahamiaji haramu hao wamekamatwa
Septemba 14,majira ya saa 2:50 usiku katika kijiji cha Mkola tarafa ya Kiwanja
wilayani Chunya.
Amesema wahamiaji hao walikamatwa wakiwa
wanasafirishwa kwenye basi lenye namba za usajiri T 791 ACJ aina ya Scania mali
ya kampuni ya Super Service lakini hakuweza kubainisha ni wapi wahamiaji hao
walikuwa wakitokea na wapi walikuwa wakielekea.
No comments:
Post a Comment