Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akisisitiza jambo wakati wa kikao.
WATAALAMU katika halmashauri za wilaya mkoani Mbeya
wameagizwa kutumia utaalamu wao kuzuia hoja za mkaguzi na mdhibiti wa fedha za
serikali(CAG) badala ya kutumia utalamu huo kujibu hoja.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ametoa agizo
hilo kwa nyakati tofauti alipokuwa katika vikao vya kupitia na kujadili taarifa
ya CAG kwa halmashauri za wilaya za Chunya na Mbeya kwa mwaka wa fedha
2012/2013.
Kandoro amesema ni kwa miaka mingi sasa wataalamu
katika halmashauri za mkoani hapa wamekuwa wakionesha umahiri mkubwa katika
kujibu hoja zinazoibuliwa na CAG lakini wamekuwa wakishindwa kuonesha umahiri
huo kuzuia hoja zisiibuliwe.
Amesema ni wakati sasa kwa wataalamu hao kuziwezesha
halmashauri kutokumbwa na hoja kwa kuonesha umahili wanaoutumia kujibu hoja
kuzuia hoja kuibuliwa kwa kutekeleza wajibu wao wa msingi.
Kufuatia uzembe huo,kandoro ameyaagiza mabaraza ya
madiwani kuhakikisha wanawawajibishwa wale wote watakaosababisha halmashauri
zao kupata hoja kutokana na uzembe wa mtu mmoja.
Amesema serikali haiwezi kuendelea kufumbia macho
uzembe unaofanywa na watu wachache na kuzisababishia halmashauri kuendelea kuwa
na hoja zisizo za msingi na wakati mwingine kusababisha kupata hati chafu.
Amesema kuwajibishwa kwa watu wanaosababisha kuwepo
kwa hoja za namna hiyo kutatoa fundisho kwa wengine kuanza kuwajibika ipasavyo
wakitambua kuwa uwepo wao katika halmashauri husina kunapaswa kudhihirishwa kwa
kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa taratibu za kazi na si ubabaishaji.
No comments:
Post a Comment