ILI kuwezesha jiji la Mbeya kuwa katika mpangilio na
muonekano mzuri,shirika la nyumba la taifa(NHC) limejitolea kutoa ushirikiano
wa kitaalamu kwa halmashauri ya jiji hilo.
Mkurugenzi mkuu wa NHC Nehemea Mchechu alisema jana
kuwa jiji la Mbeya halipo katika muonekano mzuri kutokana na ujenzi kufanyika
kiholela huku akisema yawezekana halmashauri ya jiji hilo halina wataalamu
wanaoweza kusaidia kuondokana na adha hiyo.
Mchechu amesema ni malengo ya NHC kuona miji nchini
inakuwa katika muonekano wenye kuvutia na kuendana na hadhi stahili badala ya
miji na majiji kuwa katika mpangilio usiofaa.
Kwa upande wake meya wa jiji la Mbeya Athanas
Kapunga amekubaliana na ushauri huo na kusisitiza kuwa halmashauri iko tayari
kuwashirikisha wataalamu wa NHC ili kuweza kutumia utaalamu wao katika
kuliboresha jiji hilo.
Kapunga pia amesema halmashauri ya jiji iko tayari
kutoa ardhi kwaajili ya NHC kujenga nyumba zitakazowezesha jiji kuwa na mvuto
zaidi ya ilivyo hivi sasa.
No comments:
Post a Comment