Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, September 17, 2014

MAUAJI YA KIKATILI YAFANYIKA MSIBANI,WAOMBOLEZAJI WAMPIGA MWANAMKE HADI KUUA



JESHI la polisi mkoani Katavi  linawasaka watu wanaodaiwa  kumuua  kikatili mkazi wa  kijiji cha Kapalala wilayani Mlele ,Rehema Msole(32)   kwa  kupigwa  na shoka  mawe  na nondo  na kisha mwili wake kuchomwa  moto  wakimtuhumu kuwa mchawi

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa  Katavi Dhahiri Kidavashari  amesema tukio hilo  lilitokea kijijni hapo  ,Septemba 13 saa 12  jioni baada la kundi la waombolezaji kumvamia   na kumshambulia kwa kumkata kwa shoka na kumpiga na nondo mawe fimbo na  kisha waliuchoma mwili wake moto

Kidavashari alidai kuwa siku   chache  kabla ya tukio hilo  kulitokea  msiba kijijini hapo  nyumbani  kwa  Christopher Baharia  ambaye alifiwa  na mtoto wake  aitwaye   Elizabeth Baharia

Alifafanua baaada ya kutokea kwa msiba huo  kuliibuka  hisia  kuwa kuna mtu  amemloga  binti huyo wakimshuku  Rehema  Msole

‘’Inasadikiwa    siku za  nyuma  wakati  ndugu wa marehemu  Elizabeth walipokuwa  wakimuuguza   walimuona  Rehema  akichugulia  dirishani  katika chumba   alichokuwa amelala  mgonjwa huyo  kabla ya kufikwa na umauti  .........Hivyo  ndugu hao walihisi kuwa mtu huyo aliyechungulia  dirishani ni mchawi wao ‘’ alidai  Kamanda Kidavashari

Aliongeza  kuwa  siku moja baada ya Elizabeth  kufariki, Rehema akiwa  na familia  yake  nyumbani kwa Isaya  Kyejo aliona kundi waombolezaji  wakitokea  kwenye msibani nyumbani kwa Christopher Baharia  ambao walizingira  nyumba hiyo huku wakishauriana kilicho kuwa kimewaleta ndipo  walipomvamia marehemu  na kuanza kumpiga kwa nondo shoka mawe na fombo   na kisha mwili wake kuuchoma moto huku wakidai kuwa marehemu ni mchawi

 Kamanda  huyo alisema polisi linaendelea na uchunguzi wa  tukio hilo ambapo hadi  sasa hakuna watu wala mtu aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo.

HABARI HII NI KWA HISANI YA BLOGU YA PEMBEZONI KABISA

No comments:

Post a Comment