Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, July 27, 2014

RC Kandoro azindua barabara kati ya Stendi kuu -Meta maarufu kama Mbalizi Road

. Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akikata utepe kuzindua Barabara ya Mbalizi Hapa Kandoro akisisitiza jambo mbelea ya umati wa watu waliofika kushuhudia tukio la uzinduzi. Kandoro akipongezana na Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga MKUU wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro jana amezindua kipande kilometa 2.1 cha barabara cha kutoka eneo la Uhindini hadi Meta jijini Mbeya kilichokarabatiwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5.

 Gharama hiyo ya ujenzi ilipanda kutoka zaidi ya shilingi Bilioni 1.4. iliyokuwa gharama ya awali na kati ya fedha zote zilizotumika,shilingi 853,437,275 ni kutoka vyanzo vya ndani vya halmashauri ya jiji la Mbeya na shilingi 700,000,000 ni kutoka mfuko wa barabara.

 Akizindua barabara hiyo iliyokarabatiwa na kampuni ya kichina ya China Chongqing International Construction Corparation(CICO),Kandoro ameipongeza halmashauri ya jiji kwa kufanya ukarabati huo na kuondoa manung’uniko ya wananchi yaliyodumu kwa muda mrefu kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

 Amewashukuru pia wananchi wakazi na wageni wa jiji la Mbeya kwa kuonesha uvumilivu walipokuwa wakisubiri halmashauri yao kutafuta ufumbuzi kwani hawakuweza kufanya vurugu za aina yoyote badala yake waliendelea kutoa malalamiko kwa njia zilizokuwa sahihi na kuweahimiza viongozi wao.

 Amesema uvumilivu wa namna hiyo ndiyo unaohitajika akisema kutafuta suluhu ya matatizo yaliyopo katika jamii yoyote hakuhitaji malumbano wala migogoro badala yake mashauriano ya pamoja yenye kuleta mawazo ya msingi na yenye tija ya ufumbuzi.

 Kwa upande wake Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga amesema tabia ya tabaka la awali la udongo wa eneo la barabara hiyo ndiyo uliochangia kazi iliyofanywa awali na mkandarasi kuonekana haikukidhi viwango na kusababisha kurejewa upya baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST).

Friday, July 25, 2014

SIKU YA MASHUJAA YAFANA MBEYA

BAADHI YA MAOFISA WA JESHI LA WAANANCHI(JWTZ) WAKIWA WAMESHIKA NEMBO MBALIMBALI ZA MASHUJAA KWAAJILI YA VIONGOZI WA NGAZI MBALIMBALI KIMKOA KUWEKA KATIKA MNARA WA MWENGE WA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA. MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO AKITOA HESHIMA MARA BAADA YA KUWEKA NGAO NA MKUKI KATIKA MNARA WA MASHUJAA JAMII mkoani Mbeya imetakiwa kujiuliza ni kwa namna gani itaweza kukumbukwa na vizazi vijavyo kulingana na historia ya kulitumiakia taifa la Tanzania. Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na wakazi jijini Mbeya waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya mashujaa zilizofanyika katika maeneo ya Mnara wa Mwenge jijini humo. Bw.Kandoro amesema uwepo wa siku ya kuwakumbuka mashujaa kunaikumbusha jamii kutambua kuwa kuna watu waliojitolea kumwaga damu yao ili kwaajili ya kulinda taifa lao. Amesema huenda bila uwepo wa watu waliomwaga damu zao kulilita taifa,wanaoitwa mashujaa hivi sasa taifa la Tanzania lisingekuwa katika muonekano wa hali ya amani na utulivu. Amesema ni wakati sasa kwa wanajamii kujiuliza kizazi kijacho kitawakumbuka kwa mazuri yapi waliyoyatenda kwa taifa lao. Amesema kumbukumbu nzuri pekee na itakayoenziwa kwa heshima ni kuidumisha amani na utulivu uliopo kwa kila mmoja kuhakikisha anatekeleza wajibu wake wa kushirikiana na mwenzake kwa moyo wa upendo na mshikamano.