Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, July 3, 2014

VILABU LIGI KUU VYATAKIWA KUTAFUTA FEDHA KULIPIA VIKUNDI VYA MASHABIKI

MSEMAJI WA TFF BONIFACE WAMBURA AKIFAFANUA JAMBO KATIKA SEMINA YA MATUMIZI YA TIKETI ZA KIELEKTRONIKI LEO JIJINI MBEYA Mwenyekiti wa kamati ya Habari na Mawasiliano ya Chama cha soka mkoani Mbeya(MREFA) Bw.Lwitiko akihoji jambo katika semina hiyo. Wajumbe wa semina wakioneshwa namna mashine za tiketi za kielektroniki zitakavyotumika katika mchezo kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons katika uwanja wa sokoine.Mchezo huu wa kirafiki utachezwa jumamosi hii VILABU vya soka nchini vimepewa changamoto ya kujipanga kutafuta fedha kwaajili ya kulipia mashabiki wao kuingia uwanjani kutokana na mfumo mpya wa uingiaji uwanjani kwa kutumia tiketi za kielektroniki kutotoa nafasi ya mashabiki kuingia bure. Ofisa habari wa shirikisho la soka nchini(TFF) Boniface Wambura ametoa tahadhari hiyo leo katika semina ya siku moja iliyolenga kujifunza matumizi ya tiketi mpya za Kielektroniki zitakazofanyiwa majaribio katika mchezo wa kirafiki kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons jumamosi hii. Wambura amesema mfumo huo mpya hautotoa nafasi kwa vikundi vya mashabiki wa timu kuingia bure uwanjani kama ilivyokuwa awali badala yake timu husika italazimika kuvilipia vikundi hivyo iwapo itaona umuhimu wa kushangiliwa. Amesema ni muhimu vilabu vya soka vikatambua kuwa siku zote mabadiliko huja na changamoto zake hivyo kujipanga kunahitajika ili kukabiliana na changamoto zitakazo jitokeza. Hata hivyo katika semina hiyo iliyowahusisha wanahabari,viongozi wa vyama vya soka na viongozi wa timu kuliibuka changamoto ya mashabiki wa timu za majeshi kutumia ubabe kuingia viwanjani ambapo wadau waliishauri TFF kujipanga vilivyo kukabiliana na hali hiyo. Baadhi ya wajumbe wamesema timu hizo zimekuwa zikija viwanjani zikiwa na mashabiki kutoka ambao ni askari kutoka kambi zao za jeshi na mara nyingi wanapofika milangoni wamekuwa wakitishia walinzi na wao kulazimika kuwafungulia. Akijibu hoja hiyo,Wambura amesema TFF inalipokea hilo kama changamoto na miongoni mwa mikakati itakayofanyiwa kazi ni pamoja na kukutana na uongozi wa timu za majeshi ili kusaidia kutoa elimu.

No comments:

Post a Comment