Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, February 27, 2018

wanahabari Rukwa wanusurika kifo katika ajali

Waandishi watatu wamejeruhiwa katika baada ya gari aina Land Cruiser kuacha njia na kudumbukia kwenye Kolongo lililokuwa kando ya barabara ya Ilemba kuelekea  Kalambanzite wakati wakitoka ziarani na mkuu wa mkoa wa Rukwa.

Waandishi waliojeruhiwa ni Willroad Sumia wa kituo cha Channel 10 ambaye anadai kupata maumivu makali sehemu za kichwa, ambapo amelazwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU) Katika hospitali ya mkoa wa Rukwa.

Wengine ni Juddy Ngonyani (Azam TV)  na Peti Siyame (Dailynews) ambao waliruhusiwa mara baada ya kufika hospitalini hapo.

Kwa mujibu wa mmoja wa majeruhi hao,  Juddy Ngonyani, ajali hiyo imetokea nyakati za mchana katika kijiji cha Ilembo wilayani Sumbawanga, Rukwa ambapo wanahabari hao walikuwa kwenye msafara wa mkuu wa mkoa wa Rukwa ambaye alifanya ziara ya kikazi eneo la Ilemba bonde la ziwa Rukwa.


Inadaiwa wakiwa njiani kuelekea mjini Sumbawanga dereva wa gari walilokuwa wamepanda wanahabari hao wakiwa na watendaji wengine wa serikali ngazi ya mkoa na wilaya alilikwepa kugongana na Lori la mizigo.

Pia gari hilo lilinusurika kugonga mti akiwa katika mwendo wa kasi ndipo aliingia kwenye Kolongo na gari hiyo kupinduka.

Licha ya wanahabari hao, baadhi watendaji wa serikali walipata majeraha ni kaimu Mganga mkuu wa mkoa, Emmanuel Mtika na Katibu uenezi wa CCM mkoa wa Rukwa,  Clement Bakuli ambao nao wamepumzishwa hospitalini hapo wakipatiwa matibabu.

Tuesday, February 20, 2018

MKANDARASI UWANJA WA SONGWE KUFIKISHWA MAHAKAMANI











Chini-Naibu waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi ,Mhandisi Atashasta Nditiye(katikati) akikagua picha za jengo la abiri la uwanja wa ndege Songwe alizopiga kwenye simu yake baada ya kutoridhishwa na kazi ya ujenzi wa jengo hilo
SERIKALI imeiagiza Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini(TAA) kuipeleka mahakamani kampuni ya DB Shapraya kwa kushindwa kutekeleza kwa wakati kazi ya ujenzi wa Jengo la Abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo mkoani Mbeya.

Serikali pia imeagiza TAA kuanza kukata fedha kama adhabu ya kuchelewesha mradi kuanzia Januari 30 mwaka huu kwa kampuni hiyo ambayo licha ya kulipwa fedha zote na Serikali imeshindwa kutekeleza mradi huo.

Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano,Mhandisi Atashasta Nditiye alitoa maagizo hayo juzi(jumamosi) alipofanya ziara ya kushitukiza katika uwanja wa Songwe na kukuta hakuna kazi yoyote inayoendelea.

Nditiye alisema ni jambo lisilokubalika kuona fedha ya watanzania iliyolipwa ikiendelea kuchezewa kwa miaka mitano huku kazi iliyotarajiwa kufanyika ikiendelea kupigwa danadana.

“Mkataba ulielekeza kwamba hili jengo liishe ndani ya miezi minane.Kulitokea matatizo ya hapa na pale,kubalilisha design na design ikabadilishwa kweli kukawa na delay ya mabadiliko na ilikubalika kwa pande zote mbili.Lakini vile vile kukawa na tatizo la kifedha kutoka Serikalini sababu zikatolewa mkandarasi akazielewa na Serikali ikazielewa.”

“Ikafika mahali 2015 mapema mwezi wa pili pesa flani ya ajabu ajabu ikatoka kwaajili ya kumpatika mkandarasi ajenge amalizie hili jengo lakini tangu kipindi hicho apate hiyo pesa kwanza yeye mwenyewe alikuwa haamini ameipataje pataje!Kwa maneno yao lakini wao wanajua waliipataje kwa sababu kwa bahati mbaya au nzuri kuna ujanja ujanja mwingi sana ulikuwa unatumika hapa siku za nyuma”

“Lakini mpaka saa hizi ninavyoongea ni kwamba hawa watu hawaidai Serikali fedha yoyote .Sasa hivi Serikali ndiyo inawadai kwa hatua iliyofikiwa.Nawashauri waache kufanya kazi kiujanja ujanja na nitataka TAA kuanzia tarehe 31 ambayo ni deadline waliyopewa na waziri waanze kukata hasara inayotokana na kuchelewesha kazi” alisisitiza naibu waziri

Alisema kwa hali aliyoiona baada ya kutembelea mradi huo mkandarasi huyo hata angeongezewa muda zaidi mwaka huu ungemalizika pia pasipo jengo hilo kukamilika na hata mwakani pia hivyo hakuna sababu ya kuendelea na kazi hiyo.

“Nimeingia hapa hakuna shughuli yoyote inayoendelea ninyi wenyewe mmeona. Tulichofanikiwa ni kuvalishwa haya manguo na kupewa makofia lakini hakuna kazi,sehemu yenye kazi ninyi wenyewe mnajua inavyokuwa imechangamka.Hakuna mafundi tumekuta hawa wasimamizi tu ambao nao ni wageni hata hawajui lolote wana miezi mitatu”

“Nimemuona mkandarasi mshauri naye yuko hapa naye amekuja kwakuwa amejua nakuja hana maelezo yoyote kwa ujumla.Ataniambia nini wakati mkandarasi hayupo kwenye site.Taa wajiandae kumpeleka mahakamani”

Nditiye alisema lengo la Serikali ni kuona miradi inayotakiwa na wananchi inafanyika na kumalizika kwa wakati,hivyo kwa mradi huo atatafutwa mkandarasi mwingine tatakayemalizia ujenzi huo ndani ya mwaka huu.

“Tunataka awamu hii kuonyesha kwa vitendo kuwa tunafanya kazi za wananchi.Na tumejipanga kweli kufanya kazi za nchi.Mh Rais halali anatafuta pesa,pesa inalipwa mtu hataki kufanya kazi anakimbia site.Tutahakikisha hizi pesa anazitema na kweli tutahakikisha zinarudi hizi pesa na hili jengo litaisha kwa wakati tunaohitaji sisi”

Naibu waziri huyo alilaumu hatua ya baadhi ya wakandarasi wazawa kutowajibika kwa kazi wanazopewa licha ya Serikali kuwapa upendeleo ikiamini fedha izaowalipa zitabakia hapa nchini na kuwaongezea mitaji watanzania.

Alisema hatua stahiki dhidi ya mkandarasi huyo haitoishi kumfikisha mahakamani na kumtoza adhabu ya fidia ya kuchelewesha mradi bali pia kumshitaki katika bodi ya makandarasi nchini ili nayo ichukue hatua stahiki.

Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa viwanja vya ndege vya mikoa,Joseph Nyahende alisema mradi huo ulikuwa wa kukamilisha kazi tatu ambazo ni ujenzi wa maegesho ya ndege,barabara na jengo la abiria.

Alisema ulikuwa ni mkataba wa shilingi bilioni 11 na hadi Desemba mwaka jana Bilioni 9.7 zilikuwa zimelipwa kwa mkandarasi hivyo kwa hatua ya kazi iliyofikiwa mkandarasi huyo haidai Serikali bali anadaiwa kazi.

Kwa upande wake Mkandarasi mshauuri kutoka kampuni ya Unitec ya nchini Dubai,Mhandisi  Silanda Dustan alisema kinachoonekana ni mkandarasi kushindwa kutekeleza majukumu ya kazi aliyopewa wakati wananchi wanamatumaini na wanasubiri miundombinu ili wakuze uchumi wao.

“Sisi tumeshauri Serikali kuwa mkandarasi hawezi tena kufanya kazi hii hivyo ni wakati kuchukua hatua zinazostahiki.Hayupo kazini.Kuna hiyo hasara ya kuchelewa kwa mradi.Kama abiria wangekuwa wanapita hapa Serikali ingepata kodi na pesa ya wananchi iliyotolewa kwaajili ya ujenzi huu ingekuwa imeanza kurudi sasa”

Naye mwakilishi wa mkandarasi mhandisi George Ngutoto alisema ana uhakika iwapo Serikali ingewaongeza fedha nyingine hadi juni 30 mwaka huu mradi huo ungekamilika na kukabidhiwa kwa Serikali.


Friday, February 16, 2018

HABARI NJEMA KWA WAKAZI MKOANI ARUSHA NA MAENEO YA JIRANI

Now Open!Quick Dry Cleaner ndo suluisho la usafi wa nguo zako,tupo nane nane ndani Njiro Arusha,mteja tunakufata ulipo.Karibuni Sana.

RC MAKALLA APOKEA MSAADA WA VYUMBA VYA MADARASA

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla akikata utepe kuashiria kupokea vyumba viwili vya madarasa na kimoja cha Ofisi ya walimu vilivyojengwa kwa msaada mkubwa wa Kampuni inayojishughulisha na unuzuzi wa zao la Kakao wilayani Kyela ya Kim’s chocolate(Belgium) Bioland International katika Shule ya msingi Ngana wilayani hapo.Wengine ni maafisa kutoka kampuni hiyo na Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudia Kita.


Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ngana wikicheza kwenye hafla ya kupokea vyumba vya madarasa shuleni kwao.





MKUU wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla amepokea vyumba viwili vya madarasa na kimoja cha Ofisi ya walimu vilivyojengwa kwa msaada mkubwa wa Kampuni inayojishughulisha na unuzuzi wa zao la Kakao wilayani Kyela ya Kim’s chocolate(Belgium) Bioland International katika Shele ya msingi Ngana iliyopo wilayani humo.

Makalla pia amepokea madarasa vyumba viwili vya madarasa vilivyojengwa na Kampuni hiyo katika Shule ya Msingi Lubele iliyopo katika kata ya Ikimba.

Kwa mujibu wa Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela,Mwalimu Polemone Ndarugiliye ujenzi wa vyumba vitatu katika shule ya msingi Ngana ulioambatana na ukarabati wa vyumba vingine viwili shuleni hapo uligharimu Shilingi 23,271,000 ambapo kampuni ya Bioland ilichangia Shilingi 17,000,000 sawa na asilimia 73.1,wananchi Shilingi 5,128,000 sawa na asilimia 22 kupitia nguvu kazi.

Mwalimu Ndarugiliye alisema Serikali kupitia fedha za mfuko wa jimbo ilichangia shilingi 600,000 sawa na asilimia 2.6 na Shule ya Msingi Ngana kupitia fedha za ruzuku ikachangia Shilingi 534,000 sawa na asilimia 2.3.

Alisema kwa Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya msingi Lubele uliogharimu Jumla ya Shilingi 14,756,500 mchango wa Kampuni hiyo ni Shilingi 9,821,000,wananchi kupitia nguvu kazi Shilingi 4,352,000,Diwani Shilingi 682,000 na madhehebu  mbalimbali ya dini Shilingi 201,000.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo,Makalla aliwataka wakazi wilayani hapa kuendelea kushirikiana kwa karibu na Kampuni hiyo kwakuwa inaonyesha jitihada nzuri za kuboresha miundombinu ya Elimu.

“Ukibebwa uwe tayari kutoa ushirikiano.Hawa wanaendelea kutuchangia kwakuwa na ninyi mmekuwa mstari wa mbele kushiriki katika utekelezaji wa miradi inayoanzishwa kwenye maeneo yenu.Lakini pia hili ni fundisho kuwa kama watu wa kutoka mataifa mengine wana utayari wa kuchangia maendeleo ya kumkomboa mtoto wa hapa Kyela kielimu kwa nini wewe mtanzania wa haapa ugome?”

“Lakini ni muhimu pia kutambua kuwa kinachotukutanisha na wadau hawa ni zao la Cocoa.Sasa ni wakati kwetu kutambua kuwa zao hili lina faida hivyo tuhakikishea tunalima zaidi ili siku zijazo hawa washawishike kuja kujenga kiwanda japo cha kuchakata zao hili katika hatua za awali hapa kwetu”alisisitiza Makalla.

Kwa upande wake Afisa kutoka Kampuni ya Bioland,Fons Maex alisema kampuni bado ina utayari wa kuendelea kusaidia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu katika Shule zote za msingi zilizopo kwenye Halmashauri za Kyela,Rungwe na Busokelo.

“Mmeomba majengo mengine hapa Ngana.Nimechungulia leo kwenye kapu langu nimeona bado nina fedha za kutosha.Tutajenga hapa jengo litakalokuwa na vyumba viwili vya madarasa na pia maktaba na stoo.Kama mko tayari tuanze kesho ujenzi.Lakini pia shule mpya mnaotaka kuipachua kutoa shule ya msingi Kasumulu tunaahidi tutajenga madarasa nane.Ninyi andaeni utaratibu tu sisi tuanze kazi”alisisitiza Maex.

Thursday, February 15, 2018

MBARALI WAIPONGEZA SERIKALI KUPELEKA ZAO LA KOROSHO

 Mkuu wa wilaya ya Mbarali,Reuben Mfune akigawa miche ya Korosho kwa wakazi wa vijiji vilivyopo katika kata ya Mawindi tayari kuanza kilimo cha zao hilo wilayani humo.
 Mkuu wa wilaya ya Mbarali,Reuben Mfune akipandikiza Mche wa Korosho kama ishara ya Uzinduzi wa kilimo cha zao hilo kwenye hafla fupi ya uzinduzi kiwilaya iliyofanyika katika kijiji cha Manienga kata ya Mawindi.
WAKAZI wa Vijiji vilivyopo katika kata ya Mawindi wilayani Mbarali,wameishukuru Serikali kwa kuwapelekea zao la Korosho wakisema kwa miaka mingi hawakuwa na zao la biashara.

Wakazi hao wamesema kutokana na eneo lao kutofaa kwa kilimo cha zao la Mpunga kwa miaka yote wamekuwa wakilazimika kulima mahindi na mazao mengine kama alizeti na karanga ambayo hayajawa na faida kubwa kwao.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mkandani kata Mawindi,Sadick Kimelei,alisema kufika kwa zao la Korosho kijijini kwao ni Mafanikio mengine makubwa kiwilaya kwakuwa wakati wakazi wakiendelea na shughuli nyingine watakuwa sasa wakisubiri baada ya miaka kadhaa kuanza kunufaika na Korosho.

“Haya ni mafanikio makubwa kiwilaya,kwa kijijini kwangu hatulimi mpunga kama maeneo mengine wilayani hapa.Nitakuwa kioo cha jamii ili wananchi wangu wapate matumaini kutoka kwangu.Nata kuona nakuja kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kunufaika na zao  hili.”alisema Mwenyekiti huyo wa kijiji.

Hata hivyo Kimelei aliuomba uongozi wa wilaya na wataalamu wa kilimo kuwatembelea mara kwa mara kijijini kwao ili kuwapa hamasa zaidi wananchi juu ya kilimo cha zao hilo.

Kwa upande wake Afisa ugani wa kijiji cha Manienga kilichopo katika kata hiyo,James Mgaya alisema baada ya wanakijiji kupata taarifa ya uwepo wa miche ya korosho inayogawiwa bure,wamehamasika kwa wingi na kila moja anataka kupanda zao hilo.

Nae Afisa ugani wa kata ya Mawindi,Samson Risbon alisema wananchi wa vijiji vyote vitano vya kata hiyo wamepokea zao hilo na tayari wakulima 86 wameandaliwa kuanza kupanda miti kwenye maeneo yao.

RC MAKALLA APIGA MARUFUKU AHADI ZA NDOA MASHULENI





WANAFUNZI wa Kike mashuleni wametakiwa kuepukana na Ahadi za kuonana baadaye kwakuwa kufanya hivyo kunaweza pia kuwasababishi kushindwa kufikia malengo yao ya baadaye.

Mkuu wa  mkoa wa Mbeya,Amos Makalla alipiga marufuku ahadi hizo aliupokuwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Madibira iliyopo katika kata ya Madibira wilayani Mbarali.

Makalla alisema kuna tabia iliyojengeka kwa wanafunzi wa vidato vya juu kuwarubuni waliopo vidato vya chini na kuwashawishi kuanzisha mahusiano ya kimapenzi kwa madai kuwa watawaoa baada ya kumaliza shule.

“Wapo wanafunzi wa kiume ambao kwa kuwa wapo kidato cha nne au cha sita wanaanza kuwadanganya mabinti walioko vidato vya chini..Ooooh unajua mimi ntatangulia kumaliza shule…kwahiyo usijali utakuta mimi nimeshakuandalia maisha hivyo nitakuoa.Hakuna kitu kama hicho na kuanzia leo usikubali ahadi ya namna hiyo”

“Muhimu ni kuzingatika kilichokuleta hapa shuleni.Malengo yako ya kuwa hapa ni nini? Haukuja kutafuta mchumba hapa ulikuja kusoma ili baadaye ufikie malengo yako. Hapa tuna wanasiasa na wataalamu mbalimbali sasa usikubali ndoto yako kufutika kwa ahadi ya kukuoa”alisisitiza Makalla.

Mkuu huyo wa mkoa pia alitoa muda wa wiki mbili kwa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali na Tanesco  kuhakikisha wanatatua changamoto ya kutopatikana kwa maji shuleni hapo kutokana na kutokana na kutofungwa kwa mashine ya kusukuma maji.


Alisema kutopatikana kwa maji safi na salama shuleni hapo kunahatarisha afya ya wanafunzi na walimu na pia kunasababisha changamoto ya kutumia muda mwingi kuyafuata maeneo ya mbali.

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA MBPC















Tuesday, February 13, 2018

ZIARA YA TAJATI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA KITULO

 Wanachama wa Chama cha waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji nchini(TAJATI) akipiga picha katika Maporomoko ya Mto Mwakipembo uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kitulo walipofanya ziara ya siku moja hifadhini humo.
Ziara ilianza namna hii.Hapa ni katika barabara kuelekea kijiji cha Kikondo kabla ya kufika ndani ya hifadjhi ya Kitulo. 
 Ni ziara iliyotawaliwa na hali ya ukungu wakati mwingi,huku ubaridi ukiwa wa hali ya juu pia. 

 Hatimaye ndani ya Hifadhi na hapa ndiyo sehemu iliyotumika kuwasubiri wenzetu waliobakia nyuma ili tuweze kuungana na kuanza ziara ndani ya hifadhi hii ya kipekee.