Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, March 31, 2012

SASA NI MKOANI RUKWA,KAAA TAYARI KUPATA HABARI ZAIDI NA MATUKIO YA MKOA WA RUKWA

Mwandishi mkuu wa mtandao huu wa kijamii Joachim Nyambo amewasili mkoani Ruklwa kwa ziara ya kikazi inayotarajiwa kuibua mambo mengi na kuwekwa bayana katika mtandao huu.Kwa habari na matukio zaidi endelea kuwa nasiUfukwe uliopo katika kijiji cha Kabwe mwambao mwa ziwa Tanganyika

WATATU KATI YA MAHABUSU WANNE WALIOCHIMBA UKUTA WA CHUMBA CHA MAHABUSU NA KUTOROKA WAKAMATWA

MKAZI wa Songwe,Mbeya Vijijini, Mkoani MbeyaVasco Lwenje (28)  mmoja wa wahabusu wanne waliotoroka kwa kuchimba ukuta wa Kituo cha kati cha jijini Mbeya Machi 22 mwaka huu amekamatwa.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunafikisha idadi ya watatu kati ya mahabusu wanne waliotoroka hivyo kazi iliyobakia ni ya kumtafuta mtuhumiwa mmoja.
 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Advocate Nyombi, amesema mtuhumiwa amekamatwa katika nyumba ya Bwana Reuben Sanga mkazi wa Iwindi nje kidogo ya mji mdogo wa Mbalizi, majira ya saa nne usiku Machi 29 mwaka huu alikoomba hifadhi.

Amesema kupatikana kwa Lwenje ni juhudi za jeshi lake pamoja na ushirikiano wa kiintelejinsia baina ya jeshi hilo na wananchi hadi kufanikisha kukamatwa mahabusu watatu kati ya wanne waliotoroka kwa muda wa juma moja tu.

Kamanda Nyombi ameongeza kuwa amesalia mahabusu mmoja aliyemtaja kwa jina la Jonas Jackson (28), mkazi wa Tunduma na mwenyeji wa Mbozi ambapo pamoja na Lwenje walikuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji.

Aidha amesema kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa Jonas Jackson, jeshi lake litatoa zawadi nono kwani pamoja na wengine waliorejeshwa mahabusu ni watu hatari sana.

Lwenje alikuwa kwenye nyumba ya Mzee Sanga ambako alipewa hifadhi na mzee huyo ambapo waliwahi kukutana gerezani, alipokuwa kifungoni kabla ya kuachiwa.

Hata hivyo Kamanda Nyombi amebainisha kuwa kukamatwa kwa Lwenje kunafanya jumla ya waliokamatwa kufikia watu watatu na kwamba mbali ya makosa ya mauaji watakabiliwa na kosa la kutoroka chini ya ulinzi wa dola.

Wednesday, March 28, 2012

CHADEMA YAMWAIBISHA MEYA MBEYA

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeongoza katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa uliofanyika Mbeya mjini jumapili iliyopita kwa kupata wajumbe wa mitaa 29 kati ya mitaa 47 iliyofanya uchaguzi huo.
Chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema kilichokuwa chama pekee cha upinzani katika uchaguzi huo kilipata wajumbe 16 wa mitaa na mingi kati ya mitaa hiyo ikiwa ni ile iliyopo katika kata ya Itiji anakotokea meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga.

Katika nafasi ya mwenyekiti wa mtaa wa Itiji anakotokea meya huyo ambaye pia ndiye katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM Mbeya mjini Chadema iliigalagaza CCM.

Msimamizi wa uchaguzi huo mkurugenzi mtendaji wa Juma Iddy akitangaza matokeo alisema katika kura 603za kumchagua mwenyekiti wa mtaa mgombea kupitia Chadema Ezekiel Kinga alipata kura 325 na wa CCM Athuman Chiba akapata kura 246 na kura 32 ziliharibika.

Kwa mujibu wa Iddy mgombea Kinga ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa huo awali lakini kutokana na tofauti kati yake na meya ikafikia hatua ya yeye kuvuliwa uanachama na ndipo nafasi hiyo ikabaki wazi.

“Kwa matokeo hayo mgombea kupitia Chadema ameshinda kuwa mwenyekiti wa mtaa wa Itiji.Kwa upande wa nafasi za wajumbe wa mitaa,kulikuwa na nafasi 47 za kujazwa katika mitaa 37” alisema.

Hata hivyo msimamizi huo alisema uchaguzi huo kwa nafasi za wajumbe utapaswa kurudiwa katika mitaa miwili kutokana na matokeo ya kura za wagombea zilizopigwa kugongana.

Tuesday, March 27, 2012

MABOMU YA KIGAMBONI

Ukweli umebainika kuwa kile kilichosadikiwa na wakazi wa kigamboni kuwa mabomu yanalipuka katika kambi ya jeshi ya Kigamboni hakikuwa na ukweli bali wanajeshi wa kambi hiyo walikuwa katika mazoezi ya upigaji mizinga lakini hawakuwaarifu wakazi wa maeneo ya jirani

SAFARI ZA NDEGE ZAZINDULIWA SUMBAWANGA.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya, akifungua mkutano wa mwaka wa wakurugenzi wa utawala na rasilimali watu na makatibu tawala wasaidizi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkoa huo (RDC) jana mjini Sumbawanga.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya akifuatilia moja ya mada katikamkutano wa mwaka wa wakurugenzi wa utawala na rasilimali watu na makatibu tawala wasaidizi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkoa huo (RDC) leo mjini Sumbawanga.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya, akizungumza na wananchi wa mji wa Sumbawanga  waliojitokeza katika uzinduzi wa safari za anga jana, pembeni yake ni walimu wawili waliofaulisha vizuri aliyesimama katika ni Morison Kibona wa shule ya Msingi Jangwani na pembeni yake ni Pius Nzwalil wa Sekondari ya Kantalamba. pia walimu hapo walipata ofa ya kusafiri na ndege hiyo kutoka Sumbawanga hadi Mkoani Mbeya.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya akiimba nyimbo ya kabila la kifipa sambamba na wanakikundi cha Katandala B cha mjini Sumbawanga jana muda mfupi baada ya kuzindua safari za anga kutoka Dar es salaam hadi Sumbawanga zinazofanywa na ndege ya Auric Air.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya akisalimiana wa viongozi mbalimbali wa Serikali muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Sumbawanga wakati wa uzinduzi wa safari za anga jana.
Katibu tawala wa mkoa wa Rukwa, Salum Chima akijiandaa kushuka katika ndege hiyo jana wakati wa uzinduzi wa safari za anga kutoka Dar es salaam kuelekea Sumbawanga.
Ndege ya Auric Air inayofanya safari kati ya Dar es salaam na Sumbawanga ikiwa imetua katika kiwanja cha ndege cha mjini Sumbawanga muda mfupi kabla uzinduzi rasmi wa safari hizo jana KWA HISANI YA pembezonikabisa.blogspot.com. 

HABARI MUHIMU KUTOKA TFF LEO

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
VITA VPL YAHAMIA MORO UNITED, VILLA
Timu za Moro United na Villa Squad ambazo ziko kwenye vita ya kukwepa kushuka daraja katika Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinapambana kesho (Machi 28 mwaka huu) kwenye moja kati ya mechi mbili za siku hiyo.
Mechi hiyo namba 153 itachezwa kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili. Moro United iko nafasi ya 11 ikiwa na pointi 18 wakati Villa Squad iko nafasi ya 14 kwa pointi zake 14.
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 kwa jukwaa kuu. Mwamuzi atakuwa Andrew Shamba akisaidiwa na Samson Kobe na Idd Mikongoti wote wa Dar es Salaam.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Arthur Mambeta wa Dar es Salaam wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Emmanuel Chaula kutoka mkoani Rukwa.
Mechi nyingine ya Machi 28 mwaka huu itakayochezeshwa na mwamuzi Judith Gamba wa Arusha itakuwa kati ya Ruvu Shooting itakayoikaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Gamba katika mechi hiyo namba 150 atasaidiwa na Saada Tibabimale kutoka Mwanza na Hellen Mduma wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa akiba ni Juma Safisha wa Pwani wakati Kamishna ni Hamis Kissiwa wa Dar es Salaam.
Mechi za Machi 31 mwaka huu ni Coastal Union dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wakati Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi ya African Lyon na Simba.
 
RHINO, POLISI DAR KUANZA FAINALI FDL
Timu za Rhino Rangers ya Tabora na Polisi Dar es Salaam zitapambana Machi 31 mwaka huu katika moja ya mechi za ufunguzi wa fainali za Ligi Daraja la Kwanza zitakazochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kila siku zitachezwa mechi mbili, moja ikianza saa 8 mchana wakati ya pili ni saa 10 jioni ambapo fainali hiyo itamalizika Aprili 22 mwaka huu kwa timu tatu za kwanza kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao- 2012/2013.
Morogoro imepewa uenyeji baada ya kulipa sh. milioni 20.5 kati ya sh. milioni 25 zilizotakiwa. Sh. milioni 4.5 zilizobakia imekubaliana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa itazilipa moja kwa moja kwenye huduma zitakazotumiwa na wasimamizi wa fainali hizo.
Mkoa mwingine ulioomba uenyeji ulikuwa Mbeya. Lakini wenyewe hadi Machi 26 mwaka huu ambayo ilikuwa siku ya mwisho kufanya malipo ulikuwa umeingiza kwenye akaunti ya TFF sh. milioni 15.
Upangaji ratiba (draw) ulifanyika jana (Machi 26 mwaka huu) kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kushuhudiwa na viongozi wa timu saba kati ya tisa zinazocheza fainali hizo.
Mechi ya pili siku ya ufunguzi itakuwa kati ya Trans Camp na Mbeya City Council. Aprili Mosi ni Tanzania Prisons na Polisi Morogoro zitakazocheza mchana wakati jioni ni Mgambo Shooting na Mlale JKT.
Aprili 2 mwaka huu ni Polisi Tabora vs Rhino Rangers (mchana) na Polisi Dar es Salaam vs Trans Camp (jioni). Aprili 3 mwaka huu ni Mbeya City Council vs Tanzania Prisons (mchana) na Polisi Morogoro vs Mgambo Shooting (jioni).
Aprili 5 mwaka huu ni Polisi Tabora vs Mlale JKT (mchana) wakati jioni ni Rhino Rangers vs Trans Camp. Aprili 6 mwaka huu Polisi Dar es Salaam vs Mbeya City Council (mchana) wakati jioni ni Tanzania Prisons vs Mgambo Shooting.
April 8 mwaka huu ni Mlale JKT vs Polisi Morogoro (mchana) wakati jioni itakuwa Polisi Tabora vs Polisi Dar es Salaam. Aprili 9 mwaka huu ni Mgambo Shooting vs Rhino Rangers (mchana) wakati jioni ni Trans Camp vs Tanzania Prisons.
Aprili 11 mwaka huu ni Mbeya City Council vs Polisi Tabora (mchana) na Mlale JKT vs Rhino Rangers (jioni). Aprili 12 mwaka huu Polisi Dar es Salaam vs Mgambo Shooting (mchana) na Polisi Morogoro vs Trans Camp (jioni).
 
LIGI YA TAIFA KUANZA APRILI 22
Kamati ya Mashindano ya TFF iliyokutana Machi 24 mwaka huu imepitisha michuano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa ianze Aprili 22 mwaka huu kwenye vituo vitatu tofauti.
Wakati Machi 26 mwaka huu ndiyo ilikuwa mwisho kwa vyama vya mikoa kuwasilisha TFF majina ya mabingwa wao, ni mikoa minne tu iliyomudu kufanya hivyo kwa mujibu wa kalenda ya matukio ya TFF.
Mikoa hiyo na mabingwa wake kwenye mabano ni Kigoma (Kanembwa FC ya Kibondo), Ruvuma (Mighty Elephant ya Songea), Kilimanjaro (Forest FC ya Siha) na Dodoma (CDA ya Dodoma Mjini).
Hivyo Kamati ya Mashindano imeongeza muda hadi Aprili 9 mwaka huu kwa mikoa ambayo haijawasilisha majina ya mabingwa wao iwe imefanya hivyo. Kwa itakayoshindwa ndani ya muda hiyo, mabingwa wao hawatapata fursa ya kucheza ligi hiyo.
Kamati imetoa pongezi kwa mikoa hiyo minne kwa kuhakikisha imechezesha ligi yao kwa mujibu wa kalenda ya matukio ya TFF. Pia imepanga makundi matatu ya ligi hiyo. Kundi A lina mikoa ya Rukwa, Mbeya, Ruvuma, Iringa, Morogoro, Lindi na Mtwara.
Kundi B lina mabingwa wa mikoa ya Kigoma, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Kagera, Singida na Dodoma. Kundi C ni Dar 1, Dar 2, Dar 3, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
TFF inakaribisha maombi ya uenyeji kwa kila kundi. Taarifa rasmi itatumwa kwa vyama mikoa kueleza masharti ya kutimiza kabla ya mkoa kupewa kituo cha ligi hiyo.
Mshindi katika kila kundi na washindwa bora (best losers) wawili kutoka kwenye makundi yenye timu nane watapanda daraja msimu ujao kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Pia timu zinatakiwa ziwe zimefanya usajili wa wachezaji kufikia Aprili 10 mwaka huu wakati Aprili 11-18 itakuwa ni kipindi cha kutangaza majina na pingamizi.
 
KOMBE LA FA KUANZA TENA MSIMU UJAO
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limerejesha tena mashindano ya Kombe la FA (TFF) kuanzia msimu ujao 2012/2013 ambapo bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Timu zinazotakiwa kushiriki michuano hiyo itakayochezwa kwa mtindo wa mtoano ni zilizosajiliwa ambapo katika maombi yao ni lazima ziambatanishe nakala ya hati ya usajili wa klabu ambayo itatakiwa kuidhinishwa na chama cha mpira wa miguu cha wilaya.
Ada ya fomu ya maombi ya kushiriki ni sh. 20,000 wakati ada ya mashindano ni sh. 200,000. Usajili wa wachezaji katika Kombe la FA ni ule ule mmoja wa kalenda ya usajili ya TFF ambapo unaanza Juni Mosi na kumalizika Septemba 10.
KWA HISANI YA MTANDAO

MWINGINE KATI YA WATUHUMIWA WA MAUAJI WALIOTOROKA AKAMATWA

MTUHUMIWA mmoja kati ya wale watatu wa mauaji walioshirikiana na mtuhumiwa wa wizi kuvunja chumba cha mahabusu ya kituo cha polisi kati jijini Mbeya na kutoroka amekamatwa.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema wenzake wawili bado hawajapatikanaa na jeshi hilo linaendelea na msako.
Amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Maneno Wiwa Kalinga ambapo yeye na wenzake wawili wanakabiliwa na tuhuma za mauaji lakini hivi karibuni wakiwa katika chumba kimoja cha mahabusu walitoboa ukuta na kutoroka pamoja na mahabusu mwenzao Fadhili Mwaiteleke(27) aliyekuwa anakabiliwa na tuhuma za wizi wa betri tatu za gari aliyekamatwa muda mfupi baada ya kutoroka.
Kamanda Nyombi amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa jana saa 10:00 alfajiri katika kijiji cha Ruanda Wilayani Mbozi na kikosi kazi cha askari wanaoendelea na msako wa kuwasaka watuhumiwa wengine wawili waliobaki.
Mahabusu hao walichimba ukuta wa chumba walimokuwa mnamo machi 22 mwaka huu usiku kati ya saa 8 hadi saa 9 huku askari waliokuwa zamu katika kituo hicho wakiwa hawajui lolote.

Kamanda Nyombi amesema mahabusu hao walitumia mbinu ya kulowanisha ukuta uliojengwa kwa tofali za saruji kuulainisha na baadaye wakatumia vipande vya nondo kuutoboa na kutoroka.

Sunday, March 25, 2012

NILIPOTEMBELEA SHULE YA SEKONDARI KIWANJA WILAYANI CHUNYA

Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatusi Kinawiro akifikiria jambo baada ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kulikataa jengo la hosteli akisema usakafiaji wake umechakachuliwa

SOMO LETU LEO

ALIYEZOEA KUNYIMWA HATA AKIPEWA HASHUKURU.

Saturday, March 24, 2012

SOMO LETU LEO

NI RAHISI KWA MTOTO KUWA BABA LAKINI KAMWE HAIWEZEKANI BABA KUWA MTOTO NA NDIYO MAANA YESU NI MUNGU LAKINI MUNGU HAWEZI KUWA YESU.

Friday, March 23, 2012

ABIRIA WA TAZARA WAKWAMA SIKU TATU SASA

ABIRIA 500 waliokata tiketi kwenye ofisi za Tazara mkoani Mbeya wakitarajia kusafiri kwenda mkoani Morogoro na Jijini Dar es Salaam kwa kutumia Treni ya Reli hniyo wamekwama kwa takribani siku tatu baada ya treni walilotegemea kusafiria kuchelewa kufika nchini Tanzania likitokea nchini Zambia.
 
Abiria hao waliokuwa wamekata tiketi tangu Machi 20, mwaka huu wameshindwa kusafiri baada ya kusota katika stesheni ya Tazara iliyopo Iyunga Jijini hapa kwa siku tatu wakiendelea kusubiri usafiri huo pasipo matumaini yoyote.
 
Baadhi ya abiria waliohojiwa katika stesheni hiyo walisema kuwa baada ya kukata tiketi Jumatano ya Machi 20 waliambiwa watasafiri siku hiyo hiyo lakini haikuwa hivyo badala yake waliendelea kubadilishiwa muda wa kuondoka ili hali treni halionekani kituoni hapo.
Waliongeza kuwa hata ilipofika siku ya pili viongozi hawakuweza kuwaeleza sababu zozote za msingi zaidi ya kubadilisha ratiba ya muda kwenye ubao wa matangazo ambao ulikuwa ukionesha kuwa wataondoka siku hiyo hiyo baada ya muda mfupi lakini hali inabakia vile vile.
Abiria Agripa Mwamwezi ambaye ni Mchungaji alisema pamoja na kuwepo kwa sintofahamu ya usafiri huo muhimu kwa watumiaji hao bado viongozi hao waliendelea kukatisha tiketi hali ambayo iliendelea kuwaacha njia panda abiria hao.
Naye Robert Mwankusye alisema usumbufu walioupata ni gharama kuongezeka kwa sababu wengine wanasafiri na watoto na wametokea wilayani Ileje ambako ni pembezoni mwa mkoa wa Mbeya na hawana hata akiba ya fedha.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa viongozi wa Tazara Mbeya Jumanne Mnyawami ambaye pia ni Mhandisi mkuu wa wilaya ya TAZARA Mbeya alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alisema kilichokwamisha safari hiyo ni ajali ya treni ya mizigo iliyotokea usiku wa kuamkia Machi 20, mwaka huu.
Alisema ajali hiyo ilitokea kati ya stesheni ya Kiburuma na Chankaramu nchini Zambia ambapo treni la mizigo likitokea Tanzania kuelekea New Kapirimposhi  nchini humo kuanguka ambapo mabehewa matano yaliacha njia na kusababisha reli hiyo kutopitika hadi yatolewe mabehewa hayo.
Mnyawani alisema mabehewa hayo yalikuwa yamebeba mbolea hivyo ni kazi ngumu kuyaondoa na ndiyo maana umetokea usumbufu huo kwa abiria ambapo treni walilokuwa wafarie lilikuwa linatokea Nchini Zambia.
“ Nilipewa taarifa usiku wa kuamkia jumatano lakini hatukuweza kusitisha kukatisha tiketi kwa sababu hatukujua ukubwa wa ajali yenyewe kwa sababu ajali kama hizo hutokea mara nyingi ambapo hurekebishwa ndani ya muda mfupi na safari huendelea kama kawida lakini hii ya sasa ni kubwa kwa sababu waliomba mafun di kyutoka huku ambapo tulipeleka timu ya mafundi wane na behewa moja la vifaa lakini walirudishwa njia wakidai wataweza kutengeneza mafundi wa kutoka Zambia.” Alisema Mnyawani.
Aliongeza kuwa usumbufu uliojitokeza hata wao hawakutegemea kwa sababu kinachowasumbua ni mawasiliano kati ya Zambia na wao kuwa magumu ambapo wanashindwa kuwaambia abiria muda sahihi wa kusafiri kwa sababu hatra wao wanakuwa hajapewa muda stahili na Station Master.
Aidha  hadi tunaingia mtamboni treni hilo lilikuwa halijafika stesheni hapolicha ya kueleza taarifa za uhakika kuwa lingefika majira ya saa 12:45 Machi 23 mwaka huu ambapo abiria wote hao wangeweza kusafiri hivyo hufu ya abiria hao imeendelea kutanda huku wengine msaada kwa wasamaria wema wa kupewa msaada wa chakula.
KWA HISANI YA www.kalulunga.blogspot.com

WANANCHI WAHOJI WATUHUMIWA WA MAUAJI KUVUNJA MAHABUSU NA KUTOROKA

TUKIO la watuhumiwa wanne wa mauaji na mmoja wa wizi kuvunja mahabusu ya kituo kikuu cha polisi kati jijini hapa na kutoroka limepokelewa kwa hisia tofauti na wakazi mkoani Mbeya ambapo baadhi wameonesha wasiwasi wa kuhusika kwa baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi.
Wakazi hao wameonesha kuhusisha ushiriki wa baadhi ya aaskari wa jeshi hilo kutokana na maelkezo ya kanmaanda wa Polisi Advocate Nyombi aliyoyatoa kwa wawakilishi wa vyombo vya habari jana(Machi 22) alipozungumza nao juu ya tukio hilo.

Maswali wanayohoji wakazi hao ni namna gani ukuta uliojengwa kwa tofali la saruji (Block) na kisha kusakafiwa kwa saruji unavyoweza kulainishwa na maji mpaka likalainika na mtu akaweza kuutoboa kwa vipande vya nondo.

“Nadhani hapa kuna haja ya polisi kutupa maelezo mengine lakini si ya kulowanisha kwa maji ukuta tena uliopigwa lipu na una tofari za block .Nijuavyo mimi tofali la saruji linapomwagiwa maji linaimarika zaidia.Basi tukubali kuwa mkandarasi aliyejenga jengo hilo ambalo hata muda mrefu halijamaliza alichakaachua na inabidi achukuliwe hatua kwa kutumia tofali zinazoweza kulainika kwa kumwagiwa maji,nan i kwa ukuta wa mahabusu” alisema mmoja wa wakazi hao Julius Kapandila.

Kapandila aliendelea kuhoji iwapo mahabusu walitumia maji ya bomba ni njia ipi waliyokuwa wakiitumia kuchota maji hayo na kumwagia ukuta mpaka ukalowa kiasi cha kulainika na kuwa rahisi kuchimbwa.

Mkazi mwingine Joseph Mwambene alihoji namna vipande vya nondo vilivyodaiwa kutumika kuchimba ukuta huo viliingizwa vipi katika chumba cha mahabusu hao iwapo kuna ulinzi wa kutosha katika kituo hicho kama si baadhi ya askari kituoni hapo kuviingiza wao wenyewwe kupitia mlangoni.

Wapo pia waliohoji  umakini wa askari waliokuwa zamu usiku huo wakisema si jambo la kawaida ukuta imara ukaendelea kuchimbwa tena kwa vipande vya nondo na wao wasisikie vishindo hasa kwa ukuta unaoaminiwa kuwa imara kama wa chumba kinachotomika kwaajili ya mahabusu.

“Na kama utaratibu wao ni kukagua kila baada ya saa moja kupita iliwezekana vipi katika muda mnfupi mahabusu hawa wamwagie maji ukuta,ulainike,wachimbe kwa vipande vya nondo na wakatoroka wasigundue.Hapa ni mawili huenda wao pia walihusika ama basi walikuwa wamelala” alisema mkazi mmoja aliyeomba kutotajwa jina lake.

Kwa mujibu wa kamanda Nyombi tukio la kutoboa ukuta na kukimbia kwa mahabusu wanne lakini kati yao mtuhumiwa wa wizi pekee baadaye akakamatwa na watatu wa mauaji wakaatokomea kusikojulikana lilitokea usiku wa kuamkia machi 22 mwaka huu majira ya kati ya saa nane na tisa usiku.

Habari kutoka ndani ya jeshi hilo zinaeleza kuwa askari watano wanashikiliwa kutokana na tukio hilo kutokana na kushindwa kudhibiti lindo lao na hatimaye mahabusu hao kutoroka.

Waandishi wa habari mkoani hapa jana walifika katika ofisi ya kamanda Nyombi ili kupanda undani wa habari za kushikiliwa kwa askari hao na pia hatuaa iliyofikiwa katika kuwatafuta watuhumiwa watatu wa mauaji lakini walikaa muda mrefu pasipo mafanikio ya kukutana na kamanda huyo mpaka walipoamua kuondoka.

Thursday, March 22, 2012

WATUHUMIWA WA MAUAJI WAVUNJA MAHABUSU NA KUTOROKA


WATUHUMIWA wanne kati yao wakiwemo watatu wa kesi ya mauaji wamevunja mahabusu ya kituo cha kati (Central) Mbeya na kutoroka.
Kamanda wa polisi mkoani  Mbeya Advocate Nyombi  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo alilosema limetokea usiku wa kuamkia leo machi 22 majira ya usiku wa manane kati ya saa nane na saa tisa hivi.

Amesema kati ya watuhmiwa hao watatu ambao hakuwataja majina wanakabiliwa na kesi moja ya mauaji na mmoja aliyemtaja kwa jina la Fadhil Mwaiteleke(27) mkazi wa Ilomba jijini Mbeya anakabiliwa na tuhuma za wizi wa betri tatu za gari.

Amesema kwa pamoja watuhumiwa hao waliokuwa katika moja ya vyumba vipya vilivyoongezwa katika upanuzi na uboreshaji wa mahabusu ya kituo cha kati uliofanyika hivi karibuni walifungulia maji na kulainisha ukuta kwa kuumwagia maji kabla hawajatumia vipande viwili vya nondo kuchimba ukuta huo na kutoroka.

Amesema askari waliokuwa zamu ya usiku katika chumba cha mapokezi ya mashitaka kama kawaida yao ya kukagua mahabusu kila baada ya saa moja walifika katika chumba hicho na kusikia maji yakimwagika kwa wingi hali iliyoonesha bomba lilikuwa limeachwa wazi.

Baada ya kuchunguza walibaini kuwa mahabusu wanne waliokuwamo walikuwa wametoroka kupitia tundu lililochimbwa ukutani na kukuta vipande viwili vya nondo vilivyoachwa vinavyosadikiwa kuwa kuna mtu aliyeviingiza humo kutoka upande wan je kupitia matundu madogo yaliyopo upande wa juu wa ukuta

Kamanda huyo amefafanua kuwa baada ya askari hao kubaini kutoroka kwa mahabusu walitoa taarifa kwa vyombo vingine vya usalama na kwa ushirikiano wa pamoja usiku huo wakafanikiwa mahabusu Mwaiteleka akiwa katika jitihada za kutokomea mbali zaidi.