Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, March 21, 2012

MTOTO KIZIMBANI KWA KUMWINGIA MWENZAKE KINYUME NA MAUMBILE


Mtoto aliyefahamika kwa jina la Joseph Yusuph(16) mkazi wa Jacaranda jijini hapa amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Mbeya kwa kosa kumwingilia kinyume na maumbile mtoto mwenzie wa kiume.

Akisomewa shitka hilo na wakili wa serikali Rhoda Ngole mbele ya hakimu mkazi Zabibu Mpangule alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo mach 5 mwaka huu katika maeneo ya Jacaranda.

Mshitakiwa alikana shitaka na kupelekwa katika gereza la watoto baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 5mwaka huu.

No comments:

Post a Comment