Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, March 2, 2012

KYELA WACHARUKA WAMTAKA RAIS KIKWETE ATOE TAMKO UGONJWA WA MBUNGE WAO


WAZEE wilayani Kyela wanatarajia kuagiza timu ya watu kwenda kuonana na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ili awaeleze ukweli kuhusu ugonjwa wa mbunge wao Dk.Harison Mwakyembe.

Kadhalika wazee hao wanataraji kuandaa mandamano ya amani yatakayoshirikisha wakazi wote wa jimbo hilo lengo likiwa ni kuishinikiza serikali iweke bayana juu ya kinachomsumbua mbunge huyo.

Hayo yamefikiwa katika mkutano wa wazee na wilayani hapo uliolenga kutoa tamko la wakazi wa jimbo hilo ambapo wamelaaumu serikali kuruhusu migongano ya kauli juu ya ugonjwa wad k.Mwakyembe kwa kutotoa tamko la kuwafahamisha wananchi ukweli wa mambo.

No comments:

Post a Comment