Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, March 13, 2012

TIMU TATU ZAFUNGIWA MBEYA KUSHIRIKI MICHUANO YOYOTE ILE

Kamati tendaji ya chama cha soka mkoani Mbeya MREFA imepitia taarifa ya kamati ya mashindano na kufikia maamuzi ya kuziwajibisha timu nne kwa adhabu tofauti ikiwemo tatu kati ya hizo kufungiwa kutoshhiriki michuano yoyote katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Timu zilizofungiwa ambazo pia zitapaswa kuliopa faini ya shilingi 300,000 kila moja kuwa ni Ubaruku FC ya wilayani Mbarali,Sharp Heroes ya Mbeya vijijini na Red Scopion ya wilayani Kyela huku timu ya Juhudi FC ya Mbeya vijijini akisema itawajibishwa kwa kupewa barua ya onyo.

Timu hizo kwa nyakato tofauti wakati ligi ikiendelea kwenye makundi zilionyesha utovu wa nidhamu kwa kufanya makosa mbalimbali ikiwemo kujitoa wakati ligi ikiendelea.

No comments:

Post a Comment