Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, March 20, 2012

WAETHIOPIA 55 WAKAMATWA MBEYA

WAHAMIAJI haramu 55 raia wa Ethiopia wanashikiliwa na Idara ya uhamiaji mkoani Mbeya kwa kuingia nchini bila kibali.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Rashid Mtana amesema wahabeshi hao waliokuwa wanaelekea Afrika kusini walikamatwa usiku wa kuamkia leo (Machi 20)majira ya saa 9:45 usiku katika eneo la Itewe Jijini Mbeya katika barabara kuu Iringa-Mbeya.

Mtana amesema ofisi ya uhamiaji iilipata taarifa za kuwepo kwa wahamiaji hao haramu kutoka kwa raia wema ambao waliwaona wakishushwa katika eneo hilo kutoka kwenye lori la mizigo walilokuwa wakisafiria wakitokea uelekeo wa Dar es Salaam.

Amesema baada ya kupewa taarifa hizo, maofisa wa Uhamiaji walifika eneo husika majira ya saa 5:00 usiku na kuanza msako katika vichaka vilivyopo hapo na ilipofika saa 9:45 usiku wakafanikiwa kuwakamata raia hao wote 55 wakiwa wamejificha kichakani wakisubiri mtu ambaye ilikuwa awapelekee usafiri wa kuwawezesha kuendelea na safari

Afisa uhamiaji huyo amesema wahabeshi hao watafikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake na kuwa baada ya kumaliza adhabu itakayotolewa na mahakama, watarejeshwa idara ya Uhamiaji ili waweze kurudishwa nchini kwao.

No comments:

Post a Comment