Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, March 23, 2012

WANANCHI WAHOJI WATUHUMIWA WA MAUAJI KUVUNJA MAHABUSU NA KUTOROKA

TUKIO la watuhumiwa wanne wa mauaji na mmoja wa wizi kuvunja mahabusu ya kituo kikuu cha polisi kati jijini hapa na kutoroka limepokelewa kwa hisia tofauti na wakazi mkoani Mbeya ambapo baadhi wameonesha wasiwasi wa kuhusika kwa baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi.
Wakazi hao wameonesha kuhusisha ushiriki wa baadhi ya aaskari wa jeshi hilo kutokana na maelkezo ya kanmaanda wa Polisi Advocate Nyombi aliyoyatoa kwa wawakilishi wa vyombo vya habari jana(Machi 22) alipozungumza nao juu ya tukio hilo.

Maswali wanayohoji wakazi hao ni namna gani ukuta uliojengwa kwa tofali la saruji (Block) na kisha kusakafiwa kwa saruji unavyoweza kulainishwa na maji mpaka likalainika na mtu akaweza kuutoboa kwa vipande vya nondo.

“Nadhani hapa kuna haja ya polisi kutupa maelezo mengine lakini si ya kulowanisha kwa maji ukuta tena uliopigwa lipu na una tofari za block .Nijuavyo mimi tofali la saruji linapomwagiwa maji linaimarika zaidia.Basi tukubali kuwa mkandarasi aliyejenga jengo hilo ambalo hata muda mrefu halijamaliza alichakaachua na inabidi achukuliwe hatua kwa kutumia tofali zinazoweza kulainika kwa kumwagiwa maji,nan i kwa ukuta wa mahabusu” alisema mmoja wa wakazi hao Julius Kapandila.

Kapandila aliendelea kuhoji iwapo mahabusu walitumia maji ya bomba ni njia ipi waliyokuwa wakiitumia kuchota maji hayo na kumwagia ukuta mpaka ukalowa kiasi cha kulainika na kuwa rahisi kuchimbwa.

Mkazi mwingine Joseph Mwambene alihoji namna vipande vya nondo vilivyodaiwa kutumika kuchimba ukuta huo viliingizwa vipi katika chumba cha mahabusu hao iwapo kuna ulinzi wa kutosha katika kituo hicho kama si baadhi ya askari kituoni hapo kuviingiza wao wenyewwe kupitia mlangoni.

Wapo pia waliohoji  umakini wa askari waliokuwa zamu usiku huo wakisema si jambo la kawaida ukuta imara ukaendelea kuchimbwa tena kwa vipande vya nondo na wao wasisikie vishindo hasa kwa ukuta unaoaminiwa kuwa imara kama wa chumba kinachotomika kwaajili ya mahabusu.

“Na kama utaratibu wao ni kukagua kila baada ya saa moja kupita iliwezekana vipi katika muda mnfupi mahabusu hawa wamwagie maji ukuta,ulainike,wachimbe kwa vipande vya nondo na wakatoroka wasigundue.Hapa ni mawili huenda wao pia walihusika ama basi walikuwa wamelala” alisema mkazi mmoja aliyeomba kutotajwa jina lake.

Kwa mujibu wa kamanda Nyombi tukio la kutoboa ukuta na kukimbia kwa mahabusu wanne lakini kati yao mtuhumiwa wa wizi pekee baadaye akakamatwa na watatu wa mauaji wakaatokomea kusikojulikana lilitokea usiku wa kuamkia machi 22 mwaka huu majira ya kati ya saa nane na tisa usiku.

Habari kutoka ndani ya jeshi hilo zinaeleza kuwa askari watano wanashikiliwa kutokana na tukio hilo kutokana na kushindwa kudhibiti lindo lao na hatimaye mahabusu hao kutoroka.

Waandishi wa habari mkoani hapa jana walifika katika ofisi ya kamanda Nyombi ili kupanda undani wa habari za kushikiliwa kwa askari hao na pia hatuaa iliyofikiwa katika kuwatafuta watuhumiwa watatu wa mauaji lakini walikaa muda mrefu pasipo mafanikio ya kukutana na kamanda huyo mpaka walipoamua kuondoka.

No comments:

Post a Comment