Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, March 15, 2012

RC AWAJIA JUU WATENDAJI WAPIGA POROJO MAOFISINI

MKUU wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro  amekemea vitendo vya baadhi ya watumishi katika idara za serikali kugeuza ofisi zao vijiwe vya kupigia porojo badala ya kufanya kazi.

Kandoro amesema wapo baadhi ya watumishio ambao kwao majukumu waliyopewa ya kuzitumikia ofisi si jambo la msingi bali mazungumzo yasiyo na tija katika kuleta maendeleo ndiyo wamekuwa wakiyapa nafasi kubwa.

Mkuu huyo wa mkoa aliyasemaa hayo wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa serikali ya wilaya ya Rungwe,watumishi wa halmashauri,viongozi wa dini pamoja na baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo kabla ya kuanza ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema watumishi wazembe hao wamekuwa wakiingia maofisini na baada ya kusaini vitabu vya mahudhurio wanajikusanya na kuanza porojo za kujadili vituko vilivyotokea mitaani kwao ama kujadili matokeo ya mechi mbalimbaali hasa za ligi ya ulaya.

“Wakishaaingia na kusaaini kitabu cha maahudhurio kwao inatosha.Baada ya hapo wataanza kuzungumzia matokeo ya mpira,vurugu za waalimu kudai posho zao mpaka wakalala hapa ukumbini na mengine mengi pasipo kukumbuka wajibu wao”

Aliwataka watumishi hao kujiuliza lengo la wao kuajiriwa na serikali na kisha kupelekwa katika halmashauri husika ni nini na pia watambue malipo yao kwa kuendelea kulipwa fedha za umma wakati hawatekelezi wajibu wao yanafaa kuwa yapi.

Aliwataka pia watendaji na madiwani kufanya kazi kwa kushirikiana akisema hiyo ndiyo silaha pekee ya kuwawezesha kupiga hatua katika kuwasaidia wananchi kujiletea maendeleo.

Alisema pasipo upendo wa kushirikiana hakuana atakayefaanikiwa katika mikakati ya ofisi yake na badala yake yataendelea malumbano ambayo mwisho wake ni kuwaumiza wananchi wanaaotarajiwa mwongozo wao

No comments:

Post a Comment