Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, March 11, 2012

WAMUUA MAMA WA KAMBO WAKIMTUHUMU KUWA MCHAWI

JESHI la polisi mkoani Rukwa, linawasaka vijana wawili kwa tuhuma ya kumuua mama yao wa kambo kwa kumkatakata na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake wakimtuhumu kuwa ni mchawi.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda tukio hilo lilitokea machi 9 nyakati za usiku wa manane wakati mwanamke huyo aitwaye Mwashi Saida (70) mkazi wa kijiji cha Mkole wilayani Nkasi alipokuwa amelala na mumewe.
 Alisema kuwa vijana hao ambao majina yao yanahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi, wanadaiwa kuvamia nyumba hiyo usiku na kuvunja mlango kisha kuanza kumshushia kipigo kikongwe huyo.
Kwa kutumia mapanga ambapo walimkatakata sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo na kichwani hali iliyosababisha kutokwa na damu nyingi hadi alipofariki dunia kisha wao kutoweka na kuelekea kusikojulikana.

 Inasemekana kuwa, watu hao wakati wakitekeleza unyama huo baba yao mzazi walikuwa wamemfungia katika chumba kikingine ambapo mara baada ya kutimiza lengo lao walimfungilia na wao kutoweka.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa chanzo cha kuuawa kikatili kikongwe huyo ni kwamba alikuwa akimtuhumiwa kuwa ndiye aliyemuua mama yao mzazi kwa uchawi miaka miwili iliyopita.

 Hata hivyo mama mzazi wa watoto hao alifariki kwa kuugua kwa muda mfupi lakini siku ya msiba huo watoto hao wanadaiwa kuapa kulipiza kisasi kwa njia yoyote ile.
Kamanda Mwaruanda, alisema kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na watuhumiwa hao watakapokamatwa watafikishwa mahakamani mara moja ili sheria ichukue mkondo wake. 

NA MWANDISHI WETU,SUMBAWANGA

No comments:

Post a Comment