Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, March 4, 2012

TAARIFA YA VURUGU ZA POLISI NA WANANCHI-WANAHABARI WAENDELEA KUSOTA

NI MASAA MATATU SASA YAMEPITA TANGU WANAHABARI MKOANI MBEYA WALIPOJIKUSANYA OFISINI KWA KAMANDA WA POLISI MKOANI MBEYA



Lengo la wanahabari kukusanyika hapa ni kuitikia wito wa jeshi la polisi mkoani humo uliowaomba wafike ofisini hapo ili kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi atolee maelezo sakata la vurugu zinazopendelea katika kijiji cha Lupa ambapo nyumba tatu za polisi zinaelezwa kuchomwa moto na wananchi kwa kile kinachoelezwa ni hasuira zilizotokana na polisi wa kituo kidogo kilichopo kijijini hapo kusababisha kifo cha mwanafunzi utakayemsoma hapo chini
Tofauti na walivyoahidiwa kuwa ofisa huyo angekutana na wanahabari saa nnwe kamili leo asubuhi mpaka sasa hakuna jibu sahihi ya wapi alipo na baadhi wanaeleza bado yupo kijijini Lupa akizungumza na wananchi

Endelea kutembelea mtandao huu kwa habari zaidi juu ya sakala hilo.Lakini ili kukukumbusha soma hapa chini upate kisa na mkasa wa tukio la mauaji na kuchomwa nyumba za askari
Jeshi la polisi mkoani Mbeya limeendelea kujisiriba matope kwa kuendesha mauaji ya kiholela kwa raia ambapo jana askari wa jeshi hilo wamemuua mwanafunzi Said Msabaha wa shule ya Sekondari Lupa iliyopo wilayani Chunya mkoani hapa.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Lupa wilayani humo William Patrick Mbawala, ameuambia mtandao wa huu kuwa mwanafunzi huyo kabla ya kifo chake alikamatwa na askari hao akiwa na wenzake watatu kwa tuhuma za wizi wa simu Februari 29, mwaka huu na baadaye waliachiwa kwa dhamana.
Amesema baada ya kutolewa katika kituo kidogo cha Lupa, Marehemu alionekana kuwa hali yake imedhoofika na alipoulizwa alieleza kuwa alipokuwa kituoni hapo alipigwa na askari polisi jambo ambalo liliwalazimu kumpeleka katika zahanati ya kijiji hicho chini ya Mganga aliyemtaja kwa jina la Dr. Solomon.

No comments:

Post a Comment