Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, March 23, 2012

ABIRIA WA TAZARA WAKWAMA SIKU TATU SASA

ABIRIA 500 waliokata tiketi kwenye ofisi za Tazara mkoani Mbeya wakitarajia kusafiri kwenda mkoani Morogoro na Jijini Dar es Salaam kwa kutumia Treni ya Reli hniyo wamekwama kwa takribani siku tatu baada ya treni walilotegemea kusafiria kuchelewa kufika nchini Tanzania likitokea nchini Zambia.
 
Abiria hao waliokuwa wamekata tiketi tangu Machi 20, mwaka huu wameshindwa kusafiri baada ya kusota katika stesheni ya Tazara iliyopo Iyunga Jijini hapa kwa siku tatu wakiendelea kusubiri usafiri huo pasipo matumaini yoyote.
 
Baadhi ya abiria waliohojiwa katika stesheni hiyo walisema kuwa baada ya kukata tiketi Jumatano ya Machi 20 waliambiwa watasafiri siku hiyo hiyo lakini haikuwa hivyo badala yake waliendelea kubadilishiwa muda wa kuondoka ili hali treni halionekani kituoni hapo.
Waliongeza kuwa hata ilipofika siku ya pili viongozi hawakuweza kuwaeleza sababu zozote za msingi zaidi ya kubadilisha ratiba ya muda kwenye ubao wa matangazo ambao ulikuwa ukionesha kuwa wataondoka siku hiyo hiyo baada ya muda mfupi lakini hali inabakia vile vile.
Abiria Agripa Mwamwezi ambaye ni Mchungaji alisema pamoja na kuwepo kwa sintofahamu ya usafiri huo muhimu kwa watumiaji hao bado viongozi hao waliendelea kukatisha tiketi hali ambayo iliendelea kuwaacha njia panda abiria hao.
Naye Robert Mwankusye alisema usumbufu walioupata ni gharama kuongezeka kwa sababu wengine wanasafiri na watoto na wametokea wilayani Ileje ambako ni pembezoni mwa mkoa wa Mbeya na hawana hata akiba ya fedha.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa viongozi wa Tazara Mbeya Jumanne Mnyawami ambaye pia ni Mhandisi mkuu wa wilaya ya TAZARA Mbeya alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alisema kilichokwamisha safari hiyo ni ajali ya treni ya mizigo iliyotokea usiku wa kuamkia Machi 20, mwaka huu.
Alisema ajali hiyo ilitokea kati ya stesheni ya Kiburuma na Chankaramu nchini Zambia ambapo treni la mizigo likitokea Tanzania kuelekea New Kapirimposhi  nchini humo kuanguka ambapo mabehewa matano yaliacha njia na kusababisha reli hiyo kutopitika hadi yatolewe mabehewa hayo.
Mnyawani alisema mabehewa hayo yalikuwa yamebeba mbolea hivyo ni kazi ngumu kuyaondoa na ndiyo maana umetokea usumbufu huo kwa abiria ambapo treni walilokuwa wafarie lilikuwa linatokea Nchini Zambia.
“ Nilipewa taarifa usiku wa kuamkia jumatano lakini hatukuweza kusitisha kukatisha tiketi kwa sababu hatukujua ukubwa wa ajali yenyewe kwa sababu ajali kama hizo hutokea mara nyingi ambapo hurekebishwa ndani ya muda mfupi na safari huendelea kama kawida lakini hii ya sasa ni kubwa kwa sababu waliomba mafun di kyutoka huku ambapo tulipeleka timu ya mafundi wane na behewa moja la vifaa lakini walirudishwa njia wakidai wataweza kutengeneza mafundi wa kutoka Zambia.” Alisema Mnyawani.
Aliongeza kuwa usumbufu uliojitokeza hata wao hawakutegemea kwa sababu kinachowasumbua ni mawasiliano kati ya Zambia na wao kuwa magumu ambapo wanashindwa kuwaambia abiria muda sahihi wa kusafiri kwa sababu hatra wao wanakuwa hajapewa muda stahili na Station Master.
Aidha  hadi tunaingia mtamboni treni hilo lilikuwa halijafika stesheni hapolicha ya kueleza taarifa za uhakika kuwa lingefika majira ya saa 12:45 Machi 23 mwaka huu ambapo abiria wote hao wangeweza kusafiri hivyo hufu ya abiria hao imeendelea kutanda huku wengine msaada kwa wasamaria wema wa kupewa msaada wa chakula.
KWA HISANI YA www.kalulunga.blogspot.com

No comments:

Post a Comment