Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, March 20, 2012

WAWILI WAUAWA KINYAMA MBEYA


WATU wawili wameuawa mkoani Mbeya katika matukio tofauti likiwemo la mkazi wa kijiji cha Igumila wilayani Ileje Jumapili Kasege(32) aliyekuwa  akitumikia kifungo cha miaka miwili nje kuuawa kwa kukatwakatwa  na vitu vyenye ncha kali na watu wasiofahamika
Kasege alikuwa akitumikia kifungo hicho kwa kosa la kutishia kuua kwa silaha na mpaka mauti yanamkuta alikuwa amekwishatumikia kifungo hicho kwa kipindi cha mwaka mmoja.
 
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amesema tukio hilo limetokea machi 19 mwaka huu majira ya saa 5 asubuhi katika kijiji cha Igumila na kwamba chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika na uchunguzi wa tukio unaendelea.

Katika tukio la pili kamanda Nyombi amemtaja marehemu kuwa ni mwanamke Sharuna Gimon(30)  mkazi wa kijiji cha Ndaga wilayani Rungwe aliyeuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani kutokana na wivu wa kimapenzi.

Amesema tukio hilo limetokea machi 19 mwaka huu, majira ya saa 4 asubuhi kijijini Ndaga baada ya mwanamke huyo kufumaniwa na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Yohana Mwazanga(35) mkazi kijijini hapo

Kufuatia tukio hilo kamanda Nyombi amesema watu wawili wanashikiliwa na kuwataja kuwa ni Bahati Musa(35) na Geofray Hezron(21) wote wakaziwa kijiji cha Ndaga wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment