Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Abbas Kndoro(kulia)na Afisa Mtendaji mkuu wa
kampuni ya Tigo Diego Gutierrez wakifurahi kwa kukalia moja ya dawati
700 zilizotolewa na kampuni hiyo kwaajili ya shule 32 za mkoani
Mbeya.
Afisa
Mtendaji mkuu wa kampuni ya Tigo Diego Gutierrez akizungumza lengo la msaada huo.Wednesday, September 30, 2015
Monday, September 21, 2015
IBADA YA KUWEKWA WAKFU ASKOF PANJA WA KANISA LA MORAVIAN
Maaskofu mbalimbali wakiwa mwombea kwa kumpa baraka Askofu wa kanisa la Moravian Jimbo
la kusini mchungaji Kenan Panja kwenye ibada maalumu ya kuwekwa wakfu askofu huyo iliyofanyika jumapili mjini Tukuyu wilayani Rungwe.
Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na maaskofu mara baada ya kuwasili uwanjani kwaajili ya ibada
Wachungaji mbalimbali wa kanisa la Moraviana wakiwa katika ibada
Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Mchungaji Samwel Kabigi akisoma risala ya kanisa mbele ya mgeni rasmi makamu wa Rais Dk.Bilali.
Kwaya ya Shalom ikitumbuiza katika ibada hiyo maalumu mbelea ya makamu wa Rais Dk.Bilali.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akitoa salamu za mkoa kabla ya kumkaribisha makamu wa Rais Dk.Bilali
Makamu wa rais Dk.Mohamed Gharib Bilali akimpongeza askofu Panja kwa kufikia daraja hilo la kiroho.Numa ya askofu na mkewe mama Panja.
Makamu wa Rais Dk.Bilali akihutubia waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria ibada hiyo ya kuwekwa wakfu kwa askofu Panja.
Askofu Panja akitoa neno la Shukrani mara baada ya kuwekwa wakfu.
Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na maaskofu mara baada ya kuwasili uwanjani kwaajili ya ibada
Wachungaji mbalimbali wa kanisa la Moraviana wakiwa katika ibada
Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Mchungaji Samwel Kabigi akisoma risala ya kanisa mbele ya mgeni rasmi makamu wa Rais Dk.Bilali.
Kwaya ya Shalom ikitumbuiza katika ibada hiyo maalumu mbelea ya makamu wa Rais Dk.Bilali.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akitoa salamu za mkoa kabla ya kumkaribisha makamu wa Rais Dk.Bilali
Makamu wa rais Dk.Mohamed Gharib Bilali akimpongeza askofu Panja kwa kufikia daraja hilo la kiroho.Numa ya askofu na mkewe mama Panja.
Makamu wa Rais Dk.Bilali akihutubia waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria ibada hiyo ya kuwekwa wakfu kwa askofu Panja.
Askofu Panja akitoa neno la Shukrani mara baada ya kuwekwa wakfu.
Friday, September 18, 2015
UZINDUZI WA UTALII WA NDANI KATIKA JIWE IGEREKE IRINGA
Mgeni rasmi Afisa
Utalii Tanapa Nyanda za juu kusini Risala Kabongo(katikati) akiwa na wanachama wa kikundi cha uhifadhi wa Mazingira Kihesa Kilolo( KIUMAKI) kwenye uzinduzi wa utalii wa ndani uliofanyika kwenye jiwe Igereke mkoani Iringa
Jiwe Igereke liko katika Mtaa wa Kihesa Kilolo manispaa ya Iringa
mkoani Iringa.Eneo hilo linasimamiwa na kikundi cha uhifadhi wa
Mazingira Kihesa Kilolo( KIUMAKI).Lengo la uzinduzi wa utalii huu wa ndani ni kuwahimiza wananchi wa Iringa kutembelea
vivutio vyao.
Katika uzinduzi huo pia Tanapa walikabidhi mipira kwaajili ya mchezo wa mpiara wa miguu kwa wanakikundi ili kuimarisha michezo na pia ushirikiano.
Monday, September 14, 2015
UKIRITIMBA WAKWAMISHA HALMASHAURI RUNGWE
KUTOFANYA kazi kwa umoja kwa watendaji katika
halmashauri ya wilaya ya Rungwe kumetajwa kuwa chanzo cha kudorola kwa utendaji
kazi ndani ya halmashauri hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alisema jana
kuwa taarifa alizonazo ni kuwa watendaji ndani ya halmashauri hiyo hawana
ushirikiano hata kidogo na badala yake kila mmoja anatekeleza majukumu yake
kivyake.
Hali hiyo ilijidhihirisha wazi pale watendaji
walipotakiwa kujibu maswali yaliyohojiwa na mkuuu wa mkoa yaliyotokana na hoja
za mkaguzi na ndipo kila afisa akaonekana kuwa na majibu yake na kuleta
mkinzano ndani ya kikao.
“Inaonekana hamfanyi kazi kama timu.Ninazo habari
kuwa hakuna umoja kati yenu.Kila mmoja anafanya mambo yake ajuavyo yeye.”
Alisema Kandoro kwenye kikao cha kupitia taarifa ya Mdhibiti na mkaguzi wa
hesabu za serikali(CAG) katika mwaka wa fedha 2013/2014.
Kandoro alisema hali hiyo ndiyo inayochangia kwa
kiasi kikubwa kukwama kwa shughuli za kimaendeleo na kuzalisha hoja nyingi za
kiukaguzi zisizo za msingi ndani ya halmashauri hiyo.
Aliwataka watendaji wa halmashauri hiyo kutambua
kuwa kufanya kazi kama timu ndiyo silaha pekee inayoweza kumwezesha kila mmoja
wao kuonekana anawajibika katika nafasi yake na hivyo maendeleo ya wananchi
kupatikana kwa urahisi.
Alisema anahitaji kuona wanafanya kazi kama timu
kuanzia ngazi ya mkurugenzi mtendaji,menejimenti,watendaji na mpaka kwenye kata
na vijiji huku wakitambua kuwa kilichowakutanisha ni kuwatumikia wananchi wa
Rungwe.
Akizungumzia suala la udhibiti wa mapato ya
ndani,Kandoro alisema bado inaonekana kuwepo kwa mianya ya upotevu wa fedha
hivyo si kiasi chote kinachokusanywa na halmashauri kinakwenda sehemu sahihi na
kuitaka ofisi ya katibu tawala mkoa kulifanyia kazi suala hilo.
Mkuu huyo wa mkoa pia aliagiza kutafutwa kwa
ufumbuzi wa haraka juu ya malalamiko yaliyofikishwa kwake na watumishi wa
halmashauri hiyo wakiwemo wa idara ya afya wanaolalamikia kukatwa mishahara yao
pasipo sababu za msingi.
Alisema hali hiyo inakwamisha utendaji kazi wa
watumishi na menejimenti kubaki ikitoa visingizio visivyo vya msingi pale
inapobainika wananchi kutopata huduma kikamilifu kwenye idara husika.
TBL YAALIKA WAFANYABIASHARA KUNUFAIKA NA KIWANDA MBEYA
WAFANYABIASHARA mkoani Mbeya wamehimizwa kutumia
fursa ya uwepo wa kiwanda cha bia cha TBL mkoani kwao kwa kujihusisha na
biashara zenye mahusiano na kiwanda hicho ili waweze kunufaika na uwepo wake.
Miongoni mwa fursa zilizopo ni pamoja na kuanzisha
viwanda kwaajili ya kusaga unga wa mahindi utumikao katika kutengenezea bia.
Meneja wa kiwanda cha TBL Mbeya Waziri Jemedari alitoa
hamasa hiyo alipozungumza na wanahabari mkoani hapa kwenye shindano la kuonja
na kutambua ladha ya bia lililofanyika kiwandani na kuwashirikisha wanahabari
kutoka vyombo mbalimbali.
Jemedari alisema bado wafannya biashara na wakulima
mkoani Mbeya hawajaitumia vyema fursa ya uwepo wa kiwanda hicho hatua
inayopelekea wenzao kutoka maeneo ya mbali kunufaika na fursa hiyo.
Alisema licha ya mkoa wa Mbeya kuwa miongoni mwa
mikoa inayozalisha kwa wingi mahindi,bado kiwanda hicho kinalazimika kuagiza
unga kutoka Arusha,Iringa,Kibaigwa na Dar es salaam.
“Wafanyabiashara wa Mbeya bado wamejikita katika
biashara nyingine ikiwemo ya kununua nafaka kutoka kwa wakulima na kuziuza tena
pasipo kuziongezea thamani.Hii inatulazimu kuagiza unga wa mahindi wa dona
kutoka mbali wakati hapa mahindi yanalimwa kwa wingi.”
“Nadhani hawajatambua uwepo wa kiwanda hiki
unavyoweza kuwanufaisha.Hatuwezi kufungua viwanda vya kusaga unga wa dona
kwakuwa tutakuwa tunawanytima wengine fursa.Sisi tunatengeneza bia,tunahitaji
wadau wengine wa kutuzalishia malighafi za kulisha kiwanda chetu” alisisitiza.
Alisema kwa sasa mahitaji ya unga wa mahindi wa dona
kiwandani hapo ni mkubwa ambapo jumla ya tani 30 hutumika kwa kila juma moja
hivyo ni fursa nzuri kwa watakaopenda kuwekeza kwenye uzalishaji wa malighafi
hiyo.
Alisema TBL iko tayari kukutana na mfanyabiashara
yeyote atakayeonesha nia ya kuwekeza katika biashara hiyo na itahakikisha
inampa mwongozo juu ya namna gani malighafi inayohitajika na kiwanda
inavyopaswa kutengenezwa.
Aliitaja fursa ya kilimo cha Shayiri kuwa faida
nyingine ambayo wakazi wa Mbeya hawajawekeza ipasavyo kwani hadi sasa kwa
mkoani hapa ni wakulima wa wilaya ya Mbozi pekee wanaozalisha huku kiwanda
kikilazimika kununua bidhaa hiyo kutoka maeneo mengine ikiwepo Sumbawanga
mkoani Rukwa.
Alisema licha yak ampuni kutoa fursa ya kuwawezesha
wakulima katika shughuli mbalimbali za uzalishaji wa zao hilo,bado mwitikio wa
wakulima mkoani hapa ni mdogo mno katika kilimo cha zao la Shayiri wakati soko
ni la uhakika.
Katika shindano la kuonja bia,mtangazaji wa Mbeya FM
David Nyembe anayekabidhiwa katoni ya bia aina ya Kilimanjaro Twist pichani aliibuka mshindi akifuatiwa na mwakilishi wa ITV mkoani hapa
Emmanuel Lengwa aliyeshika nafasi ya pili.
Tuesday, September 1, 2015
TANGAZO TANGAZO TANGAZO
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI
LA POLISI TANZANIA
RPC. Ofisi ya Kamanda wa
Polisi,
Mkoa wa
Mbeya,
Namba
ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax
- +255252503734
MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya.@tpf.go.tz
tanpol.mbeya@gmail.com
TANGAZO
KWA UMMA.
JESHI LA POLISI
TANZANIA LINAWAITA KWENYE USAILI WAHITIMU WALIOORODHESHWA WA SHAHADA,
STASHAHADA NA ASTASHAHADA. USAILI UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 03.09.2015 HADI TAREHE 04.09.2015 KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI HADI SAA KUMI JIONI KATIKA MAENEO
YAFUATAYO:-
·
FANI YA UTAWALA, UCHUMI, USIMAMIZI WA
SHERIA NA UTEKELEZAJI [BALE], UALIMU, UANDISHI HABARI, UHANDISI MADINI [MINING
ENGINEERING], UGAVI, LUGHA, USHAURI NASIHI, KATIBU MUKTASI, LAND SURVEY
CATHOGRAPHER NA GEOMATICS WATAFANYA USAILI
KATIKA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR ES SALAAM [DPA] KILICHOPO KANDO KANDO YA
BARABARA YA KILWA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM.
·
MAFUNDI MAGARI, MATENGENEZO YA PIKIPIKI,
MAFUNDI MATENGENEZO YA UMEME WA MAGARI [AUTO ELECTRICAL], MAFUNDI RANGI ZA
MAGARI, MAFUNDI MAGARI, MAFUNDI USHONAJI,MAFUNDI BODY ZA MAGARI NA MADEREVA. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA
POLISI UFUNDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES
SALAAM.
·
MATENGENEZO YA KOMPYUTA, FAX &
PHOTOCOPY MACHINES NA MAWASILIANO YA REDIO [DIPLOMA IN RADIO COMMUNICATION], USAILI WAO UTAFANYIKA NYUMA YA KIKOSI CHA
UFUNDI YAANI TEHAMA KEKO CHINI.
·
WAKEMIA, BAILOJIA [MOLECULAR BIOLOGY] USAILI UTAFANYIKA MAKAO MAKUU YA POLISI
YALIYOPO MAKUTANO YA BARABARA YA OHIO NA GHANA JENGO LINALOTAZAMANA NA POSTA
HOUSE.
·
KADA ZA AFYA USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA AFYA KILICHOPO KANDO KANDO YA
BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
·
MANAHODHA NA MAFUNDI MITAMBO WA MELI, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA
WANAMAJI KILICHOPO KARIBU NA JENGO LA MAHAKAMA YA RUFAA.
·
DAKTARI WA WANYAMA, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA MBWA NA FARASI KILICHOPO KANDO
KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
·
MAFUNDI AC ZA MAJUMBANI, ARCHITECTURE
DRAFTMAN, QUANTITY SURVEYORS, CIVIL ENGINEER, WELDING & FABRICATION, UMEME
WA MAJUMBANI, PAINTING, ALUMINIUM & GLASS WORK, PLUMBING, MOSONRY, MOTOR
REWINDING, HYDRO GEOLOGY DRILLING WELL, REFRIGERATION & AIR CONDITIONING. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA
POLISI UJENZI NDANI YA KAMBI YA POLISI BARRACKS KURASINI KANDO KANDO YA
BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.
·
FANI ZA BENDI, BRASS BENDI, WOODWIND,
STRING JAZZ NA PERCUSSIVE, USAILI WAO
UTAFANYIKA KIKOSI CHA BENDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI
DAR ES SALAAM.
·
FANI YA URUBANI,USAILI UTAFANYIKA KIKOSI CHA ANGA KILICHOPO UWANJA WA NDEGE
NDOGO WA ZAMANI WA J.K.NYERERE DSM.
MUHIMU:
1. MWOMBAJI
AFIKE KWENYE USAILI AKIWA NA NAKALA HALISI YA VYETI VYOTE VYA MASOMO/TAALUMA
[ACADEMIC TRANSCRIPT (S)/CERTIFICATE (S) YAANI KIDATO CHA NNE, SITA, CHUO NA
CHETI CHA KUZALIWA. KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIWA.
2. MWOMBAJI
ALIYEITWA KWENYE USAILI ATALIPIA GHARAMA ZA UPIMAJI AFYA SHILINGI ELFU KUMI
(10,000/=), USAFIRI, CHAKULA NA MALAZI KWA MUDA WOTE WA ZOEZI LA USAILI.
3. AMBAYE
HATAHUDHURIA USAILI KUANZIA SIKU YA KWANZA HATAPOKELEWA.
ILI
KUPATA/KUONA ORODHA YA MAJINA, TEMBELEA www.policeforce.go.tz
Imetolewa
na:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Subscribe to:
Posts (Atom)