Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, December 27, 2016

MBUNGE ATOA MSAADA WA BATI

 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipokea msaada wa mabati 2000 kutoka kwa mbunge wa Mbarali Phil Mohamed kwaajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa vyoo katika shule za msingi na sekondari wilayani Mbarali
 mbunge wa Mbarali Phil Mohamed

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla 

SERIKALI MKOANI SONGWE YATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI


 Mkuu wa mkoa wa Songwe,Luteni mstaafu,Chiku Galawa akiteketeza kwa kuchoma moto zana haramu zilizokamatwa katika oparesheni maalumu iliyofanywa na Halmashauri wilayani Songwe



SERIKALI mkoani Songwe imeteketeza Zana haramu za uvuvi zeye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 zilizokamatwa ndani ya ziwa Rukwa upande wa wilaya ya Songwe.

Mkuu wa mkoa wa Songwe,Luteni mstaafu,Chiku Galawa aliteketeza kwa kuchoma moto zana hizo zikiwemo Nyavu aina ya kokoro zenye matundu madogo ambazo zimekuwa zikisababisha kuvuliwa kwa samaki wadogo na pia kuharibu mazalia ya samaki.

Akizungumza na wananchi mjini Mkwajuni wakati wa zoezi la kuteketeza zana hizo,Galawa alisema Serikali haiku tayari kuendelea kuona uvuvi haramu ukiendelea ndani ya Ziwa Rukwa.

Alisema Serikali inahitaji kuona uvuvi unakuwa endelevu ndani ya ziwa hilo hivyo lazima iwe na mipango madhudhuti itakayowezesha mazingira rafiki ya kuzaaliana na kukua kwa samaki.

“Tunatambua mchango wa shughuli za uvuvi katika kuchangia uchumi wa mtu mmoja mmoja na serikali.Lakini uvuvi tunahohitaji ni ulio endelevu na si huu wa kuharibu mpaka mazalia ya samaki”

“Tutazidi kupambana na watu wote wanaotumia uvuvi haramu.Na wao pia wanapaswa kutambua athari za uvuvi huu.Wajue kuwa wakiendelea ipo siku tutakosa kabisa samaki ndani ya ziwa letu” alisema Galawa.

Mkuu huyo wa mkoa pia aliitaka halmashauri kuweka mkazo katika kusimamia sharia ya kutoingiza mifugo kwenye eneo oevu la ziwa Rukwa ili kulinda maeneo hayo muhimu kwa ustawi wa ziwa hilo.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi walioshuhudia shughuli ya uteketezaji wa zana hizo,waliipongeza serikali kwa hatua hiyo na kuishauri kuongeza nguvu zaidi ili oparesheni iwe ya kudumu.

Walisema kutokana na uvuvi haramu sambamba na kemikali zinazotoka kwenye machimbo ya madini,kumekuwepo na kupungua kwa kiasi kikubwa samaki ndani ya ziwa hilo hatua inayoonesha mwenendo mbaya wa shughuli za uvuvi kwa siku za baadae.

Friday, December 2, 2016

KIKONGWE APONZWA NA FEDHA ZA TASAF,AITWA MCHAWI NA KUTIMULIWA KIJIJINI

KIKONGWE anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 70 na 75  mkazi wa kijiji cha Tindingoma kata ya Chitete wilayani Momba mkoani Songwe amejikuta analazimika kulala porini na kwenye mapagara kwa siku mbili kwa hofu ya kuuawa na wakazi wenzake kwa tuhuma za ushirikina.

Akizungumza na mwandishi wetu jana, bibi kizee huyo aliyejitambulisha kwa jina la Agness Nakapange alisema kuwa ameamua kulala porini na kwenye mapagala kwa hofu ya kuuawa na wananchi wenzake ambao walimtisha kuwa watamuua endapo ataendelea kukaa katika nyumba yake.

Hata hivyo Nakapange aliyekataa katakata kujihusisha na masuala ya Kishirikina maishani mwake,alisema anachokiona ni wivu kutoka kwa baadhi ya majirani kutokana nay eye kuwa sehemu ya wanufaika wa Mpango wa kuokoa kaya Masikini unaoendeshwa na Mfuko wa jamii wa TASAF III

Nakapange alisema kuwa kuna wakati aliitwa na baadhi ya wananchi kijijini hapo wakimtaka awanunulie pombe za kienyeji walau nusu debe kwa lazima baada ya kumuona amepata fedha za TASAF.

Alisema wakazi hao walifanya hayo wakati wanajua dhahiri ya kuwa yeye ana wajukuu ambao wanamtegemea kwani watoto wake wote walifariki hivyo yeye na wajukuu zake hawana msaada wowote.

Alidai kuwa baada ya vitisho kuzidi nay eye kuona kuwa hali imekuwa mbaya alilazimika kununua pombe kwa kuhofia kuwa atauawa na wananchi hao kwani wakati wanazungumza naye walikuwa wakimzonga yeye ni mchawi na kuwa ndiye aliyeua wanae.

Akizungumzia sakata hilo,Afisa mtendaji wa kata ya Chitete Erasto Simchimba alikiri kumpokea bibi huyo katika ofisi zake jana majira ya asubuhi na kudai kuwa atakuwa naye katika ofisi zake mpaka pale atakapoitisha vikao na wananchi ili kutatua tatizo hilo.

Katika hatua nyingine Simchimba alisema tuhuma za Ushirikina anazopewa kikongwe huyo ni fitina tu na ni kukosa elimu kwa wananchi kwani tangu afike hapo hajawahi sikia kitu chochote kibaya kutoka kwa bibi huyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Tindingoma, Daniel Silungwe alidai kuwa yeye alikuwa hana taarifa hizo hivyo kuahidi kushughulikia tatizo hilo ambapo nae ameahidi kukaa naye nyumbani kwake ili kumnusuru  kutokana na kutishwa na wananchi.

WAJERUMANI WATENGENEZA FILAMU NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI


Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa (katikati) akizungumza na Mratibu wa uzalishaji wa filamu wa kampuni ya Polyphon ya nchini Ujerumani,Mona Lessnick alipotembelea eneo la Kogatende jirani na  Mto Mara ambapo kulikuwa kukifanyika shughuli za uchukuaji wa picha za video kwa ajili ya Tamthiliya ya Dream Boat, kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete.
......................................

HABARI KAMILI

Sekta ya Utalii nchini inatarajia kupiga hatua baada ya wasanii maarufu wa filamu kutoka nchi za nje kuanza kutumia baadhi ya maeneo katika vivutio vya Utalii vilivyoko nchini kuandaa sehemu za tamthiliyaa zao.


Kampuni kubwa ya utengezaji wa filamu ya Polyphon Group  ya Humburg  nchini Ujerumani imekuwa ya kwanza kupiga picha za video za sehemu ya tamthiliya maarufu nchini Ujerumani ya Dream Boat ambayo imekuwa ikiooneshwa katika vituo mbali mbali vya televisheni kwa nchi zinazozugumza lugha ya Kijerumani.

Maeneo ambayo picha za video zimechukuliwa ni pamoja na Kogatende na Lobo ndani ya Hifadhi za Taifa za Serengeti ,huku picha nyingine zikipigwa katika Hifadhi ya taifa ya Arusha pamoja na Pori la akiba Endumeti.


“Tumefanya Sehemu moja ya Tamthiliya yetu Botswana,moja Zambia na nyingine Kenya katika muendelezo wa tamthiliya hii inayooneshwa kwa mika 30 sasa,Sehemu ya mwisho ya muendelezo wa filamu hii iliyochukuliwa Afrika ilikua mwa 2007,ni muda mrefu na tuliangalia wapi tunaweza enda,na tukafanya utafiti ,tukaja Tanzania,Tumeona hii nchi ni nzuri tukaamua kuleta filamu yetu hapa”.alisema Manuel Schroeder mpiga picha wa kampuni ya Polyphon Studio.

Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa amesema hatua hii ni fursa nyingine muhimu kwa Tanzania  kutangaza vivutio vya utalii kimataifa huku mratibu wa uzalishaji wa filamu wa kampuni ya Polyphon,Mona Lessnick akieleza utalii utaongezeka kupitia tamthiliya hiyo.


“Kutokana na uzoefu ,watu wametuamini sisi , tumefanya hii kazi kwa miaka 30 sasa,hivyo baada ya kurusha sehemu ya tamthiliya ilichukuliwa hapa itaongeza soko la wageni kutoka nchi zinazozungumza kijerumani,kwa sababu wanajua tunafanya utafiti,tmekwisha fka hapa mara mbili na kukutana na mtaalamu na kutuonesha maeneo ,wanajua tunachukua maeneo mazuri,hoteli nzuri,tuna taarifa  na vifaa vya kutosha,hivyo kutakuwa na matokeo makubwa katika Utalii “alisema Lessnick.

Kuhusu Maudhui ya Tamthiliya hiyo ambayo inaoneshwa kwa zaidi ya miaka 30 sasa ,Mona Lessnick amesema imebeba maudhui ya aina tatu ambayo ni Vichekesho,Mahusiano pamoja na Drama.
“Ni Burudani kwa familia,tuna hadithi tatu,katika hadithi kuu watu wanasafiri kwa meli kuizunguka nchi,wakasafiri kuja Tanzania ,kuna hadithi nzuri za mahusiano ambazo vipande vyake vimechukuliwa Tanzania “alisema Lssnick.


“Katika muongozo tuna aina tatu ya hadithi,tuna hadithi ya mapenzi,tuna hadithi ya vichekesho na drama hii tunayofanya leo ni vichekesho,tuna watu wawili ,katika muongozo wa kwanza inaonesha watu haw wamepata tatizo katika gari lao hapa  Serengeti,lakini tulipaa ugumu kupiga picha ndio tukapata mahala hapa pazuri kwa kufanya video,tukafanya Drama hapa ya gari kukwama ndani ya maji na gari nyingine ikaja nyuma kuoka watu hawa wakiw wamekaa juu ya gari lao na kuondolewa katika maji”alisema Schroeder.

Tamthiliya ya Dream Boat imefikisha miaka 35 sasa tangu kuanza kurushwa katika vituo mbalimbali vya Televisheni nchini Ujerumani na kwamba sehemu mbili zenye urefu wa dakika 90 kila moja za tamthiliya hiyo ,picha zake hupigwa katika nchi moja ya kiafrika .


Eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo picha za video za sehemu ya Tamthiliya ya Dream Boat zimepigwa hapo.


Moja ya gari lililotumika katika tukio hilo likitoka eneoo la tukio kando ya Mto Mara unopita katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


Uchukuaji wa picha za video kando ya Mto Mara ukiendelea.


Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete akisaidia kubeba moja ya Kamera kubwa zilizokuwa zikitumika katika matukio ya uchukuaji wa picha katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


Moja ya Kamera kubwa iliyokuwa ikichukua matukio katika upigaji picha wa Tamthiliya ya Dream Boat katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


Mkurugenzi wa Utalii akiitizama Kamera ambayo ilikuwa iktumika kupiga picha za matukio mbalimbali wakati wa utengenezaji wa filamu hiyo.


Wataamu wakifunga Kamera katika ndge ndogo ya Shirika la ndege la Costal Airline kwa ajili ya upigaji wa picha za juu . 

HABARI KWA HISANI YA MTANDAO WA HABARI360


Thursday, December 1, 2016

KIMENUKA CCM MKOANI IRINGA,NI KUHUSU UUZAJI VIWANJA VYA UVCCM




CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Iringa kimeliibua upya suala la uuzaji wa baadhi ya viwanja vya Igumbilo vya mjini Iringa, mali ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), kikitaka viongozi watendaji wa chama wanaotuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo kusimamishwa uongozi.

Pamoja na kutaka viongozi hao kusimamishwa ili kupisha uchunguzi huru wa kashfa hiyo ya zaidi ya mwaka mmoja sasa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Dk Jesca Msambatavangu aliwataka waliouziwa viwanja hivyo kutoviendeleza mpaka mgogoro dhidi ya viwanja hivyo vinavyodaiwa kuuzwa kinyemela utakapokwisha.

Taarifa ya UVCCM iliyotolewa na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Abdukarim Alamga inaonesha UVCCM ilikuwa na shamba la zaidi ya heka 210 zilizopimwa ili kukidhi sheria za mipango miji na kupata viwanja zaidi ya 150.

Alamga alisema UVCCM ngazi ya Taifa inaendelea kulitafutia ufumbuzi kashya ya uuzaji wa baadhi ya viwanja hivyo na kwamba hivi karibuni Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shakha Mamdu Shaka alikuwepo mjini Iringa na kufanya majadiliano ya siri na baadhi ya watu waliouziwa.

Akizungumza na wanahabari katika viwanja hivyo Dk Msambatavangu alisema kumekuwepo na taarifa zinazomtaja Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga na Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa, Elisha Mwampashi kuhusika katika kashfa hiyo.

“Watendaji hao wanatajwa katika kashfa hii, na mimi kama msimamizi mkuu wa shughuli za chama mkoani hapa nitafuatilia suala la watendaji hao; ili wasivuruge uchunguzi wanatakiwa kusimamishwa kazi,” alisema.

Alimpongezea Rais Dk John Magufuli kwa kutumbua majipu na kuwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wanaotuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi na rushwa na akasema hatua kama hizo zinatakiwa kuchukuliwa pia ndani ya chama.

Alisema ataandika barua makao makuu ya chama hicho ili kuomba watendaji hao wasimashwe kazi mpaka mgogoro huu utakapokwisha na kama itabainika hawahusiki na tuhuma hiyo basi watarudishwa kazini kama taratibu zinavyotaka.

Wakati hayo yote yakiendelea, aliwaagiza wenyeviti wa UVCCM Manispaa ya Iringa na Iringa Vijijini kuhakikisha wanashirikisha vijana wao kulilinda eneo hilo mpaka pale mgogoro huo utakapokwisha.

“Naomba waliouziwa viwanja katika eneo hili wawe na subira. CCM ni chama cha haki na ni imani yangu katika hili kitatenda haki pia,” alisema.

Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Mtenga alikanusha kuhusika katika tuhuma hizo akisema UVCCM inaendeshwa kwa katiba yake ambayo yeye kama mtendaji wa chama hana mamlaka ya kuingilia.

“Katika nyaraka zote zinazohusiana na uuzaji wa viwanja hivyo, hakuna mahali ambapo mimi kama Mtenga natajwa kuhusika kwenye maamuzi yake, yawe yalifuata utaratibu au hayakufuatwa utaribu,” alisema.

Alisema moja ya hatua aliyochukua baada ya kusikika taarifa za uuzaji tata wa baadhi ya viwanja hivyo aliandikia barua katika ofisi ya Mkurugenzi ya Manispaa ya Iringa akiitaka isitoe hati za viwanja kwa watu waliouziwa kinyemela.

Alisema hakuna mali ya chama hicho inaweza kuuzwa pasipo kuridhiwa na Baraza la Wadhamini wa chama kwahiyo kama kuna mtu aliuziwa kinyume na utaratibu huo amtafute aliyemuuzia ili amdai fedha zake.

Mtenga alisema kwa kupitia msingi huo ndio maana kashafa hiyo ilipofikishwa kwenye vyombo vyo dola hakuwa mmoja wa waliofikishwa mahakamani kabla kesi hiyo haijafutwa.

Mei mwaka huu, Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa, Elisha Mwampashi na aliyekuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Alli Nyawenga walitiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani mjini Iringa wakituhumiwa kuhusika na uuzaji wa viwanja hivyo.

Baada ya wawili hao kukamatwa, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, John Kauga alizungumza na wanahabari na kusema kwamba viongozi walikamatwa baada ya kushitakiwa na Tume ya Uchunguzi ya Baraza la Wadhamini la UVCCM Taifa.

Alisema taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi hilo zilionesha watuhumiwa hao kuhusika na uuzaji wa viwanja hivyo kati ya Machi na Desemba mwaka jana.

Oktoba mwaka huu, kesi hiyo ilifutwa kwa kile kilichodaiwa kupisha uchunguzi zaidi wa kashfa hiyo iliyomuondoa madarakani Nyawenga huku Mwampashi akirudishwa kwa maelekezo ya chama kuendelea na majukumu yake ya ukatibu.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa inaonesha mapema wiki hii, Mwampashi amepata uhamisho unaompeleka mkoani Dodoma atakakokuwa Katibu wa CCM Manispaa ya Dodoma.

HABARI KWA HISANI YA BONGO LEAKS

SITA WAFA KATIKA AJALI MKOANI RUKWA,WALIKUWA WAKITOKEA NAMANYERE KWENDA SUMBAWANGA


Gari iliyopata ajali.


Gari iliyopata ajali.


Gari iliyopata ajali


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto) akipata maelezo ya kina ya majeruhi wa ajali akiwa na  Daktari Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa John Lawi 


Siti za Mbele kwa Dereva za gari hiyo


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen (katikati) Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mh. Said Mtanda kushoto pamoja na RTO Sadik Msangi wakiwa katika eneo la tukio la ajali


Katika tukio la jali

MBWANA SAMATTA AFUNGUKA KUWEKWA BENCHI



Wednesday, November 30, 2016

MRISHO NGASA ATUA RASMI MBEYA CITY


Picha inayo-trend kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ni ya Mrisho Ngasa na afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten ambayo inaashiria tayari nyota huyo wa zamani wa Yanga ameshakamilisha deal na ‘wagonga nyundo wa Mbeya’ Mbeya City.

Mwezi Septemba mwaka huu Ngasa alijiunga na Fanja FC inayoshiriki ligi kuu nchini Oman (Oman Professional League) ikiwa ni wiki tatu tu, baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Free State Stars ya South Africa.

Nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Kagera Sugar, Yanga, Azam FC na Simba vyote vya VPL hajadumu Oman na hatimaye amerejea tena nchini na kusajiliwa na klabu ya Mbeya City ambapo ataungana na kocha wake wa zamani Kinna Phiri aliyemsajili kutoka Yanga kwenda Free State Stars kabla ya kocha huyo kutimuliwa kufatia mfululizo wa matokeo mabovu.

Afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten ame-post picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa pamoja na Mrisho Ngasa na kuandika maneno yanosomeka: “Mnapokamilisha jambo kutakiana heri ndio uungwana.





POLISI SONGWE WAPEWA MSAADA WA PIKIPIKI

Chifu wa Usafirishaji na Lojistiki,Naibu Kamishina wa Polisi Shabani Mrai Hiki na Meneja mkuu wa kampuni ya Bima ya Maisha ya Sanlam nchini Wilson Mnzava wakikata utepe kama ishara ya kukabidhiana pikipiki nne zilizotolewa na kampuni hiyo kwaajili ya Jeshi la polisi mkoani Songwe.

 Meneja mkuu wa kampuni ya Bima ya Maisha ya Sanlam nchini Wilson Mnzava akizungumza jambo kabla ya kukabidhi pikipiki nne zenye thamani ya shilingi milioni 10.
 Kamanda wa Polisi mkoani Songwe Mathias Nyange akie;lezea uhaba wa vitendea kazi unaolikabili jeshi la polisi mkoani Songwe.
 Chifu wa Usafirishaji na Lojistiki,Naibu Kamishina wa Polisi Shabani Mrai Hiki na Meneja mkuu wa kampuni ya Bima ya Maisha ya Sanlam nchini Wilson Mnzava wakikabidhiana pikipiki nne zilizotolewa na kampuni hiyo kwaajili ya Jeshi la polisi mkoani Songwe.