Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, December 27, 2016

SERIKALI MKOANI SONGWE YATEKETEZA ZANA HARAMU ZA UVUVI


 Mkuu wa mkoa wa Songwe,Luteni mstaafu,Chiku Galawa akiteketeza kwa kuchoma moto zana haramu zilizokamatwa katika oparesheni maalumu iliyofanywa na Halmashauri wilayani Songwe



SERIKALI mkoani Songwe imeteketeza Zana haramu za uvuvi zeye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 zilizokamatwa ndani ya ziwa Rukwa upande wa wilaya ya Songwe.

Mkuu wa mkoa wa Songwe,Luteni mstaafu,Chiku Galawa aliteketeza kwa kuchoma moto zana hizo zikiwemo Nyavu aina ya kokoro zenye matundu madogo ambazo zimekuwa zikisababisha kuvuliwa kwa samaki wadogo na pia kuharibu mazalia ya samaki.

Akizungumza na wananchi mjini Mkwajuni wakati wa zoezi la kuteketeza zana hizo,Galawa alisema Serikali haiku tayari kuendelea kuona uvuvi haramu ukiendelea ndani ya Ziwa Rukwa.

Alisema Serikali inahitaji kuona uvuvi unakuwa endelevu ndani ya ziwa hilo hivyo lazima iwe na mipango madhudhuti itakayowezesha mazingira rafiki ya kuzaaliana na kukua kwa samaki.

“Tunatambua mchango wa shughuli za uvuvi katika kuchangia uchumi wa mtu mmoja mmoja na serikali.Lakini uvuvi tunahohitaji ni ulio endelevu na si huu wa kuharibu mpaka mazalia ya samaki”

“Tutazidi kupambana na watu wote wanaotumia uvuvi haramu.Na wao pia wanapaswa kutambua athari za uvuvi huu.Wajue kuwa wakiendelea ipo siku tutakosa kabisa samaki ndani ya ziwa letu” alisema Galawa.

Mkuu huyo wa mkoa pia aliitaka halmashauri kuweka mkazo katika kusimamia sharia ya kutoingiza mifugo kwenye eneo oevu la ziwa Rukwa ili kulinda maeneo hayo muhimu kwa ustawi wa ziwa hilo.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi walioshuhudia shughuli ya uteketezaji wa zana hizo,waliipongeza serikali kwa hatua hiyo na kuishauri kuongeza nguvu zaidi ili oparesheni iwe ya kudumu.

Walisema kutokana na uvuvi haramu sambamba na kemikali zinazotoka kwenye machimbo ya madini,kumekuwepo na kupungua kwa kiasi kikubwa samaki ndani ya ziwa hilo hatua inayoonesha mwenendo mbaya wa shughuli za uvuvi kwa siku za baadae.

No comments:

Post a Comment