Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, August 23, 2013

I LOVE MBEYA CITY

Mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Bw.Joachim Nyambo(Aliyevaa kofia) akiwa na wadau mbalimbali wa timu ya soka ya Mbeya City siku moja kabla ya kuanza kutimua vumbi kwa ligi kuu ya Tanzania bara ambayo timu hiyo ya jijini Mbeya inashiriki.Mchezo wa kwanza ndani ya Dimba la Sokoine jijini Mbeya Mbeya City itamenyana vikali na Kagera Sugar kutoka Bukoba.Lyamba Lya Mfipa inaitakia kila la Kheri Mbeya City.

MAANDALIZI MASHINDANO YA CHANETA TAIFA NDANI YA UWANJA WA SOKOINE JIONI HII

Mmoja wa viongozi wa timu ya Netiboli ya Jiji la Mbeya(Hamambe) akiwapa neno wachezaji wa timu hiyo kama walivyokutwa na Lyamba Lya Mfipa jioni hii ndani ya uwanja wa Sokoine ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya kitaifa ya mchezo huo yanayoanza kutimua vumbi jumamosi kwa michezo minne

Wednesday, August 21, 2013

MAANDALIZI YA LIGI KUU TANZANIA BARA NDANI YA UWANJA WA SOKOINE JIJINI MBEYA

Wachezaji wa timu ya soka ya Mbeya City wakiomba dua mara baada ya kumaliza mazoezi jioni hii ndani ya uwanja wa sokoine.Kwa mara ya kwanza timu hii itashiriki ligi kuu ya Tanzania bara itakayoanza kutimua vumbi jumamosi hii.SHUGHULI YA UPUNGUZAJI KIMO CHA NYASI NDANI YA UWANJA HUO LIKIENDELEA KAMA KIJANA HUYU ALIVYOKUTWA NA Lyamba Lya Mfipa JUZI.

MAANDALIZI YA MICHUANO YA CHANETA TAIFA ITAKAYOFANYIKA JIJINI MBEYA

MAFUNDI WAKIENDELEA NA UKARABATI WA KIWANJA CHA PILI KWAAJILI YA MICHUANO YA CHANETA ITAKAYOANZA KUTIMUA VUMBI SIKU YA JUMAMOSI LAKINI UZINDUZI RASMI NI JUMAPILI YA WIKI HII NDANI YA UWANJA WA SOKOINE JIJINI MBEYA.UWANJA MMOJA TAYARI UMEKAMILIKA KAMA UNAVYOONEKANA HAPA CHINIZIKIWA zimesalia siku chache kuanza kwa mashindano ya mchezo wa Netiboli taifa,maandalizi ya mashindano hayo yametajwa kuwa ya kususua kwa kiasi kikubwa. Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli(Chaneta) mkoani Mbeya Mary Mng’ong’o alithibitisha kusuasua kwa maandalizi hayo alipozungumza na Lyamba Lya Mfipa. Mng’ong’o amesema sababu ya kusuasua huko ni kukosekana kwa fedha kwaajili ya maandalizi hali aliyosema inatokana na wadau waliokuwa wakitegemewa kuchangia kutotimiza ahadi zao kwa wakati. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo hadi jana zilikiwa kimekusanywa kiasi cha fedha kisichofikia hata laki tano ilikhali kiasi cha fedha kinachohitajika ni zaidi ya shilingi milioni 16. Amesema wapo pia baadhi ya wadau ambao ni wajumbe wa kamati ya maandalizi walioahidi kuchangia kiasi cha fedha kwaajili ya kusaidia kufanikisha mashindabno lakini wao pia hawajachangia na kila wanapopigiwa simu wamekuwa wakieleza kutingwa na mambo yao binafsi. Aliwaomba wadau mbalimbali walioahidi kusaidia,kutimiza ahadi zao huku pia akisema serikali inapaswa kuliona suala la uandaaji mashindano kama hayo kwa namna nyingine itakayowapungumzia ugumu waandaaji wanaoelemewa na mzigo huo. Lyamba Lya Mfipa pia imefika katika viwanja vya mchezo huo vilivyopo ndani ya uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kuwakuta mafundi wakiendelea na ukarabati wa viwanja hivyo.

Monday, August 19, 2013

KANDORO MGENI RASMI MKUTANO WA JUMUIYA YA AHMADIYYA KESHO MBEYA

MKUU wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kesho(Agosti 20) anataraji kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya wenye lengo la kuzungumza mchango wa dini katika kuleta amani ya taifa na dunia kwa ujumla. Katika kikao chake na waandishi wa habari kiongozi mkuu wa Ahmadiyya nchini Tahir Mahmood Chaudhry amesema mkutano huo utakaoanza majira alasiri utafanyika katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. Chaudhry amesema Watendaji kadhaa wa serikali katika ngazi mbalimbali mkoani hapa pamoja na viongozi wa jumuiya za kidini na asasi zisizo za kiserikali wamealikwa kwenye mkutano huo na baadhi yao watapata nafasi ya kuchangia mada hiyo muhimu. Amesema jumuiya hiyo inauona mkutano wa aina hiyo kuwa muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linapita katika wakati mgumu wa mivutano baina ya wanadini wenyewe kwa wenyewe na wakati mwingine na serikali yao. Kiongozi huyo pia amelalamikia mapokeo yasiyo sahihi ya tafsiri za vitabu vitakatifu ikiwemo Kurani kwa baadhi ya wanadini hali aliyosema ni chanzo cha migogoro mingi inayoendelea duniani. Ametaja suala la baadhi ya waumini wa madhehebu ya kiislamu kutumia nguvu na vurugu wakidai ni njia sahihi na kupigania uislamu jambo alilosema si la kweli na kurani haifundishi hayo.

Thursday, August 15, 2013

MTANDAO WIZI WA BODA BODA WANASWA.WATUMIA SARE ZA JWTZ

MNAMO TAREHE 14.08.2013 MAJIRA YA SAA 16:50HRS HUKO AIRPORT - TANKINI JIJI NA MKOA WA MBEYA. DANIEL S/O SONGELA, MIAKA 24, KYUSA, DEREVA WA PIKIPIKI @ BODABODA, MKAZI WA ZZK-MBALIZI, ALINYANG’ANYWA PIKIPIKI YAKE T.691 CJF AINA YA KINGLION NA WATU WAWILI. MBINU NI KUKODIWA NA MTEJA MMOJA KWA UJIRA WA TSHS 5,000/= KUTOKA MBALIZI HADI ENEO LA ESSO NA NJIANI WALIKUTANA NA MTU MWINGINE ALIYEVAA SARE ZA JWTZ AKIWA AMESHIKA PANGA HIVYO WALIFANIKIWA KUMPORA MHANGA PIKIPIKI HIYO. KUFUATIA TUKIO HILO JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WAENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA LILIFANYA MSAKO NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WAWILI 1. BARAKA S/O DAUDI, MIAKA 20, KYUSA, BIASHARA MKAZI WA MAMA JOHN NA 2.SHADRACK S/O ESSAU, MIAKA 21, BIASHARA , MKAZI WA MWAMBENE WAMEKAMATWA NA KUKIRI KUHUSIKA KATIKA MATUKIO YA UPORAJI WA PIKIPIKI MAENEO MBALIMBALI. JUMLA YA PIKIPIKI NANE ZINAZODHANIWA KUWA MALI YA WIZI ZIMEKAMATWA KATIKA MSAKO HUKO TUKUYU WILAYA YA RUNGWE NA WATUHUMIWA SITA WAMEKAMATWA 1.SIMON S/O MWANYASI, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA 2.LWITIKO S/O HADSON, MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA 3. OSFA S/O MWAMAKULA, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA 4.FESTO S/O GIDEON, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA 5.SOFIA D/O GIDEON, MIAKA 35, KYUSA, MKULIMA NA 6.NOEL S/O YESAYA, MIAKA 34, KYUSA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA TUKUYU. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIPATIA KIPATO / MALI KWA NJIA YA MKATO KWA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJISHUGHULISHE NA SHUGHULI HALALI ZA KUJIPATIA KIPATO. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WALIOWAHI KUIBIWA AU KUPOTELEWA PIKIPIKI ZAO KUFIKA KITUO CHA POLISI KATI MBEYA KWA AJILI YA UTAMBUZI WA MALI ZAO.

Wednesday, August 14, 2013

NILIYOYAPENDA ZAIDI NANE NANE KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI NDANI YA UWANJA WA JOHN MWAKANGALE JIJINI MBEYA

AUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO NA MPENZI WAKE

MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA SAA 00:05 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANGA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. MARIA D/O MARTIN, MIAKA 37, MNYAMWEZI, MKULIMA, MKAZI WA KANGA ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI KICHWANI NA KUKABWA SHINGONI NA MPENZI WAKE AITWAE LAMECK S/O MSANGAWALE, MIAKA 35, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KANGA. CHANZO NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MTUHUMIWA KUMKUTA MAREHEMU AKIWA NA MWANAUME MWINGINE. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUYATATUA MATATIZO YAO YA KIJAMII KWA NJIA YA MEZA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA. PIA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

MAUAJI

MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA SAA 07:00 HRS UKO KIJIJI CHA NANSAMA KATA YA ISANSA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. SIJAONA S/O HAONGA MIAKA 45, MKULIMA, MNYIHA, MKAZI WA NANSAMA ALIKUTWA AKIWA AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA KUTUPWA KATIKA MTO MLOWO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI MGOGORO WA MASHAMBA KATI YA MAREHEMU NA SHABANI S/O MBWILI PAMOJA NA MAWAZO S/O MBWILI AMBAO WALITOROKA MARA BAADA YA TUKIO HILO. MAREHEMU ALIVIZIWA WAKATI AKIVUA SAMAKI NA PEMBENI YA MWILI WAKE KULIKUTWA NDOANO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOJICHULIA SHERIA MKONONI NA KUITATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO NA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.

Tuesday, August 13, 2013

WATATU WAFA KATIKA MATUKIO TOFAUTI

WATU watatu wamefariki dunia mkoani Mbeya, katika matukio mawili tofauti likiwemo la wachungaji wa mifugo kumuua mvuvi mmoja. Tukio la mauaji ya mvuvi, lilitokea juzi katika Kijiji cha Itindi wilayani Chunya. Mvuvi aliyeuawa alitajwa kwa jina la Hatibu Mwakalinga(36), ambaye aliuawa kwa kupigwa na fimbo mbavuni na wachunga Ng’ombe wafugaji wa kabila la kisukuma. Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa na kundi la Sungusungu wakikamata mifugo mali ya wafugaji waliofahamika kwa jina mojamoja la Mwanahela, Kabahungu na Lukangila. Tukio la pili lilitokea jana katika Kijiji cha Mshewe kata ya Utengule Usongwe wilaya ya Mbeya Vijijini, ambapo watoto wawili walikufa kwa ajali ya moto baada ya nyumba yao kuungua. Waliofariki dunia ni Desmos Raphael(2) na Dorcas Raphael mwenye umri wa miezi minne. Chanzo cha tukio hilo ni baada ya mama mzazi wa watoto hao Floiza Emmanuel(20), ambaye alikuwa amelala na watoto wake, kisha kutoka nje majira ya saa sita usiku kujisaidia na kuacha amewasha kibatari, na aliporudi akakuta nyumba yake inawaka moto. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio yote mawili na ametoa wito kwa wachunga mifugo waliosababisha kifo cha mvuvi wilayani Chunya kujisalimisha.

Sunday, August 11, 2013

AUA MKEWE KWA KUMNYONGA SHINGO.KISA WIVU WA MAPENZI

POLISI mkoani Meya inamshikila mkazi wa kijiji cha Mapogoro kata ya Miombweni wilayani Mbarali kwa tuhuma za mauaji ya mkewe kutokana na wivu wa mapenzi. Anayeshikiliwa na jeshi hilo amefahamika kwa jina la Nkuva Malale(39) ambapo inadaiwa kuwa alimuua mkewe kwa kumpiga fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo maeneo ya kichwani kabla ya kumnyonga shingo. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwan Athuman jana aliwaambia wandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea agosti 10 mwaka huu majira ya saa 10:30 kijijini Mapogoro. Kamanda Athuman alimtaja aliyeuawa katika tukio hilo la kinyama kuwa ni Mbuke Ochegeri(34) aliyekuwa mkulima na mkazi wa kijiji hicho. Alisema kabla ya kumshushia kipigo na kisha kumuua mtuhumiwa wa mauaji alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine. Aidha alisema uchughuzi zaidi juu ya mauaji hayo unaendelea na kubainisha kuwa wakati wowote mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

CRDB WALIPOPANDA MITI NA KUKARABATI JENGO LA WODI YA WANAWAKE KATIKA HOSPITALI YA META MBEYA

Waziri wa Uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe(Kushoto) akisaidiana na Mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB Dk.Charles Kimei kupanda mti kwenye eneo la hospitali ya Rufaa Mbeya tawi la Meta ambapo miti 200 ilipandwa na wafanyakazi pamoja na wadau wa benki hiyo.Katikati ni mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk.Norman Sigala.WANAHABARI NAO WALIKUWA MSTARI WA MBELE KUSHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI MITI KAMA ANAVYOONEKANA KENETH NGELESI MWENYE KOTI LA KAKI NA MWENZAKE GEORGE CHANDA ALIYEVALIA SUTI DK.Mwakyembe akipaka rangi kwenye moja ya kuta za wodi ya wazazi MetaMama Mwakyembe naye akishiriki kupaka rangi moja ya kuta za jengo la wodi ya wazazi katika hospitali ya Meta Mbeya

MBEYA CITY YATANGAZA JEZI MPYA ZA MASHABIKI

Hizi ndizo jezi zitakazoanza kuuzwa kwa mashabiki wa timu ya soka ya Mbeya City hivi karibuni.Kwa mara ya kwanza timu hiyo itashiriki ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu.

Friday, August 9, 2013

PSPF YAKUTANA NA WADAU MKOANI MBEYA

WADAU wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma(PSPF) mkoani Mbeya wameupongeza mfuko huo kwa kuanzisha mpango wa kukutana na wadau mbalimbali na kuwaongezea uelewa juu ya mifuko ya jamii. Wadau hao walitoa maoni yao kwenye warsha fupi iliyofanyika katika hoteli ya Hill View iliyopo jijini Mbeya ikiwakutanisha viongozi wa PSPF na wadau. Wadau hao walisema mfumo wa kukutana na wadau ni jambo muhimu kwakuwa itasaidia kupunguza malalamiko yanayotokana na uelewa mdogo walionao watumishi juu ya mifuko ya hifadhi za kijamii. Mmoja wa wadau hao afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Kateti Seleman,alisema mpango wa PSPF wa kukutana na wawakilishi wa watumishi unapaswa kuigwa na viongozi wa mifuko mingine. “Tumekuwa tukishuhudia kwa muda mrefu wenzenu wakikutana na wakurugenzi pekee.Wao wanaamini kwa kukutana na hao wanakuwa wamekamilisha mambo.Lakini si kweli.Wazo mlilokuja nalo hili la kukutana na watumishi na waajiri ni la msingi zaidi” alisema. Akizungumzia lengo la warsha hiyo mjumbe wa bodi ya PSPF Clement Mswanyana alisema mifuko ya hifadhi za jamiibado haijaeleweka kwa wananchi wengi nchini. “Wapo watumishi ambao wanakosa mafao yao kwa kukosa taarifa sahihi za mifuko.Ndiyo sababu tumeamua kuanzisha utaratibu huu wa kukutana na wadau ili kuongezeana uelewa.Wapo watumishi pia ambao wanapoingia kwenye ajira wamekuwa wakipewa taarifa potofu” alisema Mswanyana. Mswanyana pia alilalamikia uwepo wa waajiri hususani maafisa utumishi ambao wamekuwa wakiomba rushwa kutoka kwa maafisa mbalimbali wa mifuko ili waweze kuwaruhusu watumishi wao kujiunga na mifuko husika. Naye afisa msimamizi wa PSPF mkoani hapa Niteko Chaula alizungumzia fao la elimu,la ujasiriamali na fao la kujitoa kuwa huduma mpya ambazo zimeanzishwa na mfuko kwaajili ya kuboresha zaidi maisha ya watumishi. Akizungumzia mkopo wa nyumba,Chaula alisema mfuko huko baada ya kujenga katika mikoa mingi nchini unataraji kujenga mkoani Mbeya lakini akasisitiza kuwa ujenzi wa ofisi ni jambo litakalotangulia ili kuondokana na gharama za pango.