Tuesday, August 6, 2013
SUMAYE AZUNGUMZIA KATIBA MPYA
WAZIRI mkuu mstaafu Frederick Sumaye amesema tume ya katiba haipaswi
kuwa na msimamo wake kuhusu maoni yaliyotolewa na wananchi kwakuwa
imekwisha yaweka kwenye rasimu.
Badala yake ameitaka tume hiyo kuyaachia mabalaza ya katiba kujadili
rasimu hiyo kwakuwa kuendelea kuweka msimamo inamaanisha nayo ina
msimamo wake inaotaka upitishwe na mabalaza hayo.
Sumaye aliyasema hayo jana alipokuwa akifunga mkutano wa siku mbili wa
balaza la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu(Tahliso) uliofanyika
katika chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya likiwakutanisha na viongozi
mbalimbali wa serikali ya wanafunzi wa vyuo hivyo.
Alisema ili mradi kazi ya tume ilikuwa kuratibu maoni ya wananchi,basi
haipaswi pia kulaumiwa kwa maoni yaliyotolewa isipokuwa kama imetoa
rasimu isiyowakilisha maoni na wananchi walivyoyatoa.
“Wakati wakutoa maoni yao bila shaka wapo watanzania waliotaka
serikali moja,wapo waliotaka serikali mbili,waliotaka serikali
tatu,waliotaka serikali nne,labda wapo waliotaka serikali ya mkataba
na inawezekana labda wapo waliotaka tuachane na muungano”
“Kila mmoja aliyetoa maoni yake alikuwa na haki ya kufanya hivyo
kikatiba na sababu ya kutoa maoni yake hayo kama alivyotaka.Hivyo si
sahihi mtu au kundi la watu kukejeli au hata kutukana mtu au kundi
linguine lililotoa maoni yanayotofautiana na yake au kundi lake”
alisema
Aliwataka watanzania kujifunza ustahimilivu na kuheshimu maoni
aumawazo ya watu wengine na kama hawakubaliani nayo wayapinge kwa
nguvu ya hoja na si hoja ya nguvu.
Waziri mkuu huyo mstaafu alisema katika kufuatilia mchakato mzima wa
katiba mpya nchini amebaini mambo makubwa mawili aliyosema moja ni
baadhi ya watanzania kuamini matatizo yaliyopo ya hali ngumu ya maisha
na maendeleo duni ya jamii inatokana na katiba iliyopo hivi sasa
wanayodhani kuwa ni mbaya.
Alisema jambo la pili ni uwepo wa watu wenye fikra kuwa katiba mpya
utakuwa muarobaini wa matatizo yote mitazamo aliyosema yote si sahihi
na inaweza kupotosha taifa isipoelezwa vizuri.
Alisema kwa maoni yake hata katiba iliyopo ni nzuri na ndiyo maana
imewezesha kufikia umri wa karibu miaka 50 katika muungano watanzania
wakiwa salamaa na kuna mshikamano mzuri nchini.
Aliongeza kuwa kwa vyovyote katika miaka 50 kuna mabadiliko mengi
yametokea katika jamii hivyo katiba hiyo ingebidi tu kuhitaji
marekebisho kama ambavyo hata hiyo mpya itahitaji marekebisho baadaye
kutokana na mahitaji ya jamii.
Aidha Sumaye pia alisisitiza umuhimu wa watanzania kukumbuka kuilinda
katiba yao huku akisema mtu muhimu na wa kwanza kuilinda katika ya
nchi ni rais.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment