Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, August 13, 2013

WATATU WAFA KATIKA MATUKIO TOFAUTI

WATU watatu wamefariki dunia mkoani Mbeya, katika matukio mawili tofauti likiwemo la wachungaji wa mifugo kumuua mvuvi mmoja. Tukio la mauaji ya mvuvi, lilitokea juzi katika Kijiji cha Itindi wilayani Chunya. Mvuvi aliyeuawa alitajwa kwa jina la Hatibu Mwakalinga(36), ambaye aliuawa kwa kupigwa na fimbo mbavuni na wachunga Ng’ombe wafugaji wa kabila la kisukuma. Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa na kundi la Sungusungu wakikamata mifugo mali ya wafugaji waliofahamika kwa jina mojamoja la Mwanahela, Kabahungu na Lukangila. Tukio la pili lilitokea jana katika Kijiji cha Mshewe kata ya Utengule Usongwe wilaya ya Mbeya Vijijini, ambapo watoto wawili walikufa kwa ajali ya moto baada ya nyumba yao kuungua. Waliofariki dunia ni Desmos Raphael(2) na Dorcas Raphael mwenye umri wa miezi minne. Chanzo cha tukio hilo ni baada ya mama mzazi wa watoto hao Floiza Emmanuel(20), ambaye alikuwa amelala na watoto wake, kisha kutoka nje majira ya saa sita usiku kujisaidia na kuacha amewasha kibatari, na aliporudi akakuta nyumba yake inawaka moto. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio yote mawili na ametoa wito kwa wachunga mifugo waliosababisha kifo cha mvuvi wilayani Chunya kujisalimisha.

No comments:

Post a Comment