Wednesday, August 21, 2013
MAANDALIZI YA MICHUANO YA CHANETA TAIFA ITAKAYOFANYIKA JIJINI MBEYA
MAFUNDI WAKIENDELEA NA UKARABATI WA KIWANJA CHA PILI KWAAJILI YA MICHUANO YA CHANETA ITAKAYOANZA KUTIMUA VUMBI SIKU YA JUMAMOSI LAKINI UZINDUZI RASMI NI JUMAPILI YA WIKI HII NDANI YA UWANJA WA SOKOINE JIJINI MBEYA.UWANJA MMOJA TAYARI UMEKAMILIKA KAMA UNAVYOONEKANA HAPA CHINIZIKIWA zimesalia siku chache kuanza kwa mashindano ya mchezo wa
Netiboli taifa,maandalizi ya mashindano hayo yametajwa kuwa ya kususua
kwa kiasi kikubwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli(Chaneta) mkoani Mbeya Mary Mng’ong’o
alithibitisha kusuasua kwa maandalizi hayo alipozungumza na Lyamba Lya Mfipa.
Mng’ong’o amesema sababu ya kusuasua huko ni kukosekana kwa fedha
kwaajili ya maandalizi hali aliyosema inatokana na wadau waliokuwa
wakitegemewa kuchangia kutotimiza ahadi zao kwa wakati.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo hadi jana zilikiwa kimekusanywa kiasi
cha fedha kisichofikia hata laki tano ilikhali kiasi cha fedha
kinachohitajika ni zaidi ya shilingi milioni 16.
Amesema wapo pia baadhi ya wadau ambao ni wajumbe wa kamati ya
maandalizi walioahidi kuchangia kiasi cha fedha kwaajili ya kusaidia
kufanikisha mashindabno lakini wao pia hawajachangia na kila
wanapopigiwa simu wamekuwa wakieleza kutingwa na mambo yao binafsi.
Aliwaomba wadau mbalimbali walioahidi kusaidia,kutimiza ahadi zao huku
pia akisema serikali inapaswa kuliona suala la uandaaji mashindano
kama hayo kwa namna nyingine itakayowapungumzia ugumu waandaaji
wanaoelemewa na mzigo huo.
Lyamba Lya Mfipa pia imefika katika viwanja vya mchezo huo vilivyopo ndani
ya uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kuwakuta mafundi wakiendelea na
ukarabati wa viwanja hivyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment