Friday, August 9, 2013
PSPF YAKUTANA NA WADAU MKOANI MBEYA
WADAU wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma(PSPF) mkoani Mbeya
wameupongeza mfuko huo kwa kuanzisha mpango wa kukutana na wadau
mbalimbali na kuwaongezea uelewa juu ya mifuko ya jamii.
Wadau hao walitoa maoni yao kwenye warsha fupi iliyofanyika katika
hoteli ya Hill View iliyopo jijini Mbeya ikiwakutanisha viongozi wa
PSPF na wadau.
Wadau hao walisema mfumo wa kukutana na wadau ni jambo muhimu kwakuwa
itasaidia kupunguza malalamiko yanayotokana na uelewa mdogo walionao
watumishi juu ya mifuko ya hifadhi za kijamii.
Mmoja wa wadau hao afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya
Kateti Seleman,alisema mpango wa PSPF wa kukutana na wawakilishi wa
watumishi unapaswa kuigwa na viongozi wa mifuko mingine.
“Tumekuwa tukishuhudia kwa muda mrefu wenzenu wakikutana na
wakurugenzi pekee.Wao wanaamini kwa kukutana na hao wanakuwa
wamekamilisha mambo.Lakini si kweli.Wazo mlilokuja nalo hili la
kukutana na watumishi na waajiri ni la msingi zaidi” alisema.
Akizungumzia lengo la warsha hiyo mjumbe wa bodi ya PSPF Clement
Mswanyana alisema mifuko ya hifadhi za jamiibado haijaeleweka kwa
wananchi wengi nchini.
“Wapo watumishi ambao wanakosa mafao yao kwa kukosa taarifa sahihi za
mifuko.Ndiyo sababu tumeamua kuanzisha utaratibu huu wa kukutana na
wadau ili kuongezeana uelewa.Wapo watumishi pia ambao wanapoingia
kwenye ajira wamekuwa wakipewa taarifa potofu” alisema Mswanyana.
Mswanyana pia alilalamikia uwepo wa waajiri hususani maafisa utumishi
ambao wamekuwa wakiomba rushwa kutoka kwa maafisa mbalimbali wa mifuko
ili waweze kuwaruhusu watumishi wao kujiunga na mifuko husika.
Naye afisa msimamizi wa PSPF mkoani hapa Niteko Chaula alizungumzia
fao la elimu,la ujasiriamali na fao la kujitoa kuwa huduma mpya ambazo
zimeanzishwa na mfuko kwaajili ya kuboresha zaidi maisha ya watumishi.
Akizungumzia mkopo wa nyumba,Chaula alisema mfuko huko baada ya
kujenga katika mikoa mingi nchini unataraji kujenga mkoani Mbeya
lakini akasisitiza kuwa ujenzi wa ofisi ni jambo litakalotangulia ili
kuondokana na gharama za pango.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment