Friday, August 2, 2013
MADIWANI NA WAKUU WA IDARA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA WATIMULIWA KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA LAAC
KAMATI ya bunge ya hesabu za (LAAC) jana ililazimika kuwatimua kwa
muda madiwani na wakuu wa idaya za halmashauri ya jiji la Mbeya kwenye
kikao cha kupitia taarifa za matumizi ya fedha za umma kwenye
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kamati ililazimika kuwaondoa kwenye kikao watu hao kufuatia kuwepo kwa
mkanganyiko wa maelezo kwenye vitabu vya taarifa za matumizi hayo
ambapo vitabu vya wajumbe wa kamati vilikuwa na maelezo sawa na vile
vya maofisa kutoka ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali(CAG) lakini
vikatofautiana na vitabu walivyokuwa nanvyo wakuu wa idara.
Hoja ya matumizi ya kiasi cha shilingi milioni 104 kwaajili ya
ukarabati wa mabweni ya Kawawa na Sokoine kwenye shule ya sekondari ya
Iyunga iliyopo jijini hapa ndiyo iliyozua mgogoro na kukatisha kikao
kwa muda.
Taarifa za CAG zilionesha zilionesha kuwa hadi ukaguzi unafanyika
bweni moja lilikuwa limekarabatiwa lakini fedha zote zilionekana
kutotumika bado huku pia kukiwa hakuna mkataba uliowekwa kati ya
halmashauri na mkandarasi aliyepewa kazi hiyo na muda wa mkataba
haukujulikana.
Katika harakati za kuijibu hoja hizo ndipo wakuu wa idara akiwemo
mweka hazina James Jorojike na madiwani wakiongozwa na meya Athanas
Kapunga walipoanza kujichanganya kwa kutoa majibu yanayokinzana hali
iliyosababi mwenyekiti wa Laac Rajab Mohamed kuahirisha kwa muda kikao
na kuomba madiwani na wakuu wa idara watoke nje ya ukumbu kuanzia saa
7:40 hadi saa 8:9 mchana.
“Tuna takriban hoja 25,bado tupo kwenye hoja moja ambayo tumeshindwa
kukubaliana.Taarifa mliyompa ninyi wenyewe CAG inaonesha bweni moja
limekarabatiwa lakini fedha zote zipo.Tunataka kujua fedha mlizotumia
mlitoa wapi.Ninyi manasema mabweni yote yamekarabatiwa na fedha
zimetumika.Naomba tubaki wabunge tujadiliane tuone nini kifanyike”
alisema Mohamed kabla ya kuwatoa nje madiwani na wakuu wa idara.
Hata hivyo baada ya kurejea ukumbini,mwenyekiti huyo alisema wabunge
walikubaliana kutoa maagizo siku ya maazimisho ya ziara yote kwa mkoa
wa Mbeya itakayofanyika Agosti 3 mwaka huu katika ofisi ya mkoa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment