Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, December 29, 2012

POLISI YAONYA VIONGOZI WA DINI,WANASIASA

VIONGOZI wa madhehebu ya kidini na vyama vya siasa mkoani Mbeya wameombwa kuwaonya waumini wao kutojihusisha na vitendo vyovyote vya vitakavyosababisha uvunjifu wa awami katika kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Diwani Athumani amesema kwa mamlaka waliyo nayo viongozi hao wanayo nguvu ya kuwaonya wafuasi wao kusherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu. Alitoa pia wito kwa wananchi wote kuepuka ushawishi wa wa watu wachache wa kujihusisha na vitendo vya uvunjaji wa amani na utulivu akisema jeshi hilo halitosita kuwachukulia hatua za kisheria watakaobainika. “Tunatambua katika kusherehekea sikukuu hiyo wapo baadhi ya watu ambao huitumia vibaya.Jeshi la polisi tumejipanga kukabiliana na watu wote watakaoonesha nia ya kufanya vitendo hivyo” alisema. “Vitendo kama vurugu za kisiasa, mifarakano ya kidini, kujichukulia sheria mkononi, kuchoma matairi kwenye barabara havikubaliki na hatutavumilia.Ni kinyume na utaratibu wa sheria na ni kuisababishia serikali hasara kubwa kwani barabara hizo zimejengwa kwa mamilioni ya kodi za watanzania” Kamanda huyo pia aliwaonya watumiaji wa barabara hususani wanaoendesha vyombo vya moto kuwa makini kwa kufuata sheria za usalama barabarani, kuacha kunywa wakati wanaendesha na kuwa vyanzo vya ajali barabarani na kuwasababishia watu wengine ulemavu ama kupoteza maisha. Kwa upande wao wazazi aliwataka kuwa makini na watoto wao na kuona uwezekano wa kutokwenda nao kwenye kumbi za starehe, kutoacha nyumba zao bila waangalizi, watoto kutembea barabarani bila usimamizi wao. Alisisitiza kila mmoja kuchukua tahadhari katika kipindi hiki kwani wahalifu wanaweza kutumia udhaifu wao kukamilisha azima yao ya kuwavunjia nyumba zao na kuiba ama maeneo yao ya kibiashara kutokana na kukosekana ulinzi. Aliwaomba wananchi wote kutoficha wahalifu bali watumie uzalendo wao kuwafichua wahalifu hao kwa kutoa taarifa katika vituo vya polisi vilivyokaribu na maeneo yao kwa usalama wa mali zao na za wengine na kwamba iwapo kuna uwezekano taarifa hizo za kiuhalifu / wahalifu zitolewe kabla ya kutokea.

Thursday, December 27, 2012

MWAKA UNAKWISHA JIULIZE UMEFANYA MANGAPI NA JE UMEFIKIA MALENGO ULIYOJIWEKEA?TAFAKARI CHUKUA HATUA KWA MWAKA 2013.

Sunday, December 23, 2012

HATARIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKONAI IRINGA WAKIFANYIA SHUGHULI ZAO NDANI YA GARI LA MTU BINAFSI BADALA YA JENGO MAALAUMU LILILOJENGWA KWA KAZI HIYO LINALOONEKANA PEMBENI KATIKA KITUO CHA UKAGUZI MAGARI CHA MAKAMBAKO MKOANI IRINGA.HATUA YA ASKARI KUTUMIA GARI ZAO BINAFSI KUFANYIA SHUGHULI KAMA HIZO KUNATAJWA KUWA CHANZO CHA KUOMBA RUSHWA KUTOKA KWA MADEREVA NA MAKONDAKTA AMBAPO ASKARI WAMEKUWA WAKIDAIWA KUOMBA MCHANGO WA MAFUTA WA GARI ZAO HIZO

ZIARA YA Lyamba Lya Mfipa MPONDA KATA YA MAJENGO MANISPAA YA SUMBAWANGA MKOANI RUKWA

Friday, December 21, 2012

HATARIIIIIIIIII

WAFANYABIASHARA WAKIUZA NYANYA,MATUNDA MENGINE NA VYAKULA AINA MBALIMBALI JIRANI NA ENEO LA KUCHIMBA DAWA ABIRIA LA MAKAMBAKO MKOANI IRINGA

CCM KUMWAJIBISHA DIWANI WAKE

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WILAYANI MBARALI KIMESEMA KITAFUATILIA KWA MAKINI TUHUMA ZINAZOMKABILI DIWANI WA KATA YA LUHANGA BARAKA LWETEYOO MAMBOLEO NA IWAPO ATABAINIKA KUWA NI ZA KWELI ATAWAJIBISHWA KWA MUJIBU WA KATIBA YA CHAMA HICHO. TUHUMA ZINAZOMKABILI DIWANI HUYO NI PAMOJA NA KUWAGAWA WANANCHI KATIKA MAKUNDI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI HALI INAYOCHOCHEA MIGOGORO BAINA YA PANDE HIZO PAMOJA NA KUKWAMISHA SHUGHULI ZA UWEKEZAJI KWENYE KILIMO.

SHUGHULI YA USAGAJI KOKOTO IKIENDELEA KATIKA ENEO LA UYOLE JIJINI MBEYA

HATARIIIIIIIIIIIII

MTOTO AMBAYE JINA LAKE HALIKUFAHAMIKA MARA MOJA AKICHEZEA MAJI MACHAFU WAKATI MAMA YAKE AKIWA KATIKA FOLENI YA MAJI YA KISIMA KIREFU KATIKA KIJIJI CHA LUHANGA WILAYANI MBARALI

Wednesday, December 19, 2012

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 19/12/2012. WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO MNAMO TAREHE 18.12.2012 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO MBALIZI TARAFANI BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU DENIS S/O FRANK,MIAKA 23,MKINGA,BIASHARA MKAZI WA MBALIZI, NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO . CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO. JITIHADA ZINAENDELEA KUMTAFUTA MTUHUMIWA NA GARI KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI NA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WANYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO DEREVA HUYO AZITOE ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE. WILAYA YA MBOZI - KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] MNAMO TAREHE 18.12.2012 MAJIRA YA SAA 15:30HRS HUKO KIJIJI CHA ICHENJEZYA WILAYA MBOZI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1.VISCUS S/O SICHOLE, MIAKA 40, MNYIHA, MKULIMA 2.ELINA D/O MBAGULE, MIAKA 60, MNDALI, MKULIMA 3. HURUMA D/O KAYUNI,MIAKA 30,MNDALI MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ICHENJEZYA WAKIWA WANAKUNYWA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA 4 .WATUHUMIWA NI WANYWAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI KOSA LA JINAI, PIA NI HATARI KWA AFYA YA MNYWAJI. WILAYA YA CHUNYA KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] MNAMO TAREHE 18.12.2012 MAJIRA YA SAA 18:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KIGAMBONI KIJIJI CHA MKWAJUNI WILAYA CHUNYA MKOA WA MBEYA . ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA ABDALAHA S/O NDEGE ,MIAKA 70,MSONGWE,MKULIMA MKAZI WA KIGAMBONI-MKWAJUNI AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA 5 . MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO .TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI KOSA LA JINAI PIA NI HATARI KWA AFYA YA MNYWAJI. Signed By [ JACKOB KIANGO - SP ] Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Friday, December 14, 2012

WANAFUNZI WAOKOTA BASTOLA

WILAYA YA CHUNYA - TAARIFA KUOKOTWA KWA SILAHA [BASTOLA]. MNAMO TAREHE 12.12.2012 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IFUMBO WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. WATOTO WADOGO WALIOKUWA WAKICHEZA MPIRA WA MIGUU KATIKA UWANJA WA S/MSINGI IFUMBO WALIOKOTA BASTOLA MOJA ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI INAYOTUMIA RISASI ZA S/GUN IKIWA NA RISASI MOJA YA S/GUN . MBINU NI KUHIFADHI SILAHA HIYO KATIKA MFUKO WA RAMBO NA KUIWEKA KANDO YA UWANJA HUO . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOMILIKI SILAHA BILA YA KIBALI KWANI NI KOSA LA JINAI. AIDHA ANATOA RAI KWA WAZAZI/WALEZI KUWAELIMISHA WATOTO KUACHA TABIA YA KUOKOTA NA KUCHEZEA VITU AMBAVYO HAWAVIFAHAMU KWANI VINGINE VINAWEZA KUWA NI VITU VYA HATARI/MILIPUKO NA BADALA YAKE WATOE TAARIFA KWA WAZAZI/WALEZI AU MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA HARAKA ZICHUKULIWE KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA. KAMANDA PIA ANARUDIA KUTOA WITO KUWA KIPINDI HIKI NI CHA ‘”OFFER “ YA KUSALIMISHA SILAHA BILA KUCHUKULIWA HATUA NA KINAMALIZIKA TAREHE 05.01.2013. ANATAHADHARISHA USALIMISHAJI UYALENGE MAENEO YALIYOSALAMA ZAIDI TOFAUTI NA ILIVYO KUWA KWA SILAHA HII KWA KUWA SILAHA INAWEZA KUANGUKIA KWA WATU WASIOWEMA. WILAYA YA CHUNYA - TAARIFA YA KUPATIKANA KWA RISASI ZA SMG MNAMO TAREHE 12.12.2012 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA HIFADHI YA LUKWATI ILIYOPO KATIKA KIJIJI CHA BITIMANYANGA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA . DAIMON S/O JOHN, MIAKA 32, MNYAMWEZI, ASKARI MGAMBO MKAZI WA BITIMANYAGA AKIWA KWENYE DORIA YA KUDHIBITI MAJANGIRI KATIKA PORI HILO NA ASKARI MGAMBO WENZAKE WAWILI WALIMUONA MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE JINSIA MWANAUME AMBAYE ALIWAKIMBIA NA KUTOKOMEA PORINI BAADA YA KUTUPA KIFURUSHI KIMOJA AMBACHO NDANI YAKE KULIKUTWA RISASI 114 ZA SMG, NGUO NA REDIO MOJA NDOGO AINA YA AITKENSON AMBAYO JUU IMEANDIKWA JINA LA MBOGE. MBINU NI KUKIMBIA NA KUTELEKEZA KIFURUSHI HICHO BAADA YA KUWAONA ASKARI MGAMBO HAO. MTUHUMIWA ANADHANIWA KUWA NI MUWINDAJI HARAMU. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOMILIKI SILAHA BILA YA KIBALI KWANI NI KOSA LA JINAI. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA ALIKOJIFICHA MTUHUMIWA HUYO AZITOE KWA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE. Signed By, [ DIWANI ATHUMANI – ACP ] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Wednesday, December 12, 2012

CHADEMA WAKANA KUMJUA EDO MWAMALALA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) wilayani Mbeya kimekana kumtambua aliyewahi kuwa katibu wa chama hicho mkoa Edo Mwamalala kikisema kilikwishja mtimua miezi mitatu iliyopita hivyo matamko anayoyatoa kupitia vyeo anavyojipa si ya cha hicho. Uongozi wa chama hicho umeyasema hayo katika kikao chake na waandishi wa habari na kubainisha kuwa Mwaalala alikwisha timuliwa uanachama baada ya kamati tendaji ya chama wilaya kujiridhisha kuwa hakisaidii chama bali ni miongoni mwa watu wanaokisaliti. Hata hivyo kauli ya kutanganzwa kufutiwa uanachama imekuja baada ya Mwamalala kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akithibitisha katibu mkuu wa Chadema dk.Wilbrod Slaa kuendelea kuwa na kadi mbili za vyama vya siasa ikiwemo ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kauli ambayo imekuwa ikiwaumiza wanachadema kila inapotamkwa. Mwenyekiti wa Chadema Mbeya mjini David Mwambigija alisema jana kuwa japo ilikuwa haijatangazwa kwenye vyombo vya habari,Makata alienguliwa katika chama hicho muda mrefu kwa mujibu wa katiba ya chama hicho sura ya kumi kifungu cha tisa,kumi na kumi na moja. “Tulikwisha mfutia uanachama hivyo aliyetoa taarifa kwenye vyombo vya habari majuzi ni mhuni wa mtaani tu.si katibu wa chama wala mjumbe wa mkutano mkuu kama alivyojiita.Hayupo tena Chadema ndiyo maana kwa sasa utamuona jirani sana na Thomas Nyembo wa chama kipya cha NDC” “Tulimgundua hakuwa mtu mwema kwa chama chetu bali mamluki.Mwamalala aliwahi kukutwa yuko na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa chadema Sambwee Shitambala baadae akahamia CCM wakiwa wanataka kwenda Dodoma kuonana na Nape bahati mbaya wakakutana na Sugu ndipo kwa aibu akaamua kuahirisha hiyo safari” alisema Mwambigija. Alilalamikia kauli ya dk.Slaa kutajwa kuwa na kadi ya CCM akisema hakuna katiba inayosema lazima mwanachama anapokihama chama flani arejeshe kadi kwa chama anachokihama au akikabidhi chama anachohamia japokuwa ni mtindo ambao Chadema wamekuwa wakiutumia siku zote kunyang’anya kadi za wanachama wanaohamia kutoka vyama vingine. Alimtaja Mwamalala sawa na mbwa anayebweka baada ya kutimuliwa kwenye lindo ambako walau alikuwa akisukuma maisha klwa kuokota mifupa ndiyo maana haishi kutapatapa. Alisema kwa mujibu wa katiba ya chama chao hairuhusiwi mwanachama wa kawaida kumjadili kiongozi wa ngazi ya kitaifa nje ya vikao vya chama na kufanya hivyo ni makosa na angekuwa ni mwanachama wangeweza kumwajibisha

Tuesday, December 11, 2012

ASKARI MAGEREZA AUAWA NA MWILI KUCHOMWA MOTO

WATU wawili akiwemo Askari Magereza wa gereza la Luanda jijini Mbeya wameuawa kwa kupigwa na kuchomwa moto na wananchi wakidhaniwa kuwa wezi wa pikipiki. Askari aliyeuawa ametambulika kwa jina la Abel Mwakajinga(24) aliyekuwa likizo na nduguye Ezekiah Gambi(30)mkazi wa Chizumbi Wilayani Mbozi ambapo wameuawa walipokwenda katika kijiji cha Ukwile kata ya mlangali Wilaya ya hapa kwa lengo la kumkamata mtuhumiwa wa mauji ya ndugu yao. Mwenyekiti wa kijiji cha Ukwile Osiah Mtawa amesema tukio hilo limetokea Desemba 8, mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni katika kijiji hicho ambapo marehemu hao wakiwa wanandugu walifika kijijini hapo kwa njia ya pikipiki ya kukodi(Bodaboda) wakilenga kumkamata Laiton Nganya anayetuhumiwa kwa mauaji ya ndugu yao Salum Gambi aliyeuawa Novemba 14, mwaka huu. Baada ya kufika katika kijiji hicho askari magereza alishuka na kwenda moja kwa moja kumkamata mtuhumiwa lakini kabla ya kutimiza malengo yake mtuhumiwa huyo alipiga yowe kuomba msaada wa wanakijiji akisema amevamiwa na wezi wa pikipiki na ndipo wananchi wakaanza kuwashambulia kwa kuwachoma na vitu vyenye ncha kali na hatimaye kuwachoma moto hadi kufa. Mdogo wa marehemu Ezekiah Gambi aliyejitambulisha kwa jina la Godfrey Gambi(26) amesema ndugu zake walikwenda katika kijiji hicho kwa lengo la kumkamata mtuhumiwa wa mauji ya ndugu yao baada ya kupata taarifa ya uwepo wake kijijini hapo lakini hakamatwi na polisi. Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athuman alikiri kuwa na taarifa za tukio hilo na kusema tayari watuhumiwa wa mauaji hayo wametambuliwa na utaratibu unafanyika ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Monday, December 10, 2012

CHADEMA WADAIWA KUVUNJA MASANDUKU YA KURA NA KUIBA FEDHA ZA UCHAGUZI

WATU 13 akiwemo diwani wa viti maalumu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kata ya saza Benadetha Zacharia(38) wanashikiliwa na jershi la polisi kwa kufanya vurugu zilizosababisha uharibifu wa mali ya umma yakiwemo masanduku ya kupigia kura.
Wengine ni katibu wa Chadema kata ya Saza wilayani Chunya Braison Mwasimba(34),John Mponzayo(52),Seleman Tanganyika(24),Ambokile Francis(23),Amos Joseph(24),Abdul Mwandeule(20),Christopher Mwanjayo(37), Baraka Saul(19),Musa Mnyonga(32),Essa Pius(18),Marco Gibson(25) wote wakazi wa kata ya Saza na Paradiso Emanuel(26) mkazi wa kijiji cha Njenjele wilayani Mbeya. Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athuman alisema kuwa mnamo desemba 8 mwaka huu majira ya saa 11:15 katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya Saza baadhi ya wananchi wakiongozwa na watuhumiwa waliamua kujichukulia sheria mikononi na kusababisha uharibifu wa mali za umma. Kamanda Athuman alitaja uharibifu uliofanyika kuwa ni kuvunjwa kwa kioo cha mbele cha gari yenye namba SM 3830 Toyota Landcruiser mali ya halmashauri ya wilaya ya Chunya,kuvunja mlango na dirisha la ofisi ya afisa mtendaji kata. Alisema hbaada ya uharibifu huyo watuhumiwa waliingia ndani ya ofisi hiyo na kuharibu masanduku 24 ya kupigia kura ambapo thamani ya mali zote bado haujafahamika. Alisema chanzo cha vurugu hizo ilikuwa kushinikiza kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya mwenyekiti wa kijiji na vitongoji uliokuwa ufanyike siku ya jumapili. Kufuatia vurugu hizo uchaguzi huo ililazimu kusogezwa mbele siku moja na kufanyika jana(Disemba 10) huktaratibu za kisheria zikiendelea ikiwemo kufikishwa jana mahakamani katioka mahakama ya wilaya ya Chumnuya watuhumiwa 12 na kusomewa mashitaka. Ukiachilia mbali shitaka la uharibifu wa mali za umma linalowakabili washitakiwa wote mahakamani hapo washitakiwa Amos Joseph,Braison Mwasimba na Paradiso Emanuel wanakabiliwa na shitaka jingine la unyang’anyi. Alisema washitakiwa hao walifanya unyang’anyi wa fedha kiasi cha shilingi 2,150,000 zilizokuwa sehemu ya gharama za uchaguzi,simu ya kiganjani na saa ya mkononi.

Sunday, December 9, 2012

TUNAWATAKIA JUMAPILI NJEMA WASOMAJI WETU WOTE POPOTE MLIPO NDANI NA NJE YA TANZANIA

Thursday, December 6, 2012

BUNDUKI MBILI ZAKAMATWA MBARALI


SIKU chache baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Emmanuel Nchimbi kutangaza ongezeko la vitendo vya uharifu ikiwemo mauaji ya kutumia silaha na kutoa onyo kwa watanzania wanaomiliki silaha kiholela kuzisalimisha ndani ya siku 30 watu wawili wanashikiliwa na polisi mkoani Mbeya kwa umiliki wa aina hiyo wa silaha.

Miongoni mwa wanaoshikiliwa ambao wote walikamatwa na askari wanyamapori ni pamoja na mwanamke Esther Msigwa(30) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Madibira wilayani Mbarali.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Adam Simfukwe amesema Esther amekamatwa Desemba 5 mwaka huu saa saba mchana na askari wanyamapori waliokuwa doria na kwakuwa mtuhumiwa amekuwa akijihusisha na uwindaji haramu ndipo waliamua kufanya msako nyumbani kwake na kukuta bunduki moja aina ya Gobole aliyokuwa ameificha chumbani kwake.

Katika msako huo pia askari hao wa TANAPA wamemkamata Badede Chafumbo(49) mkazi wa kijiji hicho baada ya kukuta anamiliki gobore moja goroli 41 ambazo hutumika kama risasi na chupa mbili za baruti.

Simfukwe amesema silaha hizo zote zimekuwa zikitumiwa na mtuhumiwa kwa uwindaji haramu katika hifadhi ya Ruaha iliyopo jirani na kijiji cha Madibira jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

WAHAMIAJI HARAMU

WAHAMIAJI haramu 28 wote raia wa Ethiopia wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa kuingia nchini kinyume cha sheria.

Kadhalika jeshi hilo linamshikilia dreva taxi aliyefahamika kwa jina la Christopher Alfred(39) mkazi wa Veta jijini Mbeya kutokana na wahamiaji hao haramu kukutwa katika pagala la nyumba yake anayoendelea kuijenga.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Adam Simfukwe amesema kuwa wahabeshi hao wamekamatwa na askari waliokuwa doria desemba 5 mwaka huu majira ya saa  4:00 usiku katika eneo la Veta jijini Mbeya.

Simfukwe amesema watuhumiwa wakiongozwa na mwenzao aliyefahamika kwa jina la Mohamed Kabebe(27) walikuwa wamejificha ndani ya pagala hilo lakini haikufahamika mara moja waliingia jijini hapa wakitokea wapi na ni wapi wanakoelekea.

Amesema taratibu za kisheria zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kuwakabidhi wahamiaji hao kwa Idara ya Uhamiaji ili iendelee na mchakato mwingine wa kisheria dhidi yao.

Wednesday, December 5, 2012

VIJANA MBALIZI WAJITOLEA KUSAFISHA MIFEREJI ILIYOJAA UDONGO

 Ni kwa kujitolea kama ilivyokuwa enzi za baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere vijana hawa wa mji mdogo wa Mbalizi wilayani Mbeya wakiwemo wanawake leo hii wameamua kufanya usafi wa mji huo kwa kusafisha mitaro ya maji katika barabara zilizopo jirani na kituo cha mabasi.
 Ni vijana wachache lakini wsalioonekana kuwa na ari ya kutoa somo kwa wenzao kuwa si kila jambo wasubiri serikali ikawafanyie.Waanze wao watakapoishia ndipo serikali kupitia halmashauri iende kusaidia
 Mbunge wa jimbo la Mbeya(Kulia) mchungaji Luckson Mwanjala akavutiwa na kazi ya vijana hao alipopata taarifa na kuamua kufika eneo la tukio kujionea
 Mwanjala akavutiwa na kazi ya vijana hao na kuamua kutoa shilingi 150,000 zisaidia kununua vinywaji baridi wakati vijana wakiendelea na shughuli hiyo

 Mbunge akaondoka na kuacha vijana wakiendelea na kazi hiyo ikiwa ni siku ya kwanza ambapo kesho wataendelea.Lakini ni kazi ambayo vijana hawa wanasema haihusishi hata kidogo itikadi za kisiasa bali maendeleo ya eneo lao.
 Kuna wakati ililazimu nguvu ya ziada itumike ili kurahisisha usafishaji wa mitaro iliyoziba.Hapa ni daraja dogo ambalo lazima lizibuliwe lakini ili kufanya hivyo lazima pia kuondoakaravati za zege na saruji.

Mratibu wa shughuli ya kujitolea kwa vijana hao Godorn Kalulunga hakuwa nyuma kuonyesha mfani kwa kufanya kazi kama anavyoonekana katika picha hii juu.
Baada ya kazi ya siku ya kwanza ikawalazimu vijana kukaa kujadiliana nini kitafanyika kesho alhamisi

Tuesday, December 4, 2012

OFISI ya Katibu Tawala mkoani Rukwa imefikishwa katika mahakama kuu ya
kazi kanda ya nyanda za juu kusini iliyopo jijini Mbeya kwa kukiuka
makubaliano ya kumlipa mtumishi madai ya malipo ya uhamisho
yaliyowekwa chini ya Tume ya usuluhishi na maamuzi.

Mnamo Juni 7 mwaka huu tume hiyo ilisuluhisha mgogoro wa madai kati ya
Dereva Revocatus Nkonje na ofisi ya katibu tawala mkoa wa Rukwa kwa
makubaliano ya ofisi hiyo kumlipa mtumishi huyo kwa awamu jumla ya
shilingi 14,000,000.

Kiasi hicho cha fedha kilipunguzwa kutoka shilingi 60884,000 alizokuwa
akidai mtumishi ikiwa ni gharama za uhamisho baada ya mlalamikaji
kuridhia ombi la mdaiwa na ndipo makubaliano yakawa fedha hizo zilipwe
kwa awamu shilingi 2500,000 kila mwezi na muda wa ukomo ikapangwa iwe
desemba mwaka huu.

Kinyume na makubaliano yaliyofikiwa ofisi hiyo ilikaidi kwa kutomlipa
dereva huyo hali iliyopelekea kuchukua maamuzi ya kupeleka shitaka
hilo katika mahakama kuu ya Kazi iliyopo jijini Mbeya ili kuomba
kukazia hukumu.

Awali shitaka hilo ilikuwa lianze kusikilizwa novemba 28 mwaka huu
lakini limesogezwa mbele hadi desemba 3 mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili jijini Mbeya mara baada ya kuahirishwa kwa
shitaka lake Nkonje alisema baada ya kufikisha shitaka hilo mahakamani
hapo hali ya utumishi wake imekuwa katika misukosuko na manyanyaso
makubwa toka kwa mwajiri.

Alisema ni zaidi ya mwezi mmoja umepita tangu azuiliwe kuendesha gari
ya idara ya afya katika hospitali ya mkoa wa Rukwa aliyokuwa
akiendesha siku zote na pia amezuiwa kuendesha gari nyingine yoyote
bali kila siku afike ofisini kwake na kuripoti.

Alisema alipohoji sababu ya kuzuiwa aliambiwa ni kwakuwa amempeleka
katibu tawala katika mahakama kuu ya kazi hivyo jambo ambalo
halijampendeza na kuamua kutoa adhabu hiyo.

Kwa mujibu wa Nkonje madai yake ni ya uhamisho wa muda uliofanyika
Agosti 14 mwaka 2009 alipotolewa wilayani Mpanda kwenda ofisi za mkoa
wa Rukwa ambapo madai halisi yalikuwa shulingi 60884000 lakini mpaka
leo hajalipwa hata shilingi moja licha ya kukubali kupunguza madai
hayo hadi shilingi milioni 14.

VIJANA WAJITOSA KUFANYA USAFI MBALIZI

VIJANA wa Mji mdogo wa Mbalizi uliopo katika wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa, wanatarajia kufanya usafi katika mji huo kwa lengo la kuufanya mji huo kuwa safi na kuonesha uzalendo wao kwa nchi.

Taarifa iliyosainiwa na mratibu wa Vijana hao Gordon Kalulunga na kutumwa kwa vyombo vya habari jana, imesema kuwa dhumuni la usafi huo ni kuonesha uzalendo wao kwa taifa na kuwafanya vijana kutambua kuwa si kila jambo wanapaswa kulipwa.

‘’Kwa  Uzalendo wetu kwa nchi yetu bila kujali itikadi zetu za siasa wala dini na rangi zetu tumeamua kwa pamoja kufanya usafi wa mazingira katika mji wetu kwa kujitolea wenyewe bila ufadhili wa mtu yeyote na tutafanya hivyo kila mara’’ alisema Kalulunga.

Alisema kwa kuanzia watakutana kesho Jumatano eneo la Stendi ya Mbalizi huku kila mmoja akiwa na kifaa chake cha kufanyia usafi zikiwemo sululu, mifagio na koleo kisha watazibua mitalo na kufagia.

Kalulunga aliongeza kuwa baada ya hapo watafanya tathimini na kujiwekea malengo ya kufanya usafi kama huo katika eneo linguine na kwamba mwitikiowa vijana wa eneo hilo ni mkubwa na kwamba pia baadhi ya vijana kutoka Jiji la Mbeya wameomba na kuthibitisha kuwa watahusika kuonesha uzalendo wao kwa kujumuika na wenzao.

‘’Tukio hilo ni kubwa, tunaamini kwa kushirikiana na Serikali na wananchi wengine wazalendo tutashinda na kuiletea maendeleo jamii yetu na kutokomeza magonjwa yanayotokana na uchafu wa Mazingira na kwa kufanya hivyo tunaamini kila mmoja atatimiza wajibu wake kwa Taifa letu la Tanzania badala ya kutegemea kufanyiwa kila kitu na Serikali’’ alisema Kalulunga.

Aliongeza kuwa kabla ya zoezi hilo wametoa taarifa kwa viogozi wa Serikali akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkuu wa wilaya, Afisa Mtendaji wa kata ya Utengule Usongwe, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbalizi na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho.

Aliwaomba vijana wote ambao wapo tayari kushirikiana na wenzao bila malipo wajitokeze kufanya usafi huo na kujadiliana zaidi na wenzao kwa lengo moja la kuiletea maendeleo jamii na kuiepusha na magonjwa ya mlipuko kwa kufanya usafi katika maeneo watakayokubaliana na kuyabainisha.

Sunday, December 2, 2012

SAFARI YA MPENDWA WETU MAREHEMU CLEMENCE MPEPO.

Saturday, 1 December 2012

Kabla ya kuelekea Kanisani kwa ajili ya Sala ya mwisho ya kumwombea Marehemu Clemence Nurdin Lionge (Mpepo), ambaye safari yake ya mwisho mwili wake utahifadhiwa katika Nyumba yake ya milele katika Makaburi ya Segerea Jijini Dar es salaam.

Eee Mola ilaze roho ya Marehemu Clemence Mpepo mahali pema peponi Ameen.

MAADHIMISHO SIKU YA UKIMWI KWA JIJINI MBEYA YALIDOROLA UTASEMA SIYO JIJINI.HAMASA NDOGO IKASABABISHA WATU WASIHUDHURIE

 Kikundi cha wauzaji wa baa mbalimbali waliopewa elimu ya kujikinga na maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi VVU na shirika la Child Suport Tanzania


 Kikundi cha vijana wa kike waishio katika mazingira magumu cha jijini Mbeya




 Kikundi cha Kihumbe cha jijini Mbeya kikitumbuiza katika uwanja wa Ruanda Nzovwe



 Waliohudhuria wakicheza kwa pamoja kujifariji kwa kufika kwao wakiwa wachache

 Meza kuu ikitafakari baada ya kubaini mahudhurio ya watu ni kidogo tofauti na ilivyotarajiwa

Shughuli ilikosa mvuto kama unavyoweza kuona hapa