Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, May 20, 2014

CHATU MDOGO AKAMATWA,HOFU YATANDA ALIKO CHATU MKUBWA

Mganga wa Jadi Mazoea Hamisi(30) mkazi wa Chalinze mkoani Pwani(Kushoto) na msaidizi wake Athman Keneth(30) mkazi wa Chunya wakimwonesha chatu waliyemkamata HATIMAYE juhudi za kumsaka nyoka mkubwa aina ya Chatu anayesadikiwa kuwepo maeneo ya pembezoni mwa mto Meta jijini Mbeya zimeanza kuzaa matunda baada ya Chatu mdogo anayesadikiwa kuwa mtoto kukamatwa. Juhudi za kuanza kumsaka nyoka huyo zilianza siku chache baada ya mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mbeya kutoa taarifa ya tahadhari kwa wakazi juu ya uwepo wa nyoka huyo mkubwa katika eneo hilo na kuwataka wakazi kuwa makini wanapopita katika njia za mkato zilizopo kwenye maeneo anayotajwa kuonekana. Hatimaye leo juhudi za kumsaka chatu huyo zilionekana kuanza kuzaa matunda baada ya wataalamu ambao ni waganga wa jadi wakishirikiana na maafisa maliasili kutoka halmashauri ya kiji kufanikiwa kumnasa chatu mdogo anayesadikiwa kuwa ni mtoto wa chatu ambaye amekuwa akionekana. Majira ya asubuhi leo wataalamu hao wakiongozwa na Mazoea Hamisi(30) mkazi wa Chalinze mkoani Pwani wameweza kumnasa chatu mdogo katika waliyemkuta pembezoni mwa Mto Meta jirani na hoteli ya Rift Valley. Siku ya kwanza wataalamu hao waliweza kumsaka nyoka huyo walini hawakuweza kufanikiwa zaidi ya kubaini njia ambazo amekuwa akipita na dalili zikaonesha kuwa alipita jana yake na si siku nyingi. Alisema jioni yake baada ya kupumzika waliona waweke dawa za kienyeji ambazo zingeweza kumtoa mafichoni na kusogea karibu ambapo asubuhi waliwahi kuendelea kumtafuta. Alisema baada ya muda kidogo wakati akiendelea kufyeka vichaka lakini kwa bahati nzuri alimkanyaga chatu huyo na yeye kukurupuka ndipo alipofanikiwa kumkamata. Kwa mujibu wa mganga huyo ambaye anasaidiwa na Athman Keneth(30) mkazi wa Chunya mkoani hapa, Chatu aliyekamatwa ni mdogo na juhudi za kuendelea kumtafuta mkubwa zitaendelea kama kweli yupo. Alisema mara nyingi Chatu mdogo anapoonekana Mkubwa anakuwa amehama ili kuwapisha wadogo kuendelea na maisha yao ama huyo mdogo alisombwa na maji kipindi cha mvua kutoka kwenye hifadhi na wenzie.

Monday, May 19, 2014

HALMASHAURI YA JIJI YATOA AJIRA KWA MGANGA WA JADI KUMSAKA CHATU

Mganga wa Jadi Mazoea Hamis kutoka mkoani Pwani akitumia dawa zake kumsaka nyoka aina ya Chatu anayesadikiwa kuwepo kandokando ya mto Meta na kuhatarisha maisha ya wakazi wa maeneo ya jirani na wapita njia Hapa akionesha njia ambayo chatu huyo amekuwa akiitumia akiwa katika safari. Hapa akizungumza na waandishi wa habari waliofika eneo la tukio kushuhudia utafutaji wa nyoka huyo Waandishi wa habari wakiondoka eneo la tukio baada ya kuona jitihada za kumpata nyoka huyo zimegonga mwamba na kuacha harakati zikiendelea.

Friday, May 16, 2014

DENGUE ILIVYOLETA UBUNIFU BONGO

. HAPA NI SEBULENI AMBAPO WANAFAMILIA WANAPOTEZA MUDA MUDA WA JIONI KWA KUANGALIA LUNINGA NA KUNYWA VINYWA VYA AINA MBALIMBALI.WANAMINI KWA MAVAZI HAYA WAMEMUWEZA MBU AINA YA AEDES AENEZAE VIRUSI VYA UGONJWA WA DENGUE AMBO KWA SASA NDIYO GUMZO NCHINI HAIKUWEZA KUJULIKANA MARA MOJA IWAPO HAPA NI BAR AU NISEHEMU YA MKAHAWA.LAKINI HAPA NAPO WATEJA WANAMKWEPA MBU AINA YA AEDES KWA KUNYWA VINYWAJI NA KUANGALIA LUNINGA WAKIWA NDANI YA VYANDARUA.JIJINI MBEYA SERIKALI MKOANI HUMO IMETOA TAHADHARI KWA WAKAZI KUCHUKUA HATUA ZA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU. KATIBU TAWALA WA MKOA HUO MARIUM MTUNGUJA AMEWATAKA WAKAZI KUVAA MAVAZI MAREFU,KUONDOA MAZALIA YA MBU JIRANI NA MAKAZI NA PIA KUTOSITA KUTOA TAARIFA MARA MOJA IWAPO KUNA MTU ATAONEKANA KUWA NA DALILI ZA UGONJWA WA BENGUE. lAKINI KATIBU TAWALA HUYO AMESEMA BADO HAIJATHIBITIKA KAMA UGONJWA HUO USIO NA TIBA WALA KINGA IWAPO UMEBISHA HODI MKOANI MBEYA.

Thursday, May 15, 2014

AIBU HIII

Niseme tu ni aibu kubwa kwa taifa kama Tanzania ambalo ni juzi tu limetoka kuonesha namna lilivyowekeza katika suala la ulinzi wa mipaka,raia na mali zake katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano kwa mbwembwe za Vifaru,helkopta za kivita na nyingine nyingi inaonekana linashindwa kumteketeza mbu huyu anayeendelea kulitikisa taifa kwa kueneza homa ya Dengue

WACHIMBA DHAHABU WAMUUA MWENZAO KWA SURURU

MTU MMOJA RIZIKI SIAME @ NKOTA [30] MKAZI WA KIJIJI CHA PATAMELA ALIUAWA KWA KUPIGWA SULULU UTOSINI NA MDOMONI AKIWA NYUMBANI KWAKE. TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 14.05.2014 MAJIRA YA SAA 04:00HRS KATIKA KITONGOJI CHA SHULENI, KIJIJI CHA PATAMELA,KATA YA SAZA,TARAFA YA KWIMBA WILAYA YA CHUNYA. MAREHEMU ALIUAWA NA WATU WAWILI AKIWA NJE NYUMBANI KWAKE AMBAO NI 1. MOLANI MWASHILINDI [27] NA 2. STEPHEN SINGOGO [25] WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IGANDU, KATA YA MSIHA WILAYA YA MBOZI AMBAO WALIKIMBIA MARA BAADA YA KUFANYA TUKIO HILO. CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI ULIOTOKEA KATI YA MAREHEMU NA WATUHUMIWA KUGOMBEA PESA ZILIZOTOKANA NA MAUZO YA DHAHABU. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA INALETA ATHARI KUBWA KWA JAMII. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

Wednesday, May 14, 2014

ALBINO AUAWA KINYAMA HUKO SIMIYU,WAUAJI WAONDOKA NA VIONGO VYAKE

Matukio ya kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albino) yamezuka upya mkoani Simyu, ambapo mwanamke mmoja Mughu Lugata (40) mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) ameuawa kinyama kwa kukatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana pamoja na kutoweka na baadhi ya viungo vyake. Tukio hilo lililotokea katika kitongoji cha chalala kijiji cha Gasuma kata ya Nkololo wilayani Bariadi Mkoani hapa, marehemu alikatwa mguu wake wa kushoto sehemu ya goti, vidole 2 mkono wa kushoto pamoja ukucha wa kidole gumba , ambapo wahusika walitoweka na viungo hivyo. Akitoa taarifa mbele za waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani hapa Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12 usiku hadi saa moja asubuhi,wakati marehemu akiwa nyumbani kwake. “marehemu aliuawa na kiungo chake cha mguu wa kushoto kuchukuliwa kwa kukatwa sehemu ya goti, vidole 2 vya mkono wa kushoto ambavyo ni kidole cha 3 na 4,kukatwa na kuchuliwa na ukucha wa kidole gumba cha mkono wa kushoto na viungo vyote hivyo vilitoweka na wahusika wa mauaji hayo” Alisema Mkumbo. Alisema kuwa akiwa amelala nyumbani kwake peke yake mwanamke huyo alivamiwa na watu wasiojulikana na kuanza kumkatakata mapanga na kuchukua baadhi ya viungo vyake vya mwili na kutokomea navyo kusiko julikana . Aliongeza kuwa katika upelelezi wa awali wa jeshi hilo linawashikiria watu wawili ambao ni waganga wa kinyeji Gudawa Yalema (52) msukuma na mkulima wa kijiji hicho. Alimtaja mtuhumiwa mwingine kuwa ni Shiwa Masalu (Uselengi) naye mkazi wa kijiji hicho ambaye alikuwa pamoja na mtuhumiwa wa kwanza wakiwa na vifaa vya kupigia ramli, huku akieleza chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina. Mkumbo amewataka wananchi wenye taarifa juu ya wahusika wa tukio hilo kutoa taarifa hizo kwa jeshi hilo, ikiwa pamoja na kuwataka kutodanganyika kuwa utajiri unakuja kwa imani za kishirikina, bali unaletwa kwa kufanya kazi kwa bidii. Alisema kuna baadhi ya waganga wanawadanganya wateja wao kuwa viungo vya mlemavu wa ngozi vinaleta utajiri hali ambayo inawanafanya baadhi ya watu kuamini na kuendeleza mauaji ya Albino HABARI HII NI KWA HISANI YA MITANDAO MBALIMBALI

Monday, May 12, 2014

MUST WAZINDUA MPANGO WA KUHAMASISHA WANAWAKE KUSOMA MASOMO YA UHANDISI,SAYANSI NA TEKNOLOJIA(WITED)

.Hizi ni baadhi ya kazi za kitaalamu zilizofanywa na wanafunzi wanawake katika chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST).Kazi hili zilioneshwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa kuhamasisha wanawake kusoma masomo ya Uhandisi,Sayansi na Teknolojia Albertina Leonard Mwenyekiti WITTED na mkufunzi idara ya sayansi na biashara akisoma taarifa fupi ya mpango wa WITED Naibu Makamu wa chuo cha MUST idara ya Taaluma,Utafiti na ushauri Dk Noel Mbonde ambaye alisema bado chuo hicho kinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wanafunzi wa kike kutokana na jamii kujengeka katika fikra ya mafunzo ya ufundi ni ya wanaume. Alisema kwa sasa kati ya wanafunzi 3442 waliopo chuoni hapo wanafunzi wa kike ni 640 pekee aliosema kati yao 533 wanachukua stashahada huku wengine 107 wakiwa wanachukua shahada. Mkurugenzi msaidizi Wizara ya Sayansi na Tknolojia idara ya Sayansi na Ubunifu Dk.Magreth Komba aliwataka walimu wa masomo ya sayansi kuwa wabunifu wa mbinu mbadala za ufundishaji masomo hayo ili wanafunzi hususani wanawake wasiyakimbie