Monday, May 12, 2014
MUST WAZINDUA MPANGO WA KUHAMASISHA WANAWAKE KUSOMA MASOMO YA UHANDISI,SAYANSI NA TEKNOLOJIA(WITED)
.Hizi ni baadhi ya kazi za kitaalamu zilizofanywa na wanafunzi wanawake katika chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST).Kazi hili zilioneshwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa kuhamasisha wanawake kusoma masomo ya Uhandisi,Sayansi na Teknolojia
Albertina Leonard Mwenyekiti WITTED na mkufunzi idara ya sayansi na biashara akisoma taarifa fupi ya mpango wa WITED
Naibu Makamu wa chuo cha MUST idara ya Taaluma,Utafiti
na ushauri Dk Noel Mbonde ambaye alisema bado chuo hicho kinakabiliwa na
changamoto ya uhaba wa wanafunzi wa kike kutokana na jamii kujengeka
katika fikra ya mafunzo ya ufundi ni ya wanaume.
Alisema kwa sasa kati ya wanafunzi 3442 waliopo chuoni hapo wanafunzi
wa kike ni 640 pekee aliosema kati yao 533 wanachukua stashahada huku
wengine 107 wakiwa wanachukua shahada.
Mkurugenzi msaidizi Wizara ya Sayansi na Tknolojia idara ya Sayansi na
Ubunifu Dk.Magreth Komba aliwataka walimu wa masomo ya sayansi kuwa wabunifu wa mbinu mbadala za ufundishaji masomo hayo ili wanafunzi hususani wanawake wasiyakimbie
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment