Alianza Meneja wa kiwanda hicho Nicholaus Kanyamala kama anavyoonekana hapa
Akafuata mfanyakazi mmoja baada ya mwingine.Huyu ni Stela Alexanda
Wakafuata wafanyakazi wengine pamoja na wakazi wa kata jirani na kiwanda yaani Sisitila na Ikuti
Kama ilivyo kawaida katika kupima HIV kila mmoja katika foleni ya kuingia kwa mnasibu/mshauri nasaha alikuwa akijiuliza majibu yatakuwaje.Kijasho chembamba kikawa kinamtoka kila mmoja.
Baada ya kupima na kupokea majibu Meneja wa kiwanda akaona umuhimu wa kuzungumza na wawakilishi wa vyombo vya habari
Mazungumzo ya Meneja yakamvuta mwakilishi wa kituo cha Luninga cha STAR TV Husna Mlanzi na kuamua kupima pia kama alivyoamua Hosea Cheyo wa TBC ambaye hayupo pichani.
Hakupenda kwa wakati huo apokee simu yoyote ile.Akaamua kuizima simu yake kabisaaaa.
Kupima si tatizo sana,kungoja majibu ndiyo kazi.Husna akaanza kuwaza damu tayari imechukuliwa je majibu yangu yatakuwaje?
Hamasa ya kupima ikamkuna mmiliki wa blogu ya Lyamba Lya Mfipa.Akaamua kuingia ulingoni.Ni baada ya kujiuliza iwapo watu wote wamepima ninachoogopa ninini.Na kama ni majibu si yatakuwa mali yangu bila kujalisha ni mazuri au mabaya.
Swali la kujiuliza ni je wewe unasubiri nini kuijua afya yako?Tambua Tanzania bila maambukizi mapya inawezekana!Hongera TBL Mbeya
Shughuli ikafungwa rasmi ambapo zaidi ya watu 190 wamepima ikiwa ni mpango wa kiwanda cha bia cha TBL mkoani Mbeya kama maandalizi ya siku ya ukimwi duniani ambayo kimkoa yatafanyika desemba mosi wilayani Mbozi.
Friday, November 30, 2012
BREAKING NEWZZZZZZZZ
ASKARI WA JWTZ WANNE KATI YA 10 WALIOKAMATWA KWA MAUAJI YA KIJANA MBALIZI LEO WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI
Wednesday, November 28, 2012
ASKARI Polisi wilayani Momba mkoani Mbeya wamefanikiwa kumnusuru
Mkuu wa wilaya hiyo Abiud Saudea na jopo lake baada ya kuzingilwa na wananchi
wa Kijiji cha Kamsamba.
Hali hiyo ilijitokeza kuazia majira ya saa Nane mchana leo baada
ya Mkuu hyo wa wilaya kufika kijijini hapo na kuanza kuhutubia huku viongozi hao
wa wilaya wakikusudia kumrejesha madarakani Mwenyekiti wa Kijiji hicho Vitus
Sauzen aliyetimuliwa kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha.
Hali hiyo iliwakera wananchi na kuanza kuzomea jambo ambalo
lilizusha vurugu mbele ya Mkuu huyo wa wilaya, kamanda wa polisi wa wilaya hiyo
(OCD) na viongozi wengine.
Kutokana na fujo hizo, askari polisi waliingilia kati na
kuwatawanya wnanchi na mabomu ya machozi hali ambayo haikufua dafu na kuamua
kutumia risasi za moto ambazo zimejeruhi watu watatu ambao wamekimbizwa Hospitali
ya wilaya ya Mbozi mkoani hapa.
Mbali na hao watu wanne wamekamatwa kwa kuhusika na uratibu wa
fujo hizo wakiwemo viongozi wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) katika kata na kijiji hicho cha Kamsamba.
Waliokamatwa na Polisi ni pamoja na Richard Nyoni, Michael
Simfukwe ambao ni viongozi wa Chadema. Wengine ni Jofrey Dismas na Sabati
Kigaya.
KIFO CHA MTANGAZAJI CLEMENCE MPEPO
TASINIA ya habari mkoani
Mbeya imepata pigo kufuatia kifo cha mtangazaji Clemence Mpepo(Mzee wa
Makabila) wa kituo cha redio cha Bomba FM cha jijini Mbeya.
Mpepo alifariki usiku wa
kuamkia Novemba 28 mwaka katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es
salaam alikokuwa amelazwa akiendelea kupata matibabu kufuatia maradhi ya mapafu
yaliyokuwa yakimsumbua.
Enzi za uhai wake mtangazaji
huyo alijipatia umaarufu mkubwa kwa mashabiki mkoani hapa na maeneo ya jirani
kufuatia umahiri wake wa kutangaza kipindi cha nyimbo za asili ambapo alikuwa
mtaalamu wa lugha za makabila mbalimbali hali iliyokuwa ikiwavutia wasikilizaji
wengi wa kipindi hicho kilichokuwa kikirushwa kila siku ya jumamosi.
Akizungumzia kifo hicho
Meneja wa redio Bomba Fredy Helbert alisema ofisi imepokea kifo hicho kwa
masikitiko makubwa kutokana na ushirikiano mkubwa aliokuwa nao Mpepo mpaka
anaanza kusumbuliwa na maradhi.
Alisema marehemu alianza
kuugua siku chache baada ya kufunga ndoa hivi karibuni akiwa bado katika likizo
ya ndoa na baadaye hali ilizidi kuwa mbaya na kulazwa katika hospitali ya Mkoa
na hatimaye Rufaa Mbeya kabla ya kupelekwa Muhimbili.
“Alikuwa bado katika likizo
ya ndoa hivyo hata kazini alikuwa hajaanza kuingia ndipo maradhi yalipoanza
kumsumbua.Jambo lililokuwa likitupa matumaini kuwa mpaka anaondoka na mkewe
kwenda Dar es salaam alikuwa na unafuu mkubwa.Alikuwa akizungumza vizuri na kucheka
nasi kama tulivyokuwa tumemzoea.Ghafla
tukapata taarifa hali imebadilika na leo tunazungumza msiba”.
“Ni masikitiko makubwa kwetu kama wafanyakazi wenzake.Hakuwa mtu wa kukorofishana na
mtu.Mcheshi wakati wote Lakini kikazi pia japo siku hizi watu wanasema pengo
linazibika kwa Mpembo kwakweli ni vigumu maana utangazaji wake ulikuwa si wa
kipindi kimoja.Kila kipindi tulichompa kilipata wasikilizaji wengi” alisema.
Kwa mujibu wa meneja huyo
Mpepo atazikwa siku ya jumamosi Kinyelezi jijini Dar es salaama kutokana na
maamuzi ya wazazi wake.
MTANGAZAJI WA REDIO BOMBA FM CLEMENCE MPEPO AFARIKI DUNIA
TANGAZO: KWA MASIKITIKO MAKUBWA UONGOZI WA REDIO BOMBA FM, TUNATANGAZA KIFO CHA MFANYAKAZI WETU CLEMENCE MPEPO "MZEE WA MAKABILA" ALIYEFARIKI USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI. KWA TAARIFA ZAIDI TUTAENDELEA KUWAFAHAMISHA JUU YA UTARATIBU WA MAZISHI NA PIA ENDELEA KUSIKILIZA REDIO
.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO
VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE
28/11/2012.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI
YA GARI KUACHA NJIA KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI
MNAMO TAREHE 27.11.2012 MAJIRA YA SAA 19:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI
CHA IGAWILO BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA
MBEYA . GARI T.597 BVZ SCANIA LORI LIKIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE BADO
HAJAFAHAMIKA LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA VIFO VYA WATU
WAWILI AMBAO BADO HAWAJAFAHAMIKA MAJINA WALA MAKAZI
JINSIA KIUME UMRI KATI YA MIAKA 30-35 NA MAJERAHA KWA WATU WAWILI 1. DAVI S/O MIROYI, MIAKA 18 MKAZI WA DSM NA 2. MWANSU S/O ADAM, MIAKA 28, MMAKONDE MKAZI
WA MTWARA AMBAO WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA
MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI. MIILI
YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA
WITO KWA MADEREVA KUWA NA TAHADHARI YA MATUMIZI YA BARABARA KWA KUZINGATIA
SHERIA ZA USALAMA BARABARANI. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUFIKA
HOSPITALINI HAPO ILI KUTAMBUA MIILI YA MAREHEMU HAO NA KWA MTU/WATU
WENYE TAARIFA JUU YA ALPOKIMBILIA DEREVA HUYO AZITOE POLISI ILI AKAMATWE
VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
ASKARI POLISI AMBAYE HAKUFAHAMIKA JINA WALA NAMBA YAKE ALIPOKUTWA NA Lyamba Lya Mfipa JIRANI NA HOTELI YA MBEYA PEACK JIJINI MBEYA AKICHORA CHINI
ALIANZA HIVI
AKAENDELEA NAMNA HII
HAKUISHIA HAPO AKAZIDI KUENDELEA
AKAMALIZA KAZI YAKE NA KISHA AKAONDOKA
AKAENDELEA NAMNA HII
HAKUISHIA HAPO AKAZIDI KUENDELEA
AKAMALIZA KAZI YAKE NA KISHA AKAONDOKA
Tuesday, November 27, 2012
MTOTO ALIYECHOMWA MKONO NA HATIMAE KUKATWA MKONO WAKE WA KUSHOTO ALETWA MAHAKAMANI KUTOA USHAHIDI
MTOTO ANETH KATIKATI NA MAMA YAKE KULIA WAKIINGIA ENEO LA MAHAKAMANI LEO |
WILVINA MKANDALA ANAETUHUMIWA KWA KUMUUNGUZA NA KUSABABISHA KUKATWA KWA MKONO WA MTOTO ANETH AKIINGIZWA MAHAKAMANI HUKU AKIWA HATAKI KABISA KUPIGWA PICHA |
WAKAZI WENGI WA JIJI LA MBEYA NA VITONGOJI VYAKE WAMEJITOKEZA KWA WINGI KUJA SIKILIZA KESI HIYO |
MTOTO ANETH AKISALIMIANA NA MAMA ALIYEMUHUDUMIA HOSPITALINI KABLA YA MAMA YAKE MZAZI KUJA TOKA BUKOBA |
MTOTO ANETH MARA TU BAADA YA KUTOKA KATIKA CHUMBA CHA MAHAKAMA AKISUBIRI KURUDISHWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA KUENDELEA NA MATIBABU |
HUKU AKINA MAMA WAKIWA NA JAZBA YA KUTAKA HAKIMU AWAACHIE KIDOGO JAPO KWA DAKIKA TANO WAMFUNZE ADABU MTUHUMIWA HUYO KWANI WANADAI AMEWADHALILISHA SANA KWA KITENDO HICHO CHA KUMTESA MTOTO ANETH |
KWA HISANI YA BLOGU YA MBEYA YETU |
NEWZZZZZZZZZ
TUNAZIDI KUKULETEA HUDUMA KARIBU.SIKILIZA LIVE MATANGAZO YANAYORUSHWA KILA SIKU NA KITUO CHA REDIO CHA BOMBA FM CHA JIJINI MBEYA
NI WAKATI WAKO PIA KUTANGAZA NA LYAMBA LYA MFIPA SASA
NI WAKATI WAKO PIA KUTANGAZA NA LYAMBA LYA MFIPA SASA
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO
VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE
27/11/2012.
WILAYA YA MBARALI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA
KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO
MNAMO TAREHE 26.11.2012 MAJIRA YA 14:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MLANGALI BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI
DFP 7322 AINA YA NISSAN PATROL MALI YA BARAZA LA KILIMO DSM LIKIENDESHWA
NA DEREVA JACKSON S/O PAUL LIKITOKEA MBEYA KUELEKEA IRINGA ILIMGONGA
MTEMBEA KWA MIGUU AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE JINSIA
YA KIUME MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 25- 30 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
PAPO HAPO . CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
KATIKA HOSPITALI YA MISSION CHIMALA. DEREVA AMEKAMATWA. TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA NA
TAHADHARI YA MATUMIZI YA BARABARA KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.
AIDHA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA ENEO HILO KUFIKA HOSPITALINI HAPO ILI
KUUTAMBUA MWILI WA MAREHEMU.
WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA
MOSHI [GONGO]
MNAMO TAREHE 25.11.2012 MAJIRA YA SAA 21:20HRS HUKO KATIKA KIJIJI
CHA ITINDI – MALEZA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. POLISI WAKIWA
DORIA WALIMKAMATA MWASHI D/O LUGWISHA,MIAKA 25, MSUKUMA,MKULIMA MKAZI
WA SAZA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5 . MTUHUMIWA
NI MUUZAJI NA MNYWAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUJIEPUSHA NA MATUMIZI YA POMBE
HARAMU KWANI NI HATARI KWA AFYA YAO NA NI KINYUME CHA SHERIA.
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] NA
MTAMBO WA KUTENGENEZEA
MNAMO TAREHE 26.11.2012 MAJIRA YA SAA 17:20HRS HUKO MPINDO BULYAGA
– TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. POLISI WAKIWA
DORIA WALIMKAMATA WALLACE S/O MSAMATI ,MIAKA 60, MMAKUA ,MKULIMA MKAZI
WA MPINDO BULYAGA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO
WA LITA 1 NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO . MTUHUMIWA
NI MUUZAJI NA MNYWAJI WA POMBE. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUJIEPUSHA NA MATUMIZI YA POMBE HARAMU KWANI NI
HATARI KWA AFYA YAO NA NI KINYUME CHA SHERIA.
Signed By,
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Monday, November 26, 2012
MAZISHI YA MAMA ALIYEUAWA KWA KUPIGWA NA MWANAE
Akina mama waombolezaji wakisawazisha kaburi la marehemu Sinjembele Julius(62) aliyeuawa kwa kupigwa na mwanae Ndele Julius(25)
Baadhi ya waombolezaji wakishuhudia mazishi ya Sinjembele yaliyofanyika Nyumbani kwake katika kitongoji cha Igawilo kata ya Swaya Mbeya
Kaburi baada ya kuzikwa marehemu
Baadhi ya waombolezaji wakishuhudia mazishi ya Sinjembele yaliyofanyika Nyumbani kwake katika kitongoji cha Igawilo kata ya Swaya Mbeya
Kaburi baada ya kuzikwa marehemu
Sunday, November 25, 2012
MATUMIZI HARAMU YA CHANDARUA
Vijana wakazi wa kijiji cha Kirando wilayani Nkasi mkoani Rukwa wakivua samaki wadogo katika ziwa Tanganyika kwa kutumia Chandarua kama walivyokutwa na Lyamba Lya Mfipa hivi karibuni.Hapa Chandarua(Mosquito Net) kimebadilishwa matumizi badala ya kumkinga binadamu asing'atwe na mbu akiwa amelala kinatumika kama nyenzo ya uvuvi.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO
VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE
26/11/2012.
WILAYA YA MBEYA MJINI - MAUAJI
MNAMO TAREHE 25/11/2012 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO SWAYA JIJI NA
MKOA WA MBEYA. SINJEMBELE W/O JULIUS, MSAFWA, 62YRS, MKULIMA NA
MKAZI WA SWAYA ALIFARIKI DUNIA NYUMBANI KWAKE BAADA YA KUSHAMBULIWA
KWA MATEKE NA NGUMI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTOTO WAKE
AITWAYE NDELE S/O JULIUS. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMSHAMBULIWA KWA MATEKE
NA NGUMI NA KUPELEKEA MAUMIVU MAKALI YALIYOSABABISHA KIFO CHAKE. CHANZO
NI UGOMVI ULIOKUWEPO BAINA YA MTUHUMIWA NA KIJANA MWENZAKE NA NDIPO
MAMA ALIPOKWENDA KUAMULIA NA MTUHUMIWA KUMGEUKIA MAMA YAKE. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA
MARA BAADA YA TUKIO HILO. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA TABIA YA KURUHUSU HASIRA ZIWATAWALE NA
KUFANYA MAAMUZI YANAYOWEZA KUSABABISHA MADHARA MAKUBWA BADALA YAKE BUSARA
ITUMIKE. AIDHA ANATOA WITO KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA MAHALI
ALIKO MTUHUMIWA WAZITOE ILI AKAMATWE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA
KWENYE MAMLAKA HUSIKA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed By
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Saturday, November 24, 2012
NYUMBA ZA WALIMU KYELA HOIIII
Moja ya nyumba za walimu katika shule ya msingi Ipyana wilayani Kyela mkoani MbeyaHali ya nyumba za walimu katika shule hiyo ni mbaya kama inavyoonekana hapa
Chini ni dirisha la nyumba hiyo likiwa limefunguliwa
VODACOM WAPATA AJALI MBEYA
Kwa hisani ya Blogu ya Mbeya Yetu |
Thursday, November 22, 2012
MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Norman Sigala akiwasaidia mafundi wanaojenga daraja la Itiji jijini Mbeya kupika
Mmiliki wa blogu ya Lyamba Lya Mfipa akifanyiwa vipimo
Mbele ni baadhi ya wabunge wa mkoani Mbeya wakiwa katika moja ya
mikutano mikubwa mkoani hapa.Kutoka kulia ni Aliko Kibona(Ileje),Mary
Mwanjelwa(Viti maalumu CCM),Mchnungaji Luckson Mwanjala(Mbeya V) na
Godfray Zambi(Mbozi Mashariki).
Mmiliki wa blogu ya Lyamba Lya Mfipa akifanyiwa vipimo
Mbele ni baadhi ya wabunge wa mkoani Mbeya wakiwa katika moja ya
mikutano mikubwa mkoani hapa.Kutoka kulia ni Aliko Kibona(Ileje),Mary
Mwanjelwa(Viti maalumu CCM),Mchnungaji Luckson Mwanjala(Mbeya V) na
Godfray Zambi(Mbozi Mashariki).
Wednesday, November 21, 2012
JWTZ 10 MBARONI KWA MAUAJI
WATU 14 wakiwemo askari 10 wa jeshi la wananchi(JWTZ) wa kikosi cha 44KJ kambi yaa Mbalizi wilayani Mbeya wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa tuhuma za mauaji.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athuman amesema leo kuwa kushikiliwa kwa askari hao kunatokana na mauaji ya kijana Petro Sanga(25) yaliyotokea novemba 18 mwaka huu akiwa katika baa ya Power Pub ambapo askari hao wanatuhumiwa kuhusika
Tuesday, November 20, 2012
LIGI YA MWENYEKITI YAMALIZIKA
MICHUANO ya ligi ya
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya imemalizika kwa timu ya kata ya Halungu
kunyakua ubingwa baada ya kuifunga timu ya kataa ya Ndalambo goli 2-1.
Halungu iliibuka bingwa wa
mashindano hayo na kuzawadiwa kombe la fedha taslimu shilingi laki tatu katika
mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Vwawa ambapo hadi dakika 90 za mwanzo
zinamalizika timu hizo zilikuwa sare ya goli 1-1.
RUNGWE WAJIPANGA KWA USAFI WA MAZINGIRA
SERIKALI wilayani Rungwe
mkoani Mbeya imesema imejipanga kuhakikisha hali ya usafi wa mazingira
inazingatia katika maeneo yote wa wilaya hiyo kwa kuanza kuwawajibisha
wasiofuata utaratibu uliopo.
Mkuu wa wilaya hiyo Chrispin
Meela aliyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani
yaliyofanyika kitaifa juzi katika mji mdogo wa Tukuyu wilayani hapa.
Subscribe to:
Posts (Atom)