Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, November 28, 2012


ASKARI Polisi wilayani Momba mkoani Mbeya wamefanikiwa kumnusuru Mkuu wa wilaya hiyo Abiud Saudea na jopo lake baada ya kuzingilwa na wananchi wa Kijiji cha Kamsamba.
Hali hiyo ilijitokeza kuazia majira ya saa Nane mchana leo baada ya Mkuu hyo wa wilaya kufika kijijini hapo na kuanza kuhutubia huku viongozi hao wa wilaya wakikusudia kumrejesha madarakani Mwenyekiti wa Kijiji hicho Vitus Sauzen aliyetimuliwa kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha.
Hali hiyo iliwakera wananchi na kuanza kuzomea jambo ambalo lilizusha vurugu mbele ya Mkuu huyo wa wilaya, kamanda wa polisi wa wilaya hiyo (OCD) na viongozi wengine.
Kutokana na fujo hizo, askari polisi waliingilia kati na kuwatawanya wnanchi na mabomu ya machozi hali ambayo haikufua dafu na kuamua kutumia risasi za moto ambazo zimejeruhi watu watatu ambao wamekimbizwa Hospitali ya wilaya ya Mbozi mkoani hapa.
Mbali na hao watu wanne wamekamatwa kwa kuhusika na uratibu wa fujo hizo wakiwemo viongozi wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kata na kijiji hicho cha Kamsamba.
Waliokamatwa na Polisi ni pamoja na Richard Nyoni, Michael Simfukwe ambao ni viongozi wa Chadema. Wengine ni Jofrey Dismas na Sabati Kigaya.

No comments:

Post a Comment