MHANDISI wa barabara katika
halmashauri ya wilaya ya Mbeya Jesse Shengena huenda akawajibishwa kwa
kusimamishwa kazi iwapo atashindwa kusimamia ujenzi wa barabaya ya Iwiji-Izyira
kwa kiwango cha changarawe katika kipindi cha mwezi mmoja.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro ametoa muda huo leo baada ya kutembelea barabara hiyo yenye urefu wa
kilometa sita na kukuta imejengwa kwa kiwango cha vumbi badala ya Changarawe kama mhandisi huyo alivyotoa taarifa kwake na LYAMBA LYA MFIPA imeshuhudia.
Awali mhandisi Shengena
alisema barabara hiyo imefanyiwa ukarabati kwa kuwekwa changarawe na kampuni ya
Kalambo Civil and Building work ya mkoani Mbeya kwa gharama ya zaidi ya
shilingi milioni 65 na hadi sasa amekwishalipwa zaidi ya milioni 48.
Hata hivyo mkuu wa mkoa
Kandoro hakuridhishwa na ukarabati uliofanyika na kumtaka mhandisi huyo
kuhakikisha barabara hiyo inarudiwa kwa kufanyiwa ukarabati kwa kiwango cha
changarawe katika kipindi cha mwezi mmoja vinginevyo atawajibishwa kwa
kusimamishwa kazi