Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, September 3, 2012

DIWANI ACHUKUWA FOMU KUGOMBEA NEC


Akizungumza na LYAMBA LYA MFIPA, Sabil alikishukuru chama chake kwa
kuchukua maamuzi ya kurejesha nafasi ya Unec katika ngazi za wilaya
akisema kutasaidia kuijenga CCM zaidi kuwa na wawakilishi kutoka ngazi
hiyo tofauti na kuishia kuwa na mwakalishi ngazi ya mkoa pekee.

Alisema kwa kuwa na uwakilishi wa mkoa pekee kulikibana chama ngazi ya

wilaya kujifunza mambo mengi kupitia mikutano mikuu ya kitaifa hivyo
sasa itakuwa fursa ya kipekee.

Alisema anaamini iwapo atapata nafasi hiyo atakiwezesha chama wilayani

kwake kwakuwa atakapokuwa akizungumza katika mikutano ya kitaifa
ataweza kupeleka pia changamoto za wilayani kwake na hatimaye
kujadiliwa kwa upana zaidi na kutafutiwa ufumbuzi.

“Na pia unapokuwa katika mikutano hiyo kuna mambo unajifunza ya

unapoyaleta kwenu hali inayosaidia kukijenga chama wilayani kwako na
pia unakuwa umekijenga kitaifa.Maana unapozungumzia chama taifa ni
lazima kuwa kinaanzia huku hivyo tunapokuwa na msingi imara huku ndiyo
mafanikio ya kitaifa” alisema.

Sabil ambaye ni diwani wa mwanamke pekee aliyepata nafasi kwa

kuchaguliwa kati ya kata zote wilayani hapa alisema amewahi kuwa
diwani wa viti maalumu na hatimaye akagombea na kuwa wa kuchaguliwa na
sasa anataka nafasi ya Unec.

Hata hivyo alisema si mara yake ya kwanza kugombea nafasi hiyo bali

kupitia mkoa mwaka 2002 aligombea lakini kura hazikutosha na mwaka
2007 pia akagombea hazikutosha lakini zikaongezeka tofauti na mwaka wa
kwanza.

Alisema nia anayo na amechukua fomu akiwa na uhakika wa kushinda

kwakuwa ana imani ataungwa mkono na wanachama wenzake ili awawakilishe
japo kushinda na kushindwa ni matokeo ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment