Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, September 28, 2012

MHANDISI MBEYA KUTIMULIWA KAZI


MHANDISI wa barabara katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya Jesse Shengena huenda akawajibishwa kwa kusimamishwa kazi iwapo atashindwa kusimamia ujenzi wa barabaya ya Iwiji-Izyira kwa kiwango cha changarawe katika kipindi cha mwezi mmoja.
             
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ametoa muda huo leo baada ya kutembelea barabara hiyo yenye urefu wa kilometa sita na kukuta imejengwa kwa kiwango cha vumbi badala ya Changarawe kama mhandisi huyo alivyotoa taarifa kwake na LYAMBA LYA MFIPA imeshuhudia.

Awali mhandisi Shengena alisema barabara hiyo imefanyiwa ukarabati kwa kuwekwa changarawe na kampuni ya Kalambo Civil and Building work ya mkoani Mbeya kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 65 na hadi sasa amekwishalipwa zaidi ya milioni 48.

Hata hivyo mkuu wa mkoa Kandoro hakuridhishwa na ukarabati uliofanyika na kumtaka mhandisi huyo kuhakikisha barabara hiyo inarudiwa kwa kufanyiwa ukarabati kwa kiwango cha changarawe katika kipindi cha mwezi mmoja vinginevyo atawajibishwa kwa kusimamishwa kazi

No comments:

Post a Comment