Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, July 26, 2016

KOMBE LA SHIRIKISHO | BARANI | AFRIKA | 2015 - 2016.


Medeama SC Vs Yanga SC | KUNDI A.
Uwanja - Sekondi Sports.
Muda - saa 11 : 50 Jioni.

>>>>>>>>>>>> KIKOSI CHA YANGA LEO.<<<<<<<<<<<<<<<<
1. Deogratius Bonaventura Munishi - 30.
2.Juma Jafarry Abdul - 12.
3.Oscar Fanuel Joshua - 03.
4.Kelvin Patrick Yondani - 04.
5.Nadir Haroub Ally - 23 ( C ).
6.Mbuyu Twite Jnr - 06.
7.Saimon Happygod Msuva - 27.
8.Thaban Michael Kamusoko - 13.
9.Obrey Cholla Chirwa - 07
10.Donald Dombo Ngoma - 11.
11.Haruna Fadhil Niyonzima - 08.

AKIBA.
Ally Mustafa Barthez - 01.
Vicent Andrew Dante - 28.
Said Juma Makapu - 22
Pato George Ngonyani - 15.
Juma Mahadhi Neymar - 21
Amiss Jocelyn Tambwe - 19
Malimi Marcel Busungu - 16

MUNGU IBARIKI YANGA. .
MUNGU IBARIKI TANZANIA.

SUGU AKOSOLEWA MBEYA

Na,Christopher Nyenyembe,Mbeya
 
SHIRIKISHO la vyama vya siasa mkoa wa Mbeya limetoa tamko la kulaani kitendo cha utovu wa nidhamu kilichoonyeshwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini,Joseph Mbilinyi  cha kuonyesha ishara ya kidole ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulikosababisha apewe adhabu ya kutoshiriki vikao 10.
 
Mwenyekiti wa shirikisho hilo,Godfrey Mwandulusya alitoa tamko hilo jana kwa niaba ya vyama vingine alipokuwa akizungumza na Wanahabari kuwa viongozi wa vyama vinavyounda umoja huo wamefikia uamuzi wa kulaani tukio hilo kwa misingi ya kuimarisha demokrasia ya kweli na kumtaka Mbunge huyo awaombe radhi wananchi wa jimbo lake na hususani mkoa huo kwa ujumla wa madai ameshiriki kuwadhalilisha.
 
Mwandulusya alisema kuwa kitendo cha ‘Sugu’ kuonyesha kidole ndani ya bunge ni cha utovu mkubwa wa nidhamu na hakikupaswa kufanywa na mbunge aliyechaguliwa kwa kura nyingi na wananchi ambao walimuamini kama kiongozi bora na wa mfano kwa tabia njema kumbe ni kinyume na matarajio yao.
 
“Kitendo cha kumuonyesha kidole Naibu Spika , Ackson Tulia kimewadhalilisha wanawake wote,anapaswa kuwaomba radhi wakazi wa jimbo lake ,mkoa anaotoka na watanzania wote hasa ikizingatiwa kuwa ishara hiyo ni tusi kubwa lisiloweza kutamkwa hadharani” alisema Mwenyekiti wa shirikisho hilo.
 
Alisema kwa pamoja viongozi wa shirikisho la  vyama vya siasa walioketi na kutafakari adhabu aliyopewa ya kutokushiriki vikao 10 hakutakuwa na maana yoyote kama mbunge huyo hawezi kujitokeza hadharani na kuwaomba radhi wananchi waliomchagua kwa lengo la kuwarudishia imani na jinsi walivyokipenda chama anachotoka cha Chadema.
 
Alisema kuwa mamlaka iliyomdhamini na kumpa nafasi ya kugombea ubunge ambayo ni chama chake cha Chadema kinapaswa kuliona hilo kwa vile sehemu kubwa ya wananchi walioshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 walikuwa na kiu kubwa ya kuhitaji mabadiliko na hawakustahili kuangushwa ndio maana umoja huo umeamua kutoa tamko.
 
Licha ya kumtaka Mbunge huyo kuomba radhi pia umoja huo ulipinga uamuzi wake wa  kwenda kulalamika kwa viongozi wa dini kwa madai kuwa upinzani umekuwa hautendewi haki ndani ya bunge kumbe alistahili kwanza kujisafisha kwa wananchi kwa kuwaomba radhi ili azidi kuaminika na si vinginevyo.
 
Mwenyekiti huyo alivitaja vyama nane vinavyounda shirikisho hilo katika mkoa wa Mbeya ni APPT-Maendeleo,UDP,TLP,UPDP,NLD,NCCR-Mageuzi,CUF na DP na kudai kuwa umoja huo umekuwa imara ili kuongeza nguvu ndani ya mkoa huo licha ya vyama vitatu vya NCCR-Mageuzi,NLD na CUF kujiunga na Ukawa.